2019
Kuhudumia Ni Kuwaona Wengine kama Mwokozi Anavyofanya
Juni 2019


Picha
ministering

Kanuni za Kuhudumia, Juni 2019

Kuhudumia ni Kuwaona Wengine kama Mwokozi Anavyofanya

Yesu alitumia muda Wake mwingi pamoja na wale walioonekana kama walio tofauti; Aliona uwezo wao wa kiungu.

Katika juhudi zetu za kuhudumu kama Mwokozi, tunaweza kuombwa kumhudumia mtu fulani ambaye ni tofauti na sisi. Hii inatoa nafasi kwetu kujifunza na kukua.

Tofauti za kitamaduni, kielimu, kijamii, kiuchumi, kiumri, tabia za awali au za sasa au tofauti zingine zinaweza kufanya kuwa rahisi kumhukumu mtu fulani kabla hata kumjua. Kuhukumu huku kusiko kwa haki kuko ndani ya tabia ya mtu, na Mwokozi alionya dhidi yake. (ona 1 Samweli 16:7; Yohana 7:24).

Je, tunaweza kutazama zaidi ya tofauti na kuona wengine kama Mwokozi anavyofanya? Tunawezaje kujifunza kuwapenda wengine vile walivyo na kile wanachoweza kuwa?

Kutazama na kupenda

Biblia inaelezea hadithi inayojulikana ya kijana tajiri ambaye aliuliza jinsi ya kupata maisha ya milele: “Yesu akamkazia macho, akampenda, akamwambia, Umepungukiwa na neno moja. Enenda ukauze ulivyo navyo vyote, uwape maskini, nawe utakuwa na hazina mbinguni; kisha njoo unifuate” (Marko 10:21).

Wakati Mzee S. Mark Palmer wa wale Sabini alipojifunza maandiko haya miaka michache iliyopita, sehemu mpya ya hadithi ilijitokeza kwake.

‘Kisha Yesu akimtazama na kumpenda.’

“Niliposikia maneno haya, taswira dhahiri ilijaa akilini mwangu ya Bwana wetu akitua na kumtazama kijana huyu. Kumtazama—kama katika kutazama kwa undani na kwa kupenya kwenye nafsi yake, kutambua uzuri wake na pia kuweza kwake kuwa, vilevile kutambua hitaji lake kubwa.

“Kisha maneno rahisi—Yesu akampenda. Alihisi upendo mkubwa na huruma kwa kijana huyu mwema, na kwa sababu ya upendo huu na pamoja upendo huu, Yesu aliuliza zaidi kumhusu. Nilifikiria jinsi ilivyokuwa kwa huyu kijana kuzungukwa na upendo kama huu hata wakati akiwa anatakiwa kufanya kitu fulani kilicho kikubwa kabisa na kigumu kama kuuza vyote alivyo navyo na kuwapa maskini. …

“[Nilijiuliza] ‘Ninawezaje kujazwa na upendo kama wa Kristo ili [wengine] waweze kuhisi upendo wa Mungu kupitia kwangu na kutamani kubadilika?’ Ninawezaje kuwatazama [watu binafsi wanaonizunguka] kwa njia sawa Bwana alivyomtazama kijana tajiri, kuwaona jinsi walivyo kikweli na kile wanachoweza kuwa, kuliko tu kile wanachofanya au wasichofanya? Ninawezaje kuwa zaidi kama Mwokozi?”1

Kujifunza Kuwaona Wengine

Kujifunza Kuwaona Wengine kama Mwokozi anavyofanya kunaleta thawabu nyingi. Haya ni baadhi ya mapendekezo ambayo yanaweza kusaidia tunapofanya kazi kuelekea lengo hili.

  • Pata Kuwafahamu
    Fanya juhudi za kuwafahamu watu zaidi ya utondoti wa juujuu. Tambua kwamba kujenga mahusiano kunachukua muda na juhudi za kikweli. (Ona Kanuni za Kuhudumia za Agosti 2018 mada “Kujenga Mahusiano ya Maana” kwa msaada.)

  • Jichunguze Mwenyewe
    Tilia maanani kwa hukumu unazoweza kufanya kwa kufahamu au kutokufahamu. Chukua tahadhari ya wazo lisilohakikishwa unalofanya kuhusu wengine na jaribu kuelewa kwa nini unahisi kuhusu wao kwa njia unayofanya.

  • Usihukumu
    Tambua kwamba hali hazifafanui thamani ya mtu binafsi. Jiweke mwenyewe katika hali zao na fikiria jinsi ungetaka mtu fulani akuone kama ulikuwa katika hali inayofanana nao. Kutenganisha chaguzi za mtu fulani na tabia kutoka thamani yao halisi na uwezekano mtakatifu unaweza kutusaidia kuwaona kama mwokozi angewaona.

  • Omba Kuwapenda
    Omba kwa ajili yao mara kwa mara kwa jina na kwa ajili ya utulivu kujenga urafiki wa kweli. Kuwa na mtazamo wa kimaombi kwenye huduma yako. Kuna nafasi kati ya kile unachokifanya na kile kwa kweli wanachokihitaji?

Yesu alitumia muda Wake pamoja na watu kutoka hali nyingi tofauti za maisha: matajiri, masikini, watawala, na watu wa kawaida. Mara nyingi alikuwa mhanga wa hukumu isiyo sahihi na wengine walipomtazama na umaskini wake dhahiri au hali zisizo na umuhimu. “Na tumwonapo hana uzuri hata tumtamani. … Alidharauliwa wala hatukumhesabu kuwa kitu” (Isaya 53:2–3).

Mtazamo Kama wa Kristo

Dada anashiriki hadithi hii ya kujifunza kumtazama jirani na macho kama ya Kristo:

“Julia (jina limebadilishwa) aliishi karibu nami na alionekana kutokuwa na marafiki wowote. Alionekana siku zote amefadhaika na mwenye hasira. Licha ya hayo, niliamua kuwa rafiki yake. Si tu rafiki wa kawaida wa kupita, bali rafiki wa kweli. Nilimsemesha popote nilipomwona na nilionyesha kupendezwa na chochote alichokuwa anafanya Polepole nilitengeneza urafiki wa karibu pamoja naye, kuleta furaha moyoni mwangu.

“Siku moja, niliamua kumtembelea Julia na kumwuliza kuhusu uamuzi wake kutoshiriki Kanisani.

“Nilipata kuelewa kwamba hana familia au jamaa jirani karibu. Ndugu yake pekee ni kaka ambaye anaishi mbali sana, anawasiliana naye mara moja tu kwa mwaka kwa simu. Nilipokuwa namsikiza akimwaga machungu yake, hasira, na kuvunjika moyo kuhusu familia yake na Kanisa, hisia zisizokatalika za huruma na upendo kwa dada huyu zilikuja juu yangu kwa nguvu kubwa. Nilihisi uchungu wake na kuvunjika moyo kwake. Nilitambua jinsi maisha yake yalikuwa ya kipweke. Ilikuwa kama vile nilisikia kirai cha kimya nyuma yangu: ‘Ninampenda pia. Mpende na mheshimu.’

“Nilikaa na kusikiliza mpaka alikuwa hana zaidi ya kusema. Nilihisi upendo na huruma kwa ajili yake. Huyu ni dada ambaye kamwe hajajua jinsi ilivyo kupendwa. Mara moja nilimwelewa kwa undani zaidi. Nilimshukuru kwa kuniruhusu kumtembelea, na nilimwacha kwa kumkumbatia na pamoja na upendo wangu na heshima kwa ajili yake, Kamwe hataweza kujua jinsi gani alinigusa na ziara ile. Baba wa Mbinguni amefungua macho yangu na kunifundisha kwamba nilikuwa na uwezo wa kupenda pamoja na huruma iliyoongezwa. Nimeamua katika azimio langu si tu kuwa rafiki yake bali pia kuwa familia kwake.”

Ni kitu kitakatifu kualikwa kwenye maisha ya mtu fulani. Pamoja na maombi, uvumilivu, na msaada kutoka kwa Roho, tunaweza kujifunza kufanya hivyo pamoja na ono zaidi kama la Kristo.

Muhtasari

  1. S. Mark Palmer, “Yesu Akamkazia Macho Akampenda,” Liahona, Mei 2017, 115.