2017
Kiapo na Agano la Ukuhani
April 2017


Ujumbe wa Ualimu wa Kutembelea

Kiapo na Agano la Ukuhani

Kwa maombi jifunze maneno haya na utafute maongozi ili kujua kitu cha kufundisha. Ni kwa namna gani kuelewa lengo la Muungano wa Usaidizi wa Wakina Mama kutawatayarisha mabinti wa Mungu kwa ajili ya baraka za uzima wa milele?

Picha
Kansas City Missouri Temple

Jinsi sisi kama kina dada tunavyozidi kuelewa ya kwamba kiapo na agano la ukuhani inatuhusu sisi, ndivyo tutakavyozidi kupokea baraka na ahadi za ukuhani.

Mzee M. Russell Ballard wa Akidi ya Mitume Kumi na Wawili amesema, “Wote ambao wamefanya maagano matakatifu na Bwana na wanaheshimu maagano hayo wanastahili kupokea ufunuo binafsi, kubarikiwa kwa huduma ya malaika, na kuzungumza na Mungu, kupokea utimilifu wa injili, na, hatimaye, kuwa warithi ubavuni mwa Yesu Kristo kwa yote Baba aliyo nayo.”1

Baraka hizo na ahadi hizo za kiapo na agano la ukuhani ni kwa wote wanaume na wanawake Dada Sheri L. Dew, aliyekuwa mshauri katika Urais Mkuu wa Muungano wa Usaidizi wa Wakina Mama, alisema, “Utimilifu wa ukuhani uliomo katika ibada za nyumba ya Bwana unaweza kupokelewa tu na mwanaume na mwanamke kwa pamoja.”2

Dada Linda K. Burton, Rais Mkuu wa Muungano wa Usaidizi wa Wakina Mama, ametoa wito huu, “Ninawaalikeni mkariri kiapo na agano la ukuhani, ambalo linaweza kupatikana katika Mafundisho na Maagano 84:33–44. Kwa kufanya hivyo, ninawaahidi ya kwamba Roho Mtakatifu atapanua uelewa wenu juu ya ukuhani na kuwapa maongozi na kuwainua kwa njia za ajabu.”3

Mafundisho ya Joseph Smith kwa Muungano wa Usaidizi wa Wakina Mama yalikuwa na lengo la kuwatayarisha “kuja katika kumiliki, kupokea fadhila & baraka & vipawa vya ukuhani.” Haya yangeweza kutimizwa kwa njia ya ibada za hekaluni.

“ibada za hekaluni [ni] ibada za ukuhani, lakini [hazi] tunukii ofisi ya kichungaji juu ya wanaume au wanawake. [ibada hizi zinatimiza] ahadi ya Bwana kwamba watu wake—wanawake na wanaume—watajaliwa na uwezo kutoka juu. [M&M 38:32].4

Nyongeza ya Maandiko na Taarifa

Mafundisho na Maagano 84:19–40; 121:45–46; reliefsociety.lds.org

Picha
Relief Society seal

Imani Familia Usaidizi

Muhtasari

  1. M. Russell Ballard, “Men and Women and Priesthood Power,” Liahona, Sept. 2014, 36.

  2. Sheri L. Dew, katika Daughters in My Kingdom: The History and Work of Relief Society (2011), 128.

  3. Linda K. Burton, “Priesthood Power—Available to All,” Ensign, Juni 2014, 39–40.

  4. Mada za Injili, “Joseph Smith’s Teachings about Priesthood, Temple, and Women,” topics.lds.org.