2019
Nini Hadithi ya Krismasi Inatufundisha kuhusu Kuhudumu
Desemba 2019


Kanuni za Kuhudumu, Desemba 2019

Nini Hadithi ya Krismasi Inatufundisha kuhusu Kuhudumu

“Haya ni majira yanayopendwa ya mwaka. Imba wimbo; Wakati wa Krismasi unakaribia Elezea hadithi ya kweli ya kuzaliwa kwa Yesu, wakati kama mtoto, alikuja duniani” (Wimbo wa kuzaliwa kwa Yesu,” Kitabu cha Nyimbo za Watoto, 52).

Picha
ministering

Kila kitu kutoka Tazama Mwanakondoo wa Mungu, na Walter Rane

Wakati wa Krismasi ni wakati wa ajabu wakati kondoo, wachunga kondoo, hori, na nyota ghafla vinachukuwa maana mapya. Vinakuwa wachezaji muhimu katika kueleza tena mojawapo ya matokeo muhimu mno katika historia ya binadamu: kuzaliwa kwa Yesu Kristo. Familia nyingi zinaonesha tukio la kuzaliwa kwa Yesu Kristo katika nyumba zao. Wengine hulazimika kusoma hadithi ya kuzaliwa kwake au kushiriki katika tamasha. Kama ilivyo katika hadithi za Kristo, hadithi ya kuzaliwa Kwake imejaa masomo tunayoweza kujifunza kuhusu kuhudumu, kuhusu kushiriki nuru Yake kuangaza ulimwengu. “Hadithi ya Krismasi ni hadithi ya upendo,” alisema Rais Henry B. Eyring, Mshauri wa Pili katika Urais wa Kwanza.

“… Katika hadithi za kuzaliwa kwa Kristo, tunaweza kuona na kuhisi Yeye alikuwa nani na Yeye ni nani. Ambaye anaufanya mzigo wetu mwepesi njiani. Na itatuelekeza kujisahau wenyewe na kuufanya mwepesi mzigo kwa ajili ya wengine.”1

“Hapakuwa na nafasi ya chumba kwa ajili yao katika nyumba ya wageni” (Luka 2:7)

Mwangalizi wa nyumba ya wageni alishindwa kuweke chumba kwa ajili ya Mwokozi, bali hatupaswi kufanya kosa lile! Tunaweza kuweka chumba kwa ajili ya Mwokozi katika mioyo yetu kwa kuweka nafasi kwa ajili ya kaka na dada zetu kwenye meza zetu, nyumba zetu, na katika desturi zetu. Desturi nyingi za familia zinaweza kufanywa za kupendeza zaidi na hata za kukumbukwa zaidi kwa kuwajumuisha watu wengine. Daiana na familia yake wana desturi ya kualika mtu fulani kula Krismasi pamoja nao. Kila Desemba, wanajadili na kuamua nani wangependa kumwalika.2 Pengine familia yako ingeweza kuanza desturi kama hiyo. Labda mtu fulani unayemhudumia angependa kujiunga na familia yako katika kuimba nyimbo za Krismasi mnazozipenda pamoja. Mnaweza pia kuweka nafasi kwenye chakula chenu cha jioni cha Krismasi kwa ajili ya mtu fulani ambaye hataweza kuwa na familia katika eneo lako.

Njia gani mzuri zaidi ya kumsherehekea Mwokozi kuliko kufuata mfano wake wa kujumuisha. Kumbuka kwamba anawaalika “wote kwenda Kwake na kupokea wema wake; na hamkatazi yeyote ambaye anayemjia, mweusi kwa mweupe, wafungwa na walio huru, wake kwa waume; na anawakumbuka kafiri; na wote ni sawa kwa Mungu, wote wawili, Myahudi na Myunani” (2 Nefi 26:33). Weka nafasi na jumuisha.

“Na katika nchi ile ile walikuwako wachungaji wakikaa makonde, na kulinda kundi lao kwa zamu usiku” (Luka 2:8)

Inaonekana sawa kwamba wachungaji wangekuwa miongoni mwa wa kwanza kumwamkia mtoto mchanga Mwokozi. Manabii wa kale walimtaja Yesu Kristo kama “Mchunga kondoo wa Israeli” (Zaburi 80:1) na “Mchungaji wa kondoo dunia kote (1 Nefi 13:41). Na Yesu Mwenyewe alisema, “Mimi ndimi mchungaji mwema, na nawajua kondoo wangu” (Yohana 10:14). Kuwajua kondoo wetu na kuwalinda ni sehemu muhimu ya uchungaji na kuhudumia kama Mwokozi anavyofanya.

Pamoja na mianga hafifu inayoangaza na mapambo yenye madoido, kuna mengi ya kuangalia wakati wa Krismasi. Lakini labda uzuri mkubwa mno wa majira unaweza kupatikana wakati tunapokumbuka kugeuza lengo letu kwa wale tunaowahudumia na kulinda makundi yetu wenyewe. Kulinda kunaweza kuwa kutambua kitu mtu fulani anachokipenda au kuuliza kuhusu mipango ya likizo ya mtu fulani. Tunalinda wakati tunapoona na kufahamu mahitaji ya wengine—yote yaliyo dhahiri na yasiyo dhahiri sana.

Wakati Cheryl ghafla alipompoteza mume wake, Mick, alichanganyikiwa. Kama Krismasi yake ya kwanza bila yeye alivyozidi kukaribia, upweke ulizidi. Kwa shukrani, dada anayemhudhumis Shauna alikuwa pale. Shauna na mumewe, Jim, walimwalika Cheryl kwenye matembezi mengi ya likizo. Waliona koti la Cheryl lililochakaa na waliamua kushughulikia hilo. Siku chache kabla ya Krismasi, Shauna na Jim walimletea Cheryl zawadi ya Krismasi: koti jipya zuri sana. Walifahamu juu ya mahitaji ya kimwili ya Cheryl ya koti la joto lakini pia juu ya mahitaji ya mhemuko kwa ajili ya faraja na wenza. Walijitokeza kukamilisha mahitaji hayo kwa kadri ambavyo wangeweza na kuweka mfano mzuri wa jinsi sisi pia tunavyoweza kulinda makundi yetu.3

“Wachungaji waliambiana, haya na twendeni mpaka Bethlehemu” (Luka 2:15)

“Na sasa twendeni” ni mwaliko mkunjufu sana! Wachungaji wa kondoo hawakusadiki kwamba marafiki zao wangekuwa wamechoka sana kwenda safari ndefu. Hawakwenda kimya kimya Bethlehemu wao peke yao. Kwa furaha waligeukiana na kusema, “Sasa twendeni!”

Wakati tunakuwa hatuwezi kuwaalika marafiki zetu kuja na kumwona mtoto mchanga Mwokozi, tunaweza kuwaalika kuhisi roho ya Krismasi (au roho ya Kristo) kwa kuhudumia pamoja nasi. “Njia ya kuongeza roho ya Krismasi ni kuwafikia kwa ukarimu wale wanaotuzunguka na kujitolea,” alisema Bonnie L. Oscarson, Rais Mkuu wa awali wa Wasichana.4 Fikiria unashikilia mshumaa. Wengine kwa hakika wanaweza kuona na kunufaika kutoka mwanga unaotoka kutoka kwenye mshumaa wako, bali fikiria joto wanalohisi kama utatumia mshumaa wako kuuwasha mshumaa wao na kuwaruhusu kushikilia mwanga kwa ajili yao wenyewe.

Kristo mwenyewe alifundisha kwamba wale wanaomfuata watakuwa na nuru ya uzima (ona Yohana 8:12). Kuhudumia kama alivyofanya ni njia moja tunayoweza kumfuata na kufurahia nuru ile iliyoahidiwa. Kwa hiyo shiriki nuru kwa kuwaalika wengine kuhudumia pamoja nawe! Je, wewe na wale unaowahudumia mnawejazje kutumikia pamoja? Pamoja mnaweza kuandaa chakula chenu mnachokipenda au kumshangaza mtu fulani na zawadi ndogo au barua. Pamoja mnaweza wote kuhisi nuru ambayo inakuja kutokana na kufuata mfano wa Kristo wa huduma.

“Walipomwona wakatoa habari waliyoambiwa juu ya mtoto huyu” (Luka 2:17)

Ni rahisi kufikiria msisimko wa furaha wa wachunga kondoo waliposhiriki habari za kustaajabisha za kuzaliwa kwa Kristo na watu wengi jinsi walivyoweza. Wakiwa wametabiriwa na malaika, Masiya aliyetabiriwa amekuja! Alikuwa hapa! Kwa kweli, kushiriki habari njema za Mwokozi ni wazo kubwa la hadithi ya Kuzaliwa Kristo. Malaika waliimba. Nyota ilionyesha njia. Na wachunga kondoo walifanya ijulikane kila mahali.

Tunaweza kuongeza sauti zetu kwenye hadithi ya Krismasi kwa kushiriki habari njema na kumshuhudia Mwokozi. “Unapopata fursa ya kumwakilisha Mwokozi katika juhudi zako za kuhudumia, jiulize, ‘jinsi gani ninaweza kushiriki nuru ya injili na mtu binafsi au familia?” alifundisha Dada Jean B. Bigham, Rais Mkuu wa Muungano wa Usaidizi wa Akina Mama. Roho ananishawishi kufanya nini?”5

Haya ni mapendekezo machache kwa ajili yako kufikiria unapotafuta kujua jinsi unavyoweza kushiriki ushuhuda wako wa Mwokozi na injili Yake:

  • Tafuta maandiko ambayo yanateka hisia zako kumhusu Mwokozi au elezea kwa nini una shukrani Kwake. Yashiriki pamoja na wale unaohudumia.

  • Tuma maandiko au ujumbe wa vyombo vya habari pamoja na video ya Krismasi. Kuna baadhi zinazoshangaza kwenye ChurchofJesusChrist.org!

  • Mwambie rafiki kuhusu kumbukumbu maalumu au desturi ambayo inakukumbusha wewe juu ya Kristo.

Kuwa na imani kwamba Roho Mtakatifu atashuhudia juu ya ukweli wa ushuhuda wako, kama Yeye alivyoshuhudia kwa Simeoni na Anna kwamba mtoto Yesu alikuwa Mwokozi (ona Luka 2:26, 38).

“Kwa kweli kumheshimu kuja kwa [Yesu Kristo] katika ulimwengu, lazima tufanye kama alivyofanya na kuwafikia kwa huruma na upole binadamu wenzetu,” alisema Mzee Dieter F. Uchtdorf wa Akidi ya Mitume Kumi na wawili. “Hii tunaweza kufanya kila siku, kwa neno na tendo Wacha hii iwe desturi yetu ya Krismasi, bila kujali wapi tulipo—kuwa wapole kidogo, wenye kusamehe zaidi, wenye kuhukumu kidogo, wenye shukrani zaidi, na wakarimu zaidi katika kushiriki wingi wetu na wale wenye mahitaji.”6

Muhtasari

  1. Henry B. Eyring, “Hadithi za Krismasi” (Ibada ya Krismasi ya Urais wa Kwanza, Dec.6, 2009), broadcasts.ChurchofJesusChrist.org

  2. Ona Daiana Melina Albornoz Diaz, “Kushiriki Krismasi,” Liahona, Dec. 2007,17.

  3. Ona Cheryl Boyle, “Angeweza kuinunua kwa ajili Yako,” Ensign, Dec. 2001, 57

  4. Bonnie L. Oscarson, “Krismasi Ni Upendo kama wa Kristo” (Ibada ya Krismasi ya Urais wa Kwanza, Dec.7, 2014), broadcasts.ChurchofJesusChrist.org

  5. Jean B. Bingham, “Kutumikia kama Mwokozi Anavyofanya,” Liahona, Mei 2018,106.

  6. Dieter F. Uchtdorf, “Sambaza vipande vyaako vya mkate” (Ibada ya Krismasi ya Urais wa Kwanza, Dec.3, 2017), broadcasts.ChurchofJesusChrist.org