Vitabu vya Maelekezo na Miito
38. Sera na Miongozo ya Kanisa


“38. Sera na Miongozo ya Kanisa ,” Kitabu cha Maelezo ya Jumla: Kuhudumu katika Kanisa la Yesu Kristo la Watakatifu wa Siku za Mwisho (2020).

“38. Sera na Miongozo ya Kanisa ,” Kitabu cha Maelezo ya Jumla.

38.

Sera na Miongozo ya Kanisa

38.6

Sera juu ya Masuala ya Uadilifu

Sera chache katika sehemu hii ni kuhusu mambo ambayo Kanisa “hupinga.” Waumini wa Kanisa kwa kawaida hawana uzoefu wa vizuizi vya uumini kwa sababu ya maamuzi yao kuhusu mambo haya. Hata hivyo, watu wote hatimaye wanawajibika kwa Mungu kwa maamuzi yao.

38.6.1

Kutoa Mimba

Bwana aliamuru, Usiue …, wala kufanya kitu chochote kama hicho” (Mafundisho na Maagano 59:6). Kanisa linapinga utoaji mimba kwa hiari kwa uchaguzi wa mtu binafsi au mazingira ya kijamii. Waumini wasikubali kuwa radhi, kufanya, kupanga kwa ajili ya, kulipia, au kuhimiza utoaji mimba. Hali pekee zinazoruhusu ni wakati:

  • Mimba imetokana na ubakaji au kujamiiana kwa maharimu.

  • Daktari mwenye weledi anapoamua kwamba maisha au afya ya mama ipo katika hatari kubwa.

  • Daktari mwenye weledi anapoamua kwamba kijusi kina kasoro kubwa ambazo hazitaruhusu mtoto kuishi baada ya kuzaliwa.

Hata mambo haya yasiyo ya kawaida hayahalalishi mara moja utoaji mimba. Utoaji mimba ni jambo zito sana na linapaswa kufikiriwa tu baada ya watu wanaohusika kuwa wameshauriana na maaskofu wao na kupokea uthibitisho mtakatifu kupitia sala.

Maafisa viongozi kwa uangalifu wanatathmini hali ikiwa muumini wa Kanisa amehusika na utoaji mimba. Baraza la uumini linaweza kuwa la lazima ikiwa muumini anakubali kushiriki, kufanya, kupanga kwa ajili ya, kulipia, au kuhimiza utoaji mimba (ona 32.6.2.5). Hata hivyo, baraza la uumini halipaswi kufikiriwa ikiwa muumini alihusika katika utoaji mimba kabla ya ubatizo. Wala mabaraza ya uumini au vizuizi havipaswi kufikiriwa kwa ajili ya waumini ambao walikuwa wamehusika katika utoaji mimba kutokana na sababu yoyote kati ya tatu zilizoainishwa mapema katika kipengele hiki.

Askofu anapeleka maswali ya mambo mahususi kwa rais wa kigingi. Rais wa kigingi anaweza kuelekeza maswali kwenye ofisi ya Urais wa Kwanza ikiwa ni lazima.

Kadri ambavyo imefunuliwa, mtu anaweza kutubu na kusamehewa kwa ajili ya dhambi ya utoaji mimba.

38.6.2

Unyanyasaji

Unyanyasaji ni kutendewa vibaya au kutelekeza wengine katika njia inayosababisha madhara kimwili, kijinsia, kihisia, au madhara ya kifedha. Msimamo wa Kanisa ni kwamba unyanyasaji hauwezi kuvumiliwa kwa jinsi yoyote. Wale wanaowanyanyasa wake, waume, watoto, wanafamilia wengine, au yoyote yule wanakiuka sheria za Mungu na za binadamu.

Waumini wote, hususani wazazi na viongozi, wanahimizwa kuwa macho na wenye bidii na kufanya yote wanayoweza kuwalinda watoto pamoja na wengine dhidi ya unyanyasaji. Ikiwa waumini wanafahamu juu ya matukio wa unyanyasaji, wanatoa ripoti kwa mamlaka za kiraia na kushauriana na askofu. Viongozi wa Kanisa wanapaswa kuchukua ripoti za unyanyasaji kwa uzito mkubwa na kamwe wasizidharau.

Watu wazima wote wanaofanya kazi na watoto au vijana wanatakiwa kukamilisha mafunzo ya kuwalinda watoto na vijana ndani ya mwezi mmoja wa kukubaliwa (ona ProtectingChildren.ChurchofJesusChrist.org). Wanatakiwa kurudia mafunzo kila baada ya miaka mitatu.

Wakati unyanyasaji unapotokea, wajibu wa kwanza na wa haraka wa viongozi wa Kanisa ni kuwasaidia wale walionyanyaswa na kuwalinda wahanga kutokana na unyanyasaji wa baadae. Viongozi hawapaswi kumtia moyo mtu kubaki katika nyumba au hali ambayo ni ya unyanyasaji au isiyo salama.

38.6.2.1

Namba ya Msaada dhidi ya Unyanyasaji

Katika baadhi ya nchi, Kanisa limeanzisha namba za msaada wa siri dhidi ya unyanyasaji kuwasaidia marais wa vigingi na maaskofu. Viongozi hawa wanapaswa mara moja kupiga namba za msaada dhidi ya unyanyasaji kuhusu kila hali ambayo mtu anaweza kuwa amenyanyaswa—au yuko katika hatari ya kunyanyaswa. Wanapaswa pia kuipiga kama wanafahamu muumini anaangalia, kununua, au kusambaza ponografia ya watoto.

Namba ya msaada inapatikana kwa ajili ya maaskofu na marais wa vigingi kupiga saa 24 siku 7 kwa wiki. Namba za simu zimeoneshwa hapo chini.

  • Marekani na Kanada: 1:-801-240-1911 au 1-800-453-3860, mkondo 2-1911

  • Uingereza:0800 970 6757

  • Ireland:1800 937 546

  • Ufaransa: 0805 710 531

  • Australia: 02 9841 5454 (kutoka ndani ya nchi)

  • New Zealand: 09 488 5592 (kutoka ndani ya nchi)

Maaskofu na marais wa vigingi wanapaswa kupiga namba ya msaada wakati wanaposhughulikia hali zinazohusiana na aina yoyote ya unyanyasaji. Wataalamu wa sheria na matabibu watajibu maswali yao. Wataalamu hawa watatoa pia maelekezo kuhusu jinsi ya:

  • Kawasaidia wahanga na kusaidia kuwalinda kutokana na unyanyasaji zaidi.

  • Kusaidia kuwalinda wengine wanaoweza kuwa wahanga.

  • Kukubaliana na matakwa ya sheria kwa ajili ya kuripoti unyanyasaji.

Kanisa limejitolea kutii sheria katika kuripoti unyanyasaji (ona 38.6.2.1). Sheria zinatofautiana kulingana na mahali, na viongozi wa Kanisa walio wengi sio wataalamu wa sheria. Kupiga namba ya msaada ni muhimu kwa ajili ya maaskofu na marais wa vigingi kutimiza wajibu wao wa kuripoti unyanyasaji.

Askofu anapaswa pia kumtaarifu rais wake wa kigingi juu ya matukio ya unyanyasaji.

Katika nchi ambazo hazina nambari za msaada, askofu anayepata habari juu ya unyanyasaji anapaswa kumwarifu rais wake wa kigingi. Rais wa kigingi anapaswa kuomba mwongozo kutoka kwa mshauri wa sheria wa eneo kwenye ofisi ya eneo. Pia anahimizwa kushauriana na wafanyakazi wa Huduma za Familia au meneja wa ustawi wa jamii na kujitegemea kwenye ofisi ya eneo.

38.6.2.3

Unyanyasaji wa Watoto au Vijana

Unyanyasaji wa mtoto au kijana ni dhambi kubwa (ona Luka 17:2). Kama lilivyotumika hapa, Unyanyasaji wa mtoto au kijana unajumuisha yafuatayo:

  • Unyanyasaji wa kimwili: Kusababisha madhara makubwa ya mwili kwa nguvu za kimwili. Baadhi ya madhara yanaweza yasionekane.

  • Ubakaji au unyanyasaji kijinsia: Kuwa na aina yoyote ya shughuli za kujamiiana na mtoto au kijana au kwa makusudi kuruhusu au kuwasaidia wengine kuwa na shughuli kama hizo. Kama ilivyotumika hapa, unyanyasaji wa kijinsia haujumuishi kujamiiana kwa kukubaliana kati ya watoto wawili ambao wanakaribiana kiumri.

  • Unyanyasaji wa kihisia: Kutumia vitendo na maneno kuharibu vibaya hisia za mtoto au kijana za kujiheshimu au ustahiki binafsi. Hii mara nyingi inahusisha matusi yanayoendelea na kurudiwa rudiwa, hila, na ukosoaji ambao unaaibisha na kudhalilisha. Inaweza pia kujumuisha utelekezaji wa dhahiri.

  • Ponografia ya mtoto: Ona 38.6.6.

Ikiwa askofu au rais wa kigingi anapata habari au anashuku unyanyasaji wa mtoto au kijana, mara moja anafuata maelekezo katika 38.6.2.1. Pia anachukua hatua kusaidia kuwalinda dhidi ya unyanyasaji zaidi.

Baraza la uumini la Kanisa na ufafanuzi wa rekodi vinahitajika kama muumini mtu mzima anamnyanyasa mtoto au kijana kama ilivyoelezwa katika sehemu hii. Ona pia 32.6.1.1 na 38.6.2.5.

Kama mtoto mwenye umri chini ya miaka 18 anamnyanyasa mtoto mdogo, rais wa kigingi anawasiliana na Ofisi ya Urais wa Kwanza kwa ajili ya maelekezo.

Uonevu kimwili au kihisia kati ya watoto na vijana wa umri unaofanana unapaswa kushughulikiwa na viongozi wa kata. Baraza la uumini haliitishwi.

38.6.2.4

Unyanyasaji wa mume au mke au mtu mzima mwingine

Unyanyasaji wa mume au mke au mtu mzima mwingine unaweza kutokea katika njia nyingi. Hizi zinajumuisha kimwili, kijinsia, kihisia, na unyanyasaji wa kifedha. Watu wazima ambao ni wazee, wenye kuweza kudhurika, au walemavu wakati mwingine wapo kwenye hatari kubwa ya unyanyasaji.

Mara nyingi hakuna ufafanuzi mmoja wa unyanyasaji ambao unaweza kutumika katika hali zote. Badala yake, kuna wigo mpana wa matumizi ya nguvu katika tabia ya unyanyasaji. Wigo huu unaanzia kwenye kutumia maneno makali mara kadhaa mpaka kwenye madhara makubwa.

Kama askofu au rais wa kigingi anapata habari ya unyanyasaji wa mke au mume, au mtu mzima mwingine, mara moja anafuata maelekezo katika 38.6.2.1. Pia anachukua hatua kusaidia kuwalinda dhidi ya unyanyasaji zaidi.

Viongozi wanatafuta mwongozo wa Roho kuamua kama ushauri binafsi au baraza la uumini ni mahala pazuri pa kushughulikia unyanyasaji. Wanaweza pia kushauriana na viongozi wao wa ukuhani kuhusu mazingira. Hata hivyo, unyanyasaji wa aina yoyote wa mke au mume au mtu mzima mwingine ambao unafikia kiwango kilichoelezwa hapo chini unahitaji kufanyika kwa baraza la uumini.

  • Unyanyasaji wa kimwili: Kusababisha madhara makubwa ya mwili kwa nguvu za kimwili. Baaadhi ya madhara yanaweza yasionekane.

  • Unyanyasaji wa kijinsia: Ona hali zilizoelezwa bayana katika 38.6.18.3.

  • Unyanyasaji wa kihisia: kutumia vitendo na maneno kuharibu vibaya hisia za mtu za kujiheshimu au ustahiki binafsi. Hii mara nyingi inahusisha matusi yanayoendelea na kurudiwa rudiwa, hila, na ukosoaji ambao unaaibisha na kudhalilisha.

  • Unyanyasaji kifedha: Kumdanganya mtu fulani kifedha. Hii inaweza kujumuisha matumizi yasiyo halali au ambayo hayakuidhinishwa ya mali ya mtu, fedha, au vitu vingine vya thamani. Inaweza pia kujumuisha kupata kwa udanganyifu nguvu ya kifedha juu ya mtu fulani. Inaweza kujumuisha kutumia nguvu ya fedha kulazimisha tabia fulani. Ona pia 32.6.1.3.

38.6.2.7

Masuala ya Kisheria Yanayohusiana na Unyanyasaji

Ikiwa shughuli za unyanyasaji za muumini zimekiuka sheria zinazotumika, askofu au rais wa kigingi, anapaswa kumsihi muumini kuripoti shughuli hizi kwa mtumishi mtekelezaji wa sheria au mamlaka sahihi za serikali. Askofu au rais wa kigingi anaweza kupata taarifa kuhusu masharti ya kuripoti kupitia namba ya simu ya Kanisa (ona 38.6.2.1). Ikiwa waumini wana maswali kuhusu masharti ya kuripoti, anawahimiza kupata ushauri wa kisheria wenye vigezo vinavyohitajika.

Viongozi wa Kanisa na waumini wanapaswa kutimiza wajibu wote wa kisheria wa kutoa taarifa za unyanyasaji kwa mamlaka za umma. Katika baadhi ya maeneo, viongozi na walimu wanaofanya kazi na watoto na vijana wanachukuliwa kama “watoa habari wenye mamlaka” na lazima waripoti unyanyasaji kwenye mamlaka za sheria. Vilevile, katika maeneo mengi, mtu yoyote anayepata habari ya unyanyasaji anatakiwa kuiripoti kwenye mamlaka za sheria. Maaskofu na marais wa vigingi wanapaswa kupiga namba ya msaada kwa ajili ya taarifa zaidi kuhusu watoa taarifa wenye mamlaka na masharti mengine ya kisheria kwa ajili ya kuripoti unyanyasaji. Sera ya Kanisa ni kutii sheria.

38.6.5

Usafi wa Kimwili na Uadilifu

Sheria ya Bwana ya Usafi wa kimwili ni:

  • Kujinyima mahusiano ya kujamiiana nje ya ndoa kati ya mwanamume na mwanamke kulingana na sheria ya Mungu.

  • Uadilifu ndani ya ndoa.

Vitendo vya kimwili vya kimapenzi kati ya mume na mke vinakusudiwa kuwa vizuri na vitakatifu. Vimeamriwa na Mungu kwa ajili ya uumbaji wa watoto na kwa ajili ya kuonyesha upendo kati ya mume na mke.

Mwanamume na mwanamke ambao wameoana kihalali na kwa kufuata sheria kama mume na mke ndiyo pekee wanapaswa kuwa na mahusiano ya kujamiiana. Mbele za Mungu, usafi wa maadili ni muhimu sana. Ukiukwaji wa sheria ya usafi wa kimwili ni kosa kubwa (ona Kutoka 20:14; Mathayo 5:28; Alma 39:5). Wale wanaohusika hutumia vibaya nguvu takatifu Mungu aliyoitoa kwa ajili ya uumbaji wa maisha.

Baraza la uumini la Kanisa linaweza kuwa la lazima ikiwa Muumini:

  • Ana mahusiano ya kimapenzi nje ya mahusiano ya ndoa yaliyoruhusiwa na sheria ya Mungu, kama vile uasherati, uzinzi, na mahusiano ya jinsia moja (ona 32.6.2).

  • Yupo katika mfano wa ndoa, au ubia ambao ni kinyume na sheria ya Mungu, kama vile kukaa pamoja kinyumba, muungano na ubia wa kiraia na ndoa ya jinsia moja.

  • Anatumia ponografia kwa wingi au kwa kulazimishwa, anasababisha madhara makubwa kwa ndoa au familia ya muumini (ona 38.6.13).

Uamuzi kuhusu ikiwa baraza la uumini liitishwe katika hali hizi hutegemea mambo mengi. Haya yamebainishwa katika 32.7. Kwa mfano, kukiuka maagano ya hekaluni kunaongeza uwezekano wa baraza kuwa la lazima ili kumsaidia mtu atubu. Katika baadhi ya hali, ushauri binafsi na vizuizi visivyo rasmi vya uumini vinaweza kutosha (ona 32.8).

Ona 32.6.1.2 kujua ni wakati gani baraza linahitajika kwa ajili ya dhambi za uzinzi na uasherati.

38.6.6

Ponografia ya Watoto

Kanisa linalaani ponografia ya mtoto ya aina yoyote ile. Ikiwa askofu au rais wa kigingi anapata habari ya kwamba muumini anahusika na Ponografia ya mtoto, mara moja anafuata maelekezo kwenye 38.6.2.1.

Baraza la uumini la Kanisa na ufafanuzi wa rekodi vinahitajika ikiwa muumini anatengeneza, anashiriki, anamiliki, au anarudia rudia kuangalia picha za ponografia za watoto (ona 32.6.1.2 na 32.14.5). Mwongozo huu kwa kawaida hautumiki kwa watoto au vijana wa takribani umri sawa wanaoshiriki picha zao za ngono au za wengine. Ushauri binafsi na vizuizi vya uumini visivyo rasmi vinaweza kufaa katika hali kama hizo.

Kwa maelezo zaidi, ona 38.6.13.

38.6.10

Kujamiiana kwa maharimu (kujamiiana kwa ndugu wa karibu)

Kanisa linalaani aina yoyote ya kujamiiana kwa maharimu. Kama ilivyotumika hapa, kujamiiana kwa maharimu ni mahusiano ya kimapenzi kati ya:

  • Mzazi na mtoto.

  • Babu ua Bibi na mjukuu.

  • Ndugu (wa baba na mama mmoja)

  • Mjomba au shangazi na mpwa (mtoto wa kiume au kike wa kaka au dada)

Kama ilivyotumika hapa, mtoto, mjukuu, ndugu, mpwa wa kike, na mpwa wa kiume hujumuisha mahusiano ya kibaiolojia, kuasili, ya kambo, au ya malezi. Kujamiiana kwa maharimu kunaweza kutokea kati ya watoto wawili, mtu mzima na mtoto, au watu wazima wawili. Ikiwa rais wa kigingi ana maswali kuhusu kama mahusiano ni ya kujamiiana baina ya maharimu chini ya sheria za eneo husika, anatafuta mwongozo kutoka Ofisi ya Urais wa Kwanza.

Wakati mtoto ni mhanga wa kujamiiana kwa maharimu, askofu au rais wa kigingi anapiga simu ya msaada dhidi ya unyanyasaji katika nchi ambapo inapatikana (ona 38.6.2.1). Katika nchi zingine, rais wa kigingi anapaswa kutafuta mwongozo kutoka kwa mshauri wa sheria wa eneo kwenye ofisi ya eneo. Pia anahimizwa kushauriana na Wahudumu wa Familia au meneja wa ustawi wa jamii na kujitegemea kwenye ofisi ya eneo.

Baraza la uumini wa Kanisa na ufafanuzi wa rekodi vinahitajika ikiwa muumini amefanya kosa la kujamiiana kwa maharimu (ona 32.6.1.2 na 32.14.5). Kujamiiana kwa maharimu kwa kawaida mara zote huitaji Kanisa kuondoa uumini wa mtu.

Kama mtoto mwenye umri chini ya miaka 18, amejamiiana kwa maharimu rais wa kingingi anawasiliana na Ofisi ya Urais wa Kwanza kwa ajili ya maelekezo.

Wahanga wa kujamiiana kwa maharimu mara nyingi wanateseka na kiwewe kizito. Viongozi wanajibu kwa huruma ya dhati na kujali. Wanatoa msaada wa kiroho na ushauri kuwasaidia kushinda athari za uharibifu wa kujamiiana kwa maharimu.

Wakati mwingine wahanga wana hisia za aibu na hatia. Wahanga hawana hatia ya dhambi. Viongozi wanawasaidia wao na familia zao kuelewa upendo wa Mungu na uponyaji ambao unakuja kupitia Yesu Kristo na Upatanisho Wake (ona Alma 15:8; 3 Nefi 17:9).

Kwa nyongeza kwenye kupokea msaada wenye mwongozo kutoka kwa viongozi wa Kanisa, wahanga na familia zao wanaweza kuhitaji ushauri wa kitaalamu. Kwa maelezo, ona 38.6.18.2.

38.6.13

Ponografia

Kanisa linalaani ponografia ya aina yoyote. Matumizi ya aina yoyote ya ponografia yanaharibu maisha ya mtu binafsi, familia, na jamii. Pia yanamfukuza Roho wa Bwana. Waumini wa Kanisa wanapaswa kuepuka aina zote za ponografia na kupinga uzalishaji wake, uenezaji, na matumizi yake.

Kanisa linatoa nyezo zifuatazo kuwasaidia watu ambao maisha yao yameathiriwa na ponografia:

Marais wa vigingi na maaskofu pia wanatoa msaada kwa wanafamilia kama inavyotakiwa.

Viongozi wa kanisa wanapaswa kutambua kwamba matumizi ya ponografia yanaweza kuwa shurutisho au uraibu. Kwa nyongeza kwenye msaada wenye mwongozo wa viongozi hawa, baadhi ya waumini wanaweza kuhitaji ushauri wa kitaalamu. Viongozi wanaweza kuwasiliana na Huduma za Familia kwa ajili ya msaada. Ona 31.2.6 kwa ajili ya maelezo ya mawasiliano.

Ushauri binafsi na vizuizi vya uumini visivyo rasmi kwa kawaida vinanatosha wakati wa kumsaidia mtu atubu kutokana na kutumia ponografia (ona 32.8). Mabaraza ya uumini kwa kawaida si ya lazima. Hata hivyo, baraza linaweza kuwa la lazima kwa ajili ya matumizi makubwa na ya kulazimisha ya utumiaji wa ponografia ambayo yamesababisha madhara makubwa kwa ndoa ya muumini au familia (ona 38.6.5). Baraza linahitjika ikiwa muumini anatengeneza, anashiriki, anamiliki, au anarudia rudia kuangalia picha za ponografia za watoto (ona 32.6.1.2).

38.6.18

Unyanyasaji wa Kijinsia, Ubakaji, na Aina Zingine za Shambulio la Kingono

Kanisa linalaani unyanyasaji wa kijinsia. Kama lilivyotumika hapa, unyanyasaji wa kijinsia unafafanuliwa kama kulazimisha shughuli za kingono zisizotakiwa kwa mtu mwingine. Shughuli za kingono na mtu ambaye hataki au hawezi kutoa idhini ya kisheria inafikiriwa ni unyanyasaji wa kijinsia. Unyanyasaji wa kijinsia unaweza pia kutokea kwa mume au mke au katika mahusiano ya miadi. Kwa taarifa kuhusu unyanyasaji wa kijinsia wa mtoto au kijana, ona 38.6.2.3.

Unyanyasaji wa kijinsia unajumuisha matendo mengi kuanzia usumbufu mpaka ubakaji na aina zingize za mashambulio ya kingono. Unaweza kutokea kimwili, kwa maneno na katika njia nyinginezo. Kwa ajili ya mwongozo kuhusu kuwashauri waumini waliopata uzoefu wa unyanyasaji wa kijinsia, kubakwa, au aina zingine za unyanyasaji wa kijinsia, ona 38.5.18.2.

Kama muumini anashuku au anafahamu juu ya unyanyasaji wa kijinsia, wanachukua hatua kuwalinda wahanga pamoja na wengine haraka iwezekanavyo. Hii inajumuisha kuripoti kwa mamlaka za kiraia na kumtahadharisha askofu au rais wa kigingi. Kama mtoto amenyanyaswa, waumini wanapaswa kufuata maelekezo katika 38.6.2.

38.6.18.3

Mabaraza ya Uumini

Baraza la uumini linaweza kuwa la lazima kwa ajili ya mtu ambaye amemshambulia kijinsia au amemnyanyasa mtu fulani. Baraza la uumini linahitajika kama muumini alibaka au ametiwa hatiani kwa aina nyingine ya unyanyasaji wa kijinsia (ona 32.6.1.1)

Baraza lazima pia lifanyike kwa shughuli za kingono zilizofanyika kwa watu wazima wenye kuweza kudhuriwa. Kama ilivyotumika hapa, mtu mzima mwenye kuweza kudhuriwa ni mtu ambaye, kwa sababu ya mapungufu ya kimwili au kiakili, aidha hana uwezo wa kukubali kufanyiwa kitendo hicho au hawezi kuelewa asili ya kitendo hicho.

Kushughulikia aina zingine za unyanyasaji wa kijinsia, viongozi wanatafuta mwongozo wa Roho kuhusu ikiwa ushauri binafsi au baraza la uumini ni mpangilio unaofaa zaidi (ona 32.6.2.2 na 32.8). Katika hali nzito baraza linahitajika. Viongozi wanaweza kushauriana na viongozi wao wa ukuhani kuhusu jambo hilo.

Ikiwa vizuizi vya uumini ni matokeo ya baraza la uumini ambalo limefanywa kwa ajili ya mkosaji wa unyanyasaji wa kijinsia, uumini wa mtu huyo unatiwa maelezo.

Kwa maelezo kuhusu kushauri katika mambo ya unyanyasaji, ona 38.6.2.2. Kwa maelezo kuhusu kuwashauri wahanga wa unyanyasaji wa kijinsia, ona 38.6.18.2.

38.6.23

Watu Binafsi waliobadilisha jinsia

Watu binafsi waliobadilisha jinsia wanakumbana na changamoto zisizoelezeka kirahisi. Waumini na wasio waumini ambao wanajitambulisha kama waliobadilisha jinsia—na familia zao na marafiki—wanapaswa kutendewa kwa hisia, huruma, upole, na wingi wa upendo kama ule wa Kristo. Wote wanakaribishwa kuhudhuria mikutano ya sakramenti, mikutano mingine ya Jumapili, na matukio mengine ya kijamii ya Kanisa (ona 38.1.1).

Jinsia ni tabia muhimu ya mpango wa furaha wa Baba wa Mbinguni. Maana iliyokusudiwa ya jinsia katika tangazo la familia ni jinsia ya kibaiolojia wakati wa kuzaliwa. Baadhi ya watu wanapata uzoefu usiopatana kati ya jinsia yao ya kibaiolojia na utambulisho wao wa jinsia. Matokeo yake, wanaweza kujitambulisha kama waliobadili jinsia. Kanisa halina upande wowote kwenye sababu za watu kujitambulisha wenyewe kama waliobadili jinsia.

Ushiriki mwingi Kanisani na baadhi ya ibada za hekaluni hazibagui jinsia. Watu waliobadilisha jinsia wanaweza kubatizwa na kuthibitishwa kama ilivyobainishwa katika 38.2.3.14. Wanaweza pia kushiriki sakramenti na kupokea baraka za ukuhani. Hata hivyo, kutawazwa kwenye ukuhani na ibada za hekaluni zinapokelewa kulingana na jinsia ya kibaiolojia wakati wa kuzaliwa.

Viongozi wa Kanisa wanashauri dhidi ya uchaguzi wa kuingilia kitiba au kiupasuaji kwa lengo la kujaribu kubadili jinsia kinyume na ile ya kibaiolojia ya mtu wakati wa kuzaliwa (“ubadilishaji wa jinsia”). Viongozi wanashauri kwamba kufanya vitendo hivi itakuwa sababu kwa vizuizi vya uumini wa Kanisa.

Viongozi pia wanashauri dhidi ya kujibadilisha kijamii. Kujibadilisha kijamii kunajumuisha kubadili mavazi au tabia, au kubadili jina au kiwakilishi cha jina, kujichukulia mwenyewe kama mtu fulani tofauti na jinsia yake ya kibaiolojia wakati wa kuzaliwa. Viongozi wanashauri kwamba wale wanaojibadilisha kijamii watapitia baadhi ya vizuizi vya uumini wa Kanisa kwa kipindi cha mabadiliko haya.

Vizuizi vinajumuisha kupokea au kutumia ukuhani, kupokea au kutumia kibali cha hekaluni, na kupokea baadhi ya miito ya Kanisa. Ingawa baadhi ya haki za uumini wa Kanisa zimezuiwa, ushiriki mwingine Kanisani unakaribishwa.

Watu binafsi waliobadilisha jinsia ambao hawatafuti mabadiliko ya tiba, upasuaji au ya kijamii kwenye jinsia tofauti na wanastahili wanaweza kupokea miito ya Kanisa, vibali vya hekaluni, na ibada za hekaluni.

Baadhi ya watoto, vijana, na watu wazima wanapangiwa matibabu ya homoni na watalaamu wa tiba wenye leseni ili kupunguza hofu mbaya ya jinsia au kupunguza mawazo ya kujiua. Kabla mtu hajaanza matibabu kama hayo, ni muhimu kwamba yeye (na wazazi wa mtoto) waelewe madhara na faida zinazoweza kutokea. Kama waumini hawa hawajaribu kujibadilisha kuwa jinsia nyingine na wanastahili, wanaweza kupokea miito ya Kanisa, vibali vya hekaluni, na ibada za hekaluni.

Ikiwa muumini anachagua kubadili jina lake pendwa au viwakilishi vya jina, jina linalopendwa zaidi litaandikwa kwenye sehemu ya jina pendwa kwenye kumbukumbu za uumini. Mtu anaweza kuitwa kwa jina alipendalo kwenye kata.

Hali zinabadilika sana kutoka kitengo hadi kitengo kingine na mtu hadi mtu. Waumini na viongozi wanashauriana wao kwa wao na pamoja na Bwana. Marais wa Eneo watawasaidia viongozi wa maeneo husika kushughulikia kwa makini hali za watu binafsi. Maaskofu wanashauriana na rais wa kigingi. Marais wa Vigingi na marais wa misheni lazima watafute ushauri kutoka Urais wa Eneo (ona 32.6.3 na 32.6.3.1).

Kwa maelezo zaidi juu ya kuwaelewa na kuwasaidia watu Binafsi waliobadilisha jinsia, ona “Transgender” kwenye ChurchofJesusChrist.org.

38.8

Sera za Kiutawala

38.8.2

Udanganyifu wa Uaminifu

Udanganyifu wa uaminifu unatokea wakati mtu anapotumia vibaya uaminifu au ujasiri wa mtu mwingine ili kumlaghai. Hii inaweza kutokea wakati watu wote wawili wako kundi moja, kama vile Kanisani. Inaweza pia kutokea kwa kutumia vibaya nafasi ya urafiki, au kuaminika, kama vile wito wa Kanisa au mahusiano ya familia. Udanganyifu wa uaminifu kwa kawaida ni kwa ajili ya kufaidika kifedha.

Waumini wa Kanisa wanapaswa wawe waaminifu katika shughuli zao na kutenda kwa uadilifu. Udanganyifu wa uaminifu ni usaliti wenye aibu wa uaminifu na usiri. Wahalifu wa makosa hayo wategemee kushitakiwa kwa kosa la jinai. Waumini wa Kanisa wanaofanya udanganyifu wa uaminifu wanaweza pia kukabiliana na vizuizi vya uumini au kuondolewa. Ona 32.6.2.3 na 32.6.1.3 kwa ajili ya mwongozo kuhusu mabaraza ya uumini kwa ajili ya vitendo vya ulaghai.

Waumini wasitoe maelezo au kudokeza kwamba shughuli zao zimedhaminiwa, na kuidhinishwa na, au zinawakilisha Kanisa au viongozi wake.

38.8.24

Ushauri wa Kisheria kwa ajili ya Masuala ya Kanisa

Wakati msaada wa kisheria unapohitajika kwa ajili ya masuala ya Kanisa, viongozi wanapaswa kuwasiliana na mshauri wa kisheria wa Kanisa. Nchini Marekani na Kanada, rais wa kigingi anawasiliana na ofisi ya Kanisa ya Ushauri Mkuu:

  • 1-800:-453-3860, mkondo 2‑6301

  • 1-801-240-6301

Nje ya Marekani na Kanada, rais wa kigingi anawasiliana na mshauri wa sheria wa eneo kwenye ofisi ya eneo.

38.8.24.1

Ushiriki au Nyaraka kwenye Mashtaka ya Kisheria

Viongozi wa Kanisa hawapaswi kujihusisha kwenye kesi za madai au jinai kwa ajili ya waumini katika vitengo vyao bila kwanza kushauriana na mshauri wa sheria wa Kanisa. Sera kama hii inatumika pia kwenye kuzungumza na, au kuwaandikia wanasheria au wafanyakazi wa mahakama, ikijumuisha kupitia barua pepe.

Viongozi wanapaswa kuzungumza na mshauri wa sheria wa Kanisa ikiwa, katika nafasi zao Kanisani, wao:

  • Wanaamini wanapaswa kushuhudia au kuzungumza katika masuala ya kisheria.

  • Wanahitajika kulingana na mchakato wa kisheria kushuhudia au kuzungumza kwenye masuala ya kisheria.

  • Wameamriwa kutoa ushahidi.

  • Wameombwa kutoa nyaraka au taarifa kwa hiari.

  • Wameombwa kuwasiliana na wanasheria au mamlaka za sheria kuhusu mashtaka ya kisheria, ikiwa ni pamoja na kuhukumu au kesi za mtu kuachiwa huru.

Iwe ni kwa nia nzuri, viongozi wa Kanisa wanaposhiriki taarifa kwenye mashtaka ya kisheria inaweza kutafsiriwa vibaya na yenye kuleta madhara. Kushiriki huko kunaweza kuleta madhara hususani kwa wahanga na familia zao. Kufuata sera za Kanisa pia kunasaidia kuzuia Kanisa kutokana na kuhusishwa kusikofaa katika masuala ya kisheria.

38.8.24.2

Ushuhuda kwenye Mashtaka ya Kisheria

Viongozi wa Kanisa wasishuhudie kwa niaba ya Kanisa katika mashtaka yoyote ya kisheria bila kibali cha awali kutoka Ofisi ya Mshauri Mkuu. Sera hii pia inatumika kwenye kuhukumu na kesi za kuachiwa huru. Viongozi wa Kanisa wasitoe ushahidi wa maneno au maandishi katika uwezo wao wa uongozi bila kibali hiki.

Viongozi hawapaswi kupendekeza au kudokeza kwamba ushuhuda wao katika usikilizaji wa kesi kisheria unawakilisha msimamo wa Kanisa.

Viongozi hawapaswi kushawishi ushuhuda wa shahidi katika usikilizaji wowote wa kesi kisheria.

Taarifa za mawasiliano kwa ushauri wa kisheria wa Kanisa zimetolewa kwenye 38.8.24.