2019
Jinsi ambavyo Roho Anaweza (na Atakusaidia) Kuhudumu
Septemba 2019


Kanuni za Kuhudumu, Septemba 2019

Jinsi ambavyo Roho Anaweza (na Atakusaidia) Kuhudumu

Jukumu la kikuhani la kuhudumu, lililotolewa kwa wanaume na wanawake, linajumuisha haki ya kupokea ufunuo.

Picha
ministering

Picha kutoka Getty Images

Wito wa kuhudumu na kutumikia na hata kupenda kama vile Mwokozi Alivyopenda wakati mwingine huonekana kuwa na changamoto—hasa unapojumuisha kuwafikia wengine ambao hatuwafahamu vyema. Tukiwa na njia milioni za kuhudumu tunajiuliza jinsi tunavyoweza kujua njia bora zaidi kuwafikia wale ambao tumepewa.

Hatupaswi kujiuliza kwa muda mrefu kwa sababu juhudi zetu za dhati zinaweza kuongozwa na Roho Mtakatifu.

“Jukumu lako takatifu la kuhudumu linakupa haki ya kiungu ya mwongozo,” Alisema Dada Bonnie H. Cordon, Rais Mkuu wa Wasichana. “Unaweza kutafuta mwongozo huo kwa kujiamini.”1

Tunapotafuta kuhudumu kama vile Mwokozi alivyohudumu, tunaweza kuongozwa na Roho yule yule Aliyemwongoza Yeye. Hi ni kweli hasa tunapotumikia katika majukumu kama vile kuhudumia, yaliyofanywa chini ya mamlaka ya funguo za kikuhani za askofu. Hapa kuna mapendekezo sita ya kuhudumu kwa Roho.

Ni kwa Jinsi Gani Ninaweza Kuwa na Roho Wakati Ninapohudumu?

  • Sali kwa ajili ya Mwongozo. Baba wa Mbinguni anataka tuwasiliane Naye kupitia sala. Sala haituwezeshi tu kusogea karibu naye, bali pia inahifadhi “baraka ambazo Mungu yuko tayari kutupatia lakini hilo hutendeka chini ya masharti ya kuziomba.”2 “Tunaposali na kutafuta kujua mioyo yao,” alisema dada Cordon, “ninashuhudia kwamba Baba wa Mbinguni atatuongoza na Roho Wake atakwenda pamoja nasi.”3

  • Usingoje Ushawishi. Kuwa mwenye kutenda. Iweni wenye “kujishughulisha kwa shauku” (Mafundisho na Maagano 58:27), na mtaona kwamba juhudi zenu zitaongozwa na kutukuzwa. “Kwenda mbele katika huduma na kazi yetu ni njia muhimu ya kustahili kupata ufunuo,” alisema Rais Dallin H. Oaks, Mshauri wa Kwanza katika Urais wa Kwanza. “Katika kujifunza kwangu maandiko nimepata kuona kuwa ufunuo zaidi kwa watoto wa Mungu huja wakati wakiwa katika kutenda, sio wakiwa wamekaa manyumbani mwao wakingoja Bwana kuwaambia hatua ya kwanza ya kuchukua.”4

Ni kwa namna gani ninaweza kutambua Ushawishi wa Kuhudumu?

  • Chukua ushauri wa Mormoni. Hatupaswi kukaa tu na kuhofia ikiwa wazo lilikuwa ushawishi au siyo. Si kama tuna ufunguo rahisi wa Mormoni wa kufahamu: Ukiwa na wazo ambalo linakushawishi kufanya mema na kuamini na kuwasaidia wengine kuamini katika Kristo, unaweza kujua kuwa ni la Mungu (Ona Moroni 7:16).

  • Usiwe na wasiwasi kuhusu hilo! “Ruka tu ndani ya bwawa la kuogelea na uogelee,” alisema Mzee Jeffrey R. Holland wa Jamii ya Mitume Kumi na Wawili. “Waelekee wale wenye uhitaji. Usisimame ukishangaa ikiwa unapaswa kuogelea kichali au kupiga kasia mbele. Kama tutafuata kanuni muhimu ambazo zimefundishwa, tukifungamana na funguo za ukuhani, na kumtafuta Roho Mtakatifu kutuongoza, hatuwezi kushindwa.”5

Ni ipi njia bora ya kufuata ushawishi?

  • Mara moja. Dada Susan Bednar (Mke wa Mzee David A. Bednar wa Akidi ya Mitume Kumi na Wawili) ni mfano mkuu wa kufuata ushawishi. Baada ya kusali kwa ajili ya “macho ya kiroho kuwaona wale walio na hitaji,” anaangalia kuzunguka umati na mara kwa mara “huhisi msukumo wa kiroho kumtembelea au kupiga simu kwa mtu fulani,” Alishiriki Mzee Bednar. “Na Dada Bedna anapopokea msukumo kama huo, mara moja anajibu na kutii. Ni hali ya kila mara kwamba mara ‘amina’ inaposemwa kwenye sala ya kufunga, atazungumza na kijana mbalehe au kumkumbatia dada, au anaporejea nyumbani mara moja anachukua simu na kupiga.”6

  • Kwa Ujasiri. Hofu ya kukataliwa na hisia za aibu, kutostahili, au kutofaa inaweza kutuzuia kufuata ushawishi wa kuhudumu. “Katika njia na nyakati tofauti, sote tunahisi kupungukiwa, pengine kutostahili,” alisema Mzee Gerrit W. Gong wa Akidi ya Mitume Kumi na Wawili. Hata hivyo katika juhudi zetu za dhati za kumpenda Mungu na kumhudumia jirani yetu, tunaweza kuhisi Upendo wa Mungu na mwongozo wa kiungu unaohitajika kwa ajili ya maisha yetu na yao kwa njia mpya na takatifu zaidi.”7

    Kaka mmoja alishiriki jinsi alivyokuwa akisita kumfikia mume wa mwanamke mmoja aliyekuwa amejaribu kujiua. Mwishowe, nilimwomba mume huyu kwenda kupata chakula cha mchana. “Na mara niliposema, ‘Mke wako alijaribu kujiua. Hilo laweza kuwa jambo zito kwako. Je, unataka kuliongelea jambo hili?’ alilia wazi wazi,” alishiriki. “Tulikuwa na mazungumzo ya upole na ya karibu sana na tulianzisha urafiki wa karibu na uaminifu ndani ya dakika chache.”8

Muhtasari

  1. Bonnie H. Cordon, “Kuwa Mchungaji,” Liahona, Nov. 2018, 76.

  2. Kamusi ya Biblia, “Sherehe.”

  3. Bonnie H. Cordon, “Kuwa Mchungaji,” 76.

  4. Dallin H. Oaks, “Katika Wakati Wake Mwenyewe, katika Njia Zake Mwenyewe,” Liahona, Aug. 2013, 24.

  5. Jeffrey R. Holland, “Huduma ya Upatanisho,” Liahona, Nov. 2018, 77.

  6. David A. Bednar, “Wepesi wa Kutazama,” Liahona, Des. 2006, 17.

  7. Gerrit W. Gong, “Mwako Wetu wa Imani,” Liahona, Nov. 2018, 42.

  8. Ona Bonnie H. Cordon, “Kuwa Mchungaji,” 76.