2019
Azma Ambayo Itabadili Kuhudumia Kwetu
Januari 2019


Picha
ministering

Kanuni za Kuhudumu, Januari 2019

Azma Ambayo Itabadili Kuhudumia Kwetu

Wakati kuna azma nyingi za kuhudumia, juhudi zetu zinapaswa kuongozwa na nia ya kuwasaidia wengine wafikie uongofu binafsi wa kina na kuwa zaidi kama Mwokozi.

Tunapowapenda wengine kama Mwokozi anavyofanya, tunataka kuwasaidia kama Alivyofanya. Kama Mchungaji Mwema wa kondoo, Yeye ni mfano wa mwisho wa huduma yenye maana.

Katika kuiga mfano Wake wa kuhudumia, ni muhimu kukumbuka kwamba juhudi Zake za kupenda, kuinua, kutumikia, na kubariki zilikuwa na lengo la juu zaidi kuliko kutosheleza hitaji la mara moja. Kwa hakika alijua mahitaji yao ya kila siku na alikuwa na huruma juu ya mateso yao ya sasa. Kwa hivyo Aliponya, aliwalisha, alisamehe, na alifundisha. Bali alitaka kufanya zaidi kuliko kushughulikia kiu cha leo (ona Yohana 4:13-14). Alitaka wale waliomzunguka (ona Luka 18:22; Yohana 21:22), kumjua Yeye (ona Yohana 10:14; Mafundisho na Maagano 132:22–24), na kufikia uwezekano wao wa kuwa watakatifu (ona Mathayo 5:48). Hiyo bado ni kweli leo (ona Mafundisho na Maagano 67:13).

Kuna njia nyingi zisizohesabika tunazoweza kusaidia kuwabariki wengine, bali wakati mwisho wa lengo la kuhudumia kwetu ni kuwasaidia wengine kuja kumjua Mwokozi na kuwa zaidi kama Yeye, tutakuwa tunafanya kazi kuelekea siku ambapo hatutahitaji kumfundisha jirani yetu kumjua Bwana kwa sababu sisi wote tutamjua Yeye (ona Yeremia 31:34).

Lengo la Mwokozi Lilikwenda zaidi ya Mahitaji ya Sasa

  • Baadhi ya watu walikwenda mbali zaidi kuwaleta marafiki zao kwa Yesu kuponywa ugonjwa wa kupooza. Mwishowe Mwokozi alimponya mtu yule, bali alipenda zaidi kumsamehe dhambi zake (ona Luka 5:18–26).

  • Wakati watu walipomleta kwa Mwokozi mwanamke waliyemshika akizini, kujizuia kwake kumhukumu kuliokoa maisha yake kimwili. Bali alitaka kumwokoa kiroho pia, kumwambia “aende zake, na asifanye dhambi tena” (ona Yohana 8:2–11).

  • Mariamu na Martha walituma ujumbe kwa Yesu wakimwomba aje kumponya rafiki Yake, Lazaro. Yesu, ambaye alikuwa amewaponya wengine kwenye nyakati zisizohesabika, alichelewesha kuwasili Kwake mpaka baada ya Lazaro kuwa amekufa. Yesu alijua kile familia walichotaka, bali katika kumfufua Lazaro kutoka wafu, Aliimarisha shuhuda zao za utukufu Wake (ona Yohana 11:21–27).

Ni mifano gani mingine unayoweza kuongeza kwenye orodha hii?

Tunaweza Kufanya Nini?

Kama azma yetu ni kuwasaidia wengine kuwa zaidi kama Mwokozi, itabadilisha jinsi tunavyohudumia. Hapa kuna baadhi ya njia uelewa huu unavyoweza kuongoza juhudi zetu za kuhudumia.

Wazo la 1: Unganisha huduma na Mwokozi

Juhudi zetu zote za kufanya mema ni za kufaa, lakini tunaweza kutafuta fursa nyingi kuongeza huduma zetu kwa kuziunganisha na Mwokozi. Kwa mfano, kama familia unayoihudumia inaumwa, chakula kinaweza kusaidia, bali mwonekano wako wa kawaida wa upendo ungeweza kuongezwa na ushuhuda wako wa upendo wa Mwokozi kwa ajili yao. Msaada wako na kazi kwenye ua itashukuriwa, bali labda ingefanywa kuwa ya maana zaidi na toleo la baraka za ukuhani.

Mzee Neil L. Andersen wa Akidi ya Mitume Kumi na Wawili alifundisha: “Mtu mwenye moyo mwema anaweza kumsaidia mtu fulani kufunga tairi, kumpeleka mkaazi mwenza kwa daktari, kula chakula na mtu fulani mwenye huzuni, au kutabasamu na kusema halo kuifanya siku iwe njema.

“Bali mfuasi wa amri ya kwanza kwa kawaida ataongeza kwenye matendo haya muhimu ya huduma.”1

Wazo la 2: Lenga kwenye Njia ya Agano

Akizungumza kwa waumini kwa mara ya kwanza kama Rais wa Kanisa, Rais Russell M. Nelson alisema, “Baki katika njia ya agano.” Kufanya na kuweka maagano “kutafungua mlango kwa kila baraka ya kiroho na fursa iliyopo.”2

Kama Watakatifu wa Siku za Mwisho, tumebatizwa, kuthibitishwa, na kupokea kipawa cha Roho Mtakatifu. Waumini wa kiume wanaostahili hupokea ukuhani. Tunakwenda hekaluni kwa ajili ya endaumenti zetu na kuunganishwa pamoja kama familia milele. Ibada hizi za wokovu na maagano yake yanayohusika ni muhimu kwa ajili yetu kuwa kama Yeye ili kwamba tuweze kuwa na Yeye.

Tunaweza kuwa na jukumu muhimu la kufanya katika kuwasaidia wengine kwenye njia ile tunapowasaidia kuweka maagano yao na kujitayarisha kufanya maagano ya baadae.3 Ni kwa jinsi gani unaweza kuwasaidia watu binafsi au familia unazozihudumia kupokea ibada inayofuata wanayohitaji? Hii ingeweza kumaanisha kusaidia kumtayarisha baba kumbatiza binti yake, kuelezea baraka za ibada inayofuata itakayofanywa, au kushiriki njia za kuwa na uzoefu wa maana zaidi kufanya upya maagano yetu wakati wa kupokea sakramenti.

Wazo la 3: Alika na Tia Moyo

Wakati unaofaa, shauriana na wale unaowatunza kuhusu uongofu wao na juhudi za kuwa zaidi kama Kristo. Waache wajue uwezo unaouona kwao na wasifie. Tafuta wapi wanahisi wangeweza kujirekebisha na zungumza kuhusu jinsi ambavyo ungeweza kusaidia. (Kwa kushauriana pamoja zaidi na wale ambao unawahudumia, ona “Shauri kuhusu Mahitaji Yao,” Liahona, Sept. 2018, 6–9.)

Usiogope kuwaalika kumfuata Mwokozi na Mruhusu kuwasaidia kufikia uwezekano wao mtakatifu. Mwaliko huu unaweza kuwa wa kubadilisha maisha, unapounganishwa na onyesho la imani yako kwao na imani yako katika Yeye.

Njia Sita Tunazoweza Kuwasaidia Wengine Kuendelea kuelekea kwa Kristo

Yafuatayo ni mapendekezo kwa ajili ya kuwasaidia wengine katika kufanya maboresho ya maisha na kuendelea katika njia ya agano. (Ona Hubiri Injili Yangu, Sura ya 11, kwa mawazo zaidi.)

  1. Shiriki. Kuwa mkweli na jasiri unaposhiriki jinsi Mwokozi alivyokusaidia ulipojaribu kumkaribia zaidi kwa kuishi kanuni za injili licha ya vikwazo vingi.

  2. Baraka zilizoahidiwa. Watu wanahitaji sababu ya kubadilika ambayo ni ya kuvutia sana kuliko sababu za kutobadilika. Kuelezea baraka zinazohusiana na tendo zinaweza kutoa motisha yenye nguvu mno (ona Mafundisho na Maagano 130:20–21).

  3. Alika. Kuishi kanuni ya injili huleta ushuhuda ambao ni wa kweli (ona Yohana 7:17) na kunaongoza kwenye uongofu wa kina.4 Karibia kila maongezi ungejumuisha na mwaliko wa kawaida kufanya kitu fulani ambacho kingewasaidia kuendelea.

  4. Pangeni Pamoja. Nini kinahitajika kutokea ili wafanikiwe kutunza msimamo wao wa kubadilika? Unawezaje kuwasaidia? Je, kuna mpangilio wa muda unaohusika?

  5. Usaidizi. Wakati una msaada, jenga mtandao wa usaidizi wa watu wanaoweza kusaidia mtu binafsi kubaki mwenye motisha na kufanikiwa. Sote tunahitaji kiongozi wa mashabiki.

  6. Fuatilia. Shiriki maendeleo kila mara Baki ukizingatia kwenye mpango bali rekebisha kama ni muhimu. Kuwa mwenye subira, mwenye msimamo, na mwenye kutia moyo. Mabadiliko yanaweza kuchukuwa muda.

Mwaliko wa Kutenda

Fikiria jinsi juhudi zako za kuhudumia—zote kubwa na ndogo—zinavyoweza kuwasaidia wengine kuzidisha kina cha uongofu wao na kuwa zaidi kama Mwokozi.

Muhtasari

  1. Neal L. Andersen, “A Holier Approach to Ministering” (Brigham Young University devotional, Apr,10, 2018), 3 speeches.byu.edu.

  2. Russell M. Nelson, “As We Go Forward Together,” Liahona, Apr. 2018, 7.

  3. Ona Henry B. Eyring,”Daughters in the Convenant,” Liahona May 2014, 125–28.

  4. Ona David A. Bednar, “Converted unto the Lord,” Liahona, Nov. 2012, 106–109).