2020
Kuhudumia kupitia Mkutano wa Sakramenti
Juni 2020


“Kuhudumu kupitia Mkutano wa Sakramenti,” Liahona, Juni 2020

Picha
kuhudumu

Vielelezo na Edward McGowan

Kanuni za Uhudumu, Juni 2020

Kuhudumu kupitia Mkutano wa Sakramenti

Mkutano wa sakramenti hutoa fursa za kuungana na kuwahudumia wengine.

Mkutano wa sakramenti ni muda kwa ajili ya lishe ya kiroho na tafakari binafsi juu ya Mwokozi na Upatanisho Wake. Tunashiriki sakramenti kila wiki, tunajengwa pamoja (ona Mafundisho na Maagano 84:110). Lakini wengine katika kata zetu na matawi huja na mizigo mizito au hawaji kabisa.

Hizi ni fursa chache za jinsi tunavyoweza kutumia saa hiyo takatifu kuwahudumia wengine na kufanya mabadiliko katika maisha yao.

Saidia Kufanya Mkutano wa Sakramenti kuwa Mzuri kwa Wale Unaowahudumia

Sehemu ya kwanza katika kujifunza jinsi ya kuhudumia ni kuwajua watu binafsi au familia na mahitaji yao. Kunaweza kuwa na njia ambazo unaweza kuwasaidia kufanya uzoefu wao wa ibada ya sakramenti kuwa mzuri zaidi kwa kujifunza zaidi kuhusu wao.

Kwa Mindy, mama mdogo wa watoto mapacha, juhudi rahisi za dada yake anayehudumia zilileta mabadiliko makubwa katika uzoefu wake wa mkutano wa sakramenti kila wiki.

“Kwa sababu ya ratiba ya kazi ya mume wangu, ninaenda na binti zetu mapacha kanisani mimi mwenyewe kila wiki,” Mindy anaeleza. “Ni vigumu sana kujaribu kukaa kwenye mkutano wote wa sakramenti na watoto wawili wachanga, lakini dada yangu anayehudumia amejichukulia jukumu la kunisaidia.

“Yeye huketi pamoja nasi na hunisaidia kuwatunza binti zangu kila wiki. Kuwa tu karibu na yeye humaanisha mengi na husaidia kupunguza wasiwasi wangu katika nyakati zao za kuhamaki au kutotulia. Sidhani kama atawahi kujua ni kwa jinsi gani vitendo vyake vimenisaidia wakati huu katika maisha yangu. Aliona hitaji langu kama mama kijana, aliyejawa na wasiwasi, na yeye husaidia kulifanya kanisa kuwa mahali pa amani na furaha kwetu sote.”

Mawazo ya Kuwasaidia Wale wenye Mahitaji Maalum

  • Toa ripoti kwa viongozi wa akidi ya wazee na Muungano wa Usaidizi wa Akina Mama kuhusu mahitaji ya waumini.

  • Viongozi hupanga hotuba za mkutano wa sakramenti ili kusaidia kukidhi mahitaji ya waumini. Ikiwa wale mnaowahudumia watafaidika kwa kusikia ujumbe fulani, shiriki wazo hilo pamoja na viongozi wako.

  • Ikiwa unajua kuwa mtu fulani ana ulemavu au mzio wa chakula ambao unamzuia kufurahia baraka za sakramenti, waulize kiundani kujua na ni marekebisho gani yangeweza kufanywa ili kuboresha uzoefu wao wa ibada. Shiriki taarifa hii pamoja na viongozi wako.

  • Ikiwa mtu unayemhudumia au kumfahamu yuko nyumbani, ameshindwa kutoka kabisa au ameshindwa kutoka kwa muda, muulize askofu wako kama sakramenti inaweza kutolewa kwao wakiwa nyumbani. Ungeweza hata kuandika muhtasari wakati wa mkutano wa sakramenti na kuushiriki kwa simu, kupitia barua pepe, au wewe binafsi.

  • Ikiwa mtu unayemhudumia ana watoto wadogo, unaweza kujitolea kuwasaidia wakati wa mkutano wa sakramenti.

  • Ikiwa wale unaowahudumia hawaji kwenye mkutano wa sakramenti, jaribu kuelewa na kufikiria njia za kuweza kuwasaidia. Ikiwa wanahitaji usafiri, ungeweza kuwapatia. Ikiwa wanahisi hawaungwi mkono na familia zao, ungeweza kuwaalika kukaa nao kwenye mkutano wa sakramenti. Ungeweza kutoa mialiko maalum ya kuwasaidia kuhisi wanakaribishwa na wanahitajika kwenye mkutano wa sakramenti.

Kumbuka, Ishara Rahisi Huenda Mbali Sana

Akiongea kuhusu kuhudumu, Dada Jean B. Bingham, Rais wa Muungano wa Usaidizi wa Akina Mama alifundisha: “Wakati mwingine tunadhani tunapaswa kufanya kitu kikubwa na cha kishujaa ‘kuhesabika’ kama tumewatumikia jirani zetu. Bado matendo madogo ya huduma yanaweza kuwa na athari kubwa kwa wengine—vilevile kwetu wenyewe.”1

Katika kata ndogo huko Ubelgiji, Evita mara nyingi anajitolea kutafsiri kwa ajili ya wageni na wanachama wanaoongea Kihispania wakati wa mikutano ya sakramenti. Wakati fulani, Evita alitambulishwa kwa mtu kutoka Jamhuri ya Dominika ambaye alikuwa anajifunza kuhusu Kanisa. Alijua Kiingereza kidogo, lakini Kihispania ilikuwa lugha yake ya asili. Kwa hivyo Evita alijitolea kimya kimya kumtafsiria kwenye mkutano wa sakramenti hivyo alijisikia vizuri zaidi.

Kutafsiri wakati mwingine kunaweza kuifanya Sabato yangu kuwa ya kusisimua,” Evita anasema. “Lakini kufuata mwongozo wa kuwauliza wengine ikiwa wanahitaji mtafsiri hakika hunipa hisia za furaha na husisimua kwa kujua kuwa ninaweza kuwasaidia kumhisi Roho na kufurahia mikutano yao.”

Mawazo ya Kusaidia kupitia Ishara Rahisi

  • Ongea na viongozi wako kuona ni nani anayehitaji huduma ya ziada wakati wa mkutano wa sakramenti. Au kama unamjua mtu yeyote anayehitaji, hakikisha viongozi wako wanawajua.

  • Kaa kimya ukiwa unasubiri mkutano kuanza. Hii itasaidia “mioyo mingine iliyovunjika na roho za huzuni ambazo zinatuzunguka”2 ambao wanahitaji amani ambayo inaweza kuja kupitia heshima katika mahali patakatifu.

  • Jumapili ya mfungo, fikiria kuwekea mkazo kufunga kwako na sala juu ya mtu ambaye unamuhudumia ambaye anaweza kuwa anahitaji ufariji wa ziada.

  • Sali ili kujua kama kuna mtu ambaye anaweza kufaidika kwa wewe kukaa karibu yake au karibu yao wakati wa mkutano wa sakramenti au kama kuna njia nyingine unayoweza kusaidia.

Mkutano wa Sakramenti Unaweza kuwa Mahali pa Kukaribishwa kwa ajili ya Watu Wote

Joseph Fielding Smith (1876-1972) alifundisha, “Mkutano wa sakramenti ndio muhimu sana, mtakatifu sana, kati ya mikutano yote ya Kanisa.”3 Katika hali hiyo, ni muhimu kuhakikisha kuwa wote wanaohudhuria mkutano wa sakramenti wanahisi wanakaribishwa na kulishwa kiroho—hususani waumini wapya au waumini ambao hawajahudhuria kwa muda.

Merania kutoka New South Wales, Australia, alijenga urafiki na mwanamke ambaye alikuwa akijifunza kuhusu Kanisa katika kata yake. “Yeye amekuwa mmoja wa marafiki zangu wapenzi,” Merania anasema. “Ninapenda kukaa naye katika mkutano wa sakramenti kila wiki, na mara zote huwa ninauliza jinsi anavyoendelea na iwapo kuna chochote ninachoweza kufanya ili kumsaidia.” Baada ya muda, rafiki wa Merania alibatizwa. Juhudi za waumini wa kata, pamoja na mazingira ya ukaribishwaji katika mkutano wa sakramenti, vilisaidia sana katika uamuzi wake.

Mawazo ya Kuhudumia Waumini Wanaorudi kushiriki au Wapya

  • Wakati unapokwenda kuongea kwenye mkutano wa sakramenti, ungeweza kuwaalika marafiki, familia, na wengine kuja kusikia ujumbe wako.

  • Unaweza kuwatafuta na kuwakaribisha wale ambao wako peke yao au ambao wanaweza kuhitaji msaada. Waombe iwapo unaweza kukaa karibu yao au waalike kukaa pamoja nawe.

  • Wakati mkutano unapokwisha, unaweza kuwaalika wengine na wale unaowahudumia kwenye shughuli zijazo za Kanisa, hekaluni, au hafla ya kijamii.

  • Ikiwa mtu unayemhudumia huja kwenye mkutano wa sakramenti lakini hajafanya hivyo kwa muda, unaweza kuwauliza kama walikuwa na maswali juu ya kile kilichofundishwa. Waambie wanakaribishwa wakati wote kukufuata ikiwa kuna neno, hadithi, au sehemu ya mafundisho ambayo hawakuielewa. Mnaweza kutafuta majibu kwa pamoja kama ikibidi.

Muhtasari

  1. Jean B. Bingham, “Kutumikia kama Mwokozi Anavyofanya,” Liahona, Mei 2018,106.

  2. Jeffrey R. Holland, “Tazama Mwana Kondoo wa Mungu,” Liahona, Mei 2019, 46.

  3. Joseph F. Smith, katika Ripoti ya Mkutano, Oktoba 1929, 60-61.