Mkutano Mkuu
Tumaini katika Kristo
Mkutano mkuu wa Aprili 2021


Tumaini katika Kristo

Tunatamani kuwasaidia wale wote wanaohisi wapweke au kuhisi kutokuwa sehemu ya kundi. Naomba nitaje, hasa, wale ambao kwa sasa hawajaoa wala kuolewa.

Akina Kaka na dada, katika wakati huu wa Pasaka tunafokasi katika Ufufuko mtukufu wa Bwana na Mwokozi wetu Yesu Kristo. Tunakumbuka mwaliko wake wa upendo wa “Njooni kwangu, ninyi nyote msumbukao na wenye kulemewa na mizigo, nami nitawapumzisha.

“Jitieni nira yangu, mjifunze kwangu; kwa kuwa mimi ni mpole na mnyenyekevu wa moyo; nanyi mtapata raha nafsini mwenu.

“Kwa maana nira yangu ni laini, na mzigo wangu ni mwepesi.”1

Mwaliko wa Mwokozi wa kumfuata Yeye ni mwaliko kwa wote ambao si tu mwaliko wa kumfuta Yeye bali pia kuwa wa Kanisa Lake.

Kwenye aya iliyotangulia mwaliko huu wa upendo, Yesu anafundisha jinsi hii inavyofanywa kwa kutafuta kumfuata Yeye. Alitangaza, “Hakuna mwanaume [au mwanamke] amjuaye Mwana, ila Baba; wala hakuna mwanaume yeyote [au mwanamke] amjuaye Baba, ila Mwana, na kwa mwanaume [au mwanamke] yeyote ambaye Mwana apenda kumfunulia.”2

Yesu anatutaka tufahamu kuwa Mungu ndiye Baba wa Mbinguni mwenye upendo.

Kufahamu kuwa tunapendwa na Baba yetu wa Mbinguni kutatusaidia kufahamu sisi ni nani na kufahamu kuwa sisi ni wa familia Yake kubwa ya milele.

Kliniki ya Mayo hivi karibuni ilisema: “Kuwa na hisia ya kwamba u sehemu ya ni muhimu sana. … Karibu kila sehemu ya maisha yetu imewekwa katika hali ya kuwa sehemu ya.” Ripoti hii inaongeza, “Hatuwezi kutenganisha umuhimu wa hisia ya kuwa sehemu ya kitu fulani mbali na afya yetu ya mwili na akili.”3—na, naongezea, afya yetu ya kiroho.

Jioni ile kabla ya kuteseka kwake Gethsemane na kifo msalabani Mwokozi alikutana na wafuasi wake kwa ajili ya Chakula cha Jioni cha Mwisho. Aliwaambia, “Ulimwenguni mnayo dhiki: lakini jipeni moyo; mimi nimeushinda ulimwengu.”4 Kabla ya machweo siku iliyofuata, Yesu Kristo alikuwa ameteseka na alikuwa “amekufa [msalabani] kwa ajili ya dhambi zetu.”5

Najiuliza ni upweke wa jinsi gani wanawake na wanaume wale waaminifu waliomfuata Yeye waliuhisi pale Yerusalemu wakati jua lilipochwea na giza na uwoga vilipowazunguka.6

Kama wafuasi hawa wa kale takribani miaka 2000 iliyopita, wengi wenu yawezekana pia mnajisikia upweke mara kwa mara. Mimi nimepitia upweke huu tangu kifo cha mke wangu wa thamani, Barbara, zaidi ya miaka miwili iliyopita. Ninajua inakuwaje kuzungukwa na wanafamilia, marafiki na washirika lakini bado nahisi mpweke—kwa sababu pendo la maisha yangu halipo hapa tena pembeni yangu.

Janga la COVID-19 limedhihirisha hisia ya kutengwa na upweke kwa wengi. Hata hivyo licha ya matatizo tunayokumbana nayo maishani, tunaweza, kama asubuhi ile ya asubuhi ya Pasaka, kuamka katika maisha mapya katika Kristo tukiwa na matazamio bora na mapya na uhalisia mpya pale tunapomgeukia Bwana kwa ajili ya tumaini na kuwa sehemu ya.

Mimi binafsi ninahisi uchungu wa wale wanaohisi kutokuwa sehemu ya kitu fulani. Ninapotazama habari za ulimwenguni kote, ninaona wengi wanaoonekana kupitia upweke huu. Ninafikiri kwamba, kwa wengi, ni kwa sababu huenda hawajui kuwa wanapendwa na Baba wa Mbinguni na kwamba sote tu sehemu ya familia Yake ya milele Kuamini kwamba Mungu Anatupenda na kwamba sisi ni watoto Wake kunafariji na kutupatia hakikisho.

Kwa sababu sisi ni watoto wa kiroho wa Mungu, kila mmoja ana chimbuko la kiungu, asili na uwezekano wa kuwa. Kila mmoja wetu ni “mwana au binti mpendwa wa wazazi wa mbinguni.”7 Huu ndio utambulisho wetu! Hii ndivyo kweli tulivyo!

Utambulisho wetu wa kiroho unaimarishwa tunapoelewa utambulisho wetu mwingi wa hapa duniani ikiwa ni pamoja na kabila, utamaduni au urithi wa kitaifa.

Hisia hii ya utambulisho wa kiroho na kiutamaduni, upendo, na kustahili kuwa wa inaweza kuhamasisha matumaini na upendo kwa Yesu Kristo.

Sizungumzii juu ya matumaini katika Kristo kama mawazo ya kutamani. Badala yake, nazungumza juu ya tumaini kama tarajio ambalo litatimizwa. Tumaini kama hilo ni muhimu katika kushinda shida, kukuza uthabiti wa kiroho na nguvu, na kupata kujua kwamba tunapendwa na Baba yetu wa Milele na kwamba sisi ni watoto Wake ambao ni wa familia Yake.

Tunapokuwa na tumaini katika Kristo, tunapata kujua kwamba tunapohitaji kufanya na kuyashika maagano matakatifu, hamu zetu za kupendeza na ndoto zinaweza kutimizwa kupitia kwake Yeye.

Akidi ya Mitume Kumi na Wawili wameshauriana kwa pamoja katika roho ya maombi na kwa hamu ya kuelewa jinsi ya kuwasaidia wote ambao wanahisi upweke au wanaohisi kutokuwa sehemu ya. Tunatamani kuwasaidia wote wanaohisi hivyo. Naomba nitaje, hasa, kwa wale ambao kwa sasa hawajaoa wala kuolewa.

Akina Kaka na dada, zaidi ya nusu ya watu wazima katika Kanisa leo ni wajane, wametalikiwa, au hawajaoa wala kuolewa. Wengine wanajiuliza juu ya fursa zao na mahali pao kwenye mpango wa Mungu na katika Kanisa. Tunapaswa kuelewa kuwa uzima wa milele sio swali la hali ya ndoa ya sasa lakini ya ufuasi na kuwa “majasiri katika ushuhuda wa Yesu Kristo.”8 Matumaini ya wote ambao hawajaoa wala kuolewa ni sawa na ya waumini wote wa Kanisa la Bwana lililorejeshwa—kupokea neema ya Kristo kupitia “utii wa sheria na ibada za Injili.”9

Naomba nipendekeza kwamba kuna kanuni baadhi muhimu tunazohitaji kuzielewa.

Kwanza, maandiko na manabii wa siku za mwisho wanathibitisha kwamba kila mtu ambaye ni mwaminifu katika kuyashika maagano ya injili atakuwa na fursa ya kuinuliwa. Rais Russell M. Nelson alifundisha: “Katika njia na wakati wa Bwana mwenyewe, hakuna baraka watakayonyimwa Watakatifu Wake waaminifu. Bwana atahukumu na kumlipa kila mtu kulingana na hamu ya moyoni pamoja na matendo yake.”10

Pili, muda mzuri na njia nzuri ambapo baraka za kuinuliwa huwekwa havijafunuliwa vyote, lakini hata hivyo ni hakika.11 Rais Dallin H. Oaks alielezea kwamba baadhi ya hali “ya maisha ya duniani zitawekwa sawa katika Milenia, ambapo ni wakati wa kutimiza yote ambayo hayajakamilika katika mpango mkuu wa furaha kwa watoto wote wa Baba yetu wanaostahili.”12

Hiyo haimaanishi kwamba kila baraka imeahirishwa hadi Milenia; zingine tayari zimepokelewa na zingine zitaendelea kupokelewa hadi siku hiyo.13

Tatu, kumngojea Bwana kunamaanisha utii endelevu na maendeleo ya kiroho kuelekea Kwake. Kumngojea Bwana hakumaanishi kuungojea wakati wa mtu. Haupaswi kamwe kujisikia kama uko chumba cha kusubiria.

Kumngojea Bwana kuna maanisha hatua ya tendo. Nimejifunza kwa miaka kadhaa kwamba tumaini letu katika Kristo huongezeka tunapowatumikia wengine. Kutumikia kama Yesu Alivyotumikia, kwa asili tunakuza tumaini letu Kwake.

Ukuaji binafsi ambao mtu anaweza kuufikia sasa wakati anapomngojea Bwana na ahadi zake ni jambo la maana sana, takatifu, la mpango Wake kwa kila mmoja wetu. Michango ambayo mtu anaweza kufanya sasa ili kusaidia kujenga Kanisa duniani na kukusanya Israel inahitajika sana. Hali ya ndoa haina maana yoyote kwenye uwezo wa mtu wa kutumikia. Bwana huwaheshimu wale wanaomtumikia na kumngojea kwa uvumilivu na imani.14

Nne, Mungu hutoa uzima wa milele kwa watoto Wake wote. Wale wote wanaokubali zawadi ya Mwokozi ya toba na kushika amri Zake watapokea uzima wa milele, ingawa hawafikii sifa zake zote na ukamilifu katika maisha ya duniani. Wale wanaotubu watapata utayari wa Bwana wa kusamehe, kama alivyohakikisha, “Ndio, na mara nyingi watu wangu wanapotubu nitawasamehe makosa yao dhidi yangu.”15

Katika uchambuzi wa mwisho, uwezo wa mtu, matakwa yake na fursa zake katika haki ya kujiamulia na kuchagua, pamoja na vigezo vya baraka za milele, ni mambo ambayo Bwana peke yake ndiye anaweza kuhukumu.

Tano, kujiamini kwetu katika uhakikisho huu kumetokana na imani yetu katika Yesu Kristo ambaye kwa neema yake vitu vyote vinavyohusu maisha ya duniani vimewekwa sawa.16 Baraka zote zilizoahidiwa zitawezekana kupitia Yeye, ambaye, kwa Upatanisho Wake, “alishuka chini ya vitu vyote”17 na ameushinda ulimwengu.”18 “Ameketi mkono wa kuume wa Mungu, kudai kutoka kwa Baba haki zake za huruma ambazo anazo juu ya watoto wa watu … ; kwa hivyo huzungumza akipendelea watoto wa watu.”19 Mwishowe, “watakatifu watajawa na utukufu wake, na kupokea urithi wao”20 kama “warithi pamoja na Kristo.”21

Hamu yetu ni kwamba kanuni hizi zitawasaidia wote kuwa na tumaini lililoongezeka kwa Kristo na kuhisi hali ya kuwa sehemu ya Kristo.

Kamwe usisahau kwamba wewe ni mtoto wa Mungu, Baba yetu wa Milele, sasa na hata milele. Anakupenda, na Kanisa linakutaka na kukuhitaji. Ndiyo tunakuhitaji wewe. Tunahitaji sauti zako, talanta, ustadi, wema, na uadilifu wako.

Kwa miaka mingi, tumezungumza juu ya “vijana ambao ni waseja,” “watu wazima waseja,” na “watu wazima.” Vyeo hivyo vinaweza kusaidia kiutawala wakati mwingine lakini bila kuwa waangalifu vinaweza kubadilisha jinsi tunavyowaona wengine.

Je! Kuna njia ya kuepuka tabia hii ya kibinadamu ambayo inaweza kututenganisha sisi kwa sisi?

Rais Nelson aliomba kwamba tujiite sisi wenyewe kama waumini wa Kanisa la Yesu Kristo la Watakatifu wa Siku za Mwisho. Hiyo inaonekana kutugusa sisi sote, sivyo?

Injili ya Yesu Kristo ina uwezo wa kutuunganisha. Hatimaye sisi tunafanana zaidi kuliko tulivyo tofauti. Kama washiriki wa familia ya Mungu, sisi hakika ni kaka na dada. Paulo alieleza, “Naye [Mungu] alifanya kila taifa la wanadamu kutoka katika mmoja, wakae juu ya uso wa nchi yote.”22

Kwenu nyinyi marais wa vigingi, maaskofu, na viongozi wa akidi na akina dada viongozi, ninawaombeni mumfikirie kila mshiriki wenu wa kigingi, kata, akidi, au kikundi kama mshiriki ambaye anayeweza kuchangia na kuhudumu katika miito na kushiriki kwa njia nyingi.

Kila mshiriki katika akidi zetu, vikundi, kata, na vigingi, ana zawadi na talanta alizopewa na Mungu ambazo zinaweza kusaidia kujenga ufalme Wake sasa.

Na tuwaite washiriki wetu ambao hawajafunga ndoa kuhudumu, kuinua, na kufundisha. Puuza maoni na mawazo ya zamani ambayo wakati mwingine yamechangia bila kukusudia hisia zao za upweke na kwamba hawastahili au hawawezi kutumikia.

Ninatoa ushahidi wangu katika wikendi hii ya Pasaka ya Mwokozi wetu, Yesu Kristo, na matumaini ya milele ambayo Yeye hunipatia mimi na kwa wote wanaoamini jina lake. Na ninatoa ushuhuda huu katika jina Lake takatifu, hata Yesu Kristo, amina.