Maandiko Matakatifu
3 Nefi 27


Mlango wa 27

Yesu anaamuru kwamba Kanisa liitwe kwa jina Lake—Misheni Yake na dhabihu ya kulipia dhambi ndivyo hufanya injili Yake—Watu wanaamrishwa kutubu na kubatizwa ili waweze kutakaswa na Roho Mtakatifu—Inawapasa wawe hata vile Yesu alivyo. Karibia mwaka 34–35 B.K.

1 Na ikawa kwamba vile wanafunzi wa Yesu walipokuwa wakisafiri na kuhubiri vitu ambavyo walikuwa wamesikia na kuona, na walikuwa wakibatiza katika jina la Yesu, ikawa kwamba wanafunzi walijikusanya pamoja na kushirikiana kwa sala kuu na kufunga.

2 Na Yesu tena alijidhihirisha kwao, kwani walikuwa wanaomba kwa Baba katika jina lake; na Yesu alikuja na kusimama miongoni mwao, na kuwaambia: Ni kitu gani mnachohitaji kwamba niwapatie?

3 Na wakamwambia: Bwana tunataka kwamba utuambie jina ambalo tutaita hili kanisa; kwani kuna ugomvi miongoni mwa watu kuhusu jambo hili.

4 Na Bwana akawaambia: Amin, amin, nawaambia, kwa nini watu wananungʼunika na kubishana kwa sababu ya kitu hiki?

5 Je, hawajasoma maandiko, ambayo yanasema, lazima mjivike juu yenu jina la Kristo, ambalo ni jina langu? Kwani, kwa jina hili ndilo mtaitwa nalo katika siku ya mwisho;

6 Na yeyote atakayechukua jina langu na kuvumilia hadi mwisho, huyo huyo ndiye atakayeokolewa katika siku ya mwisho.

7 Kwa hivyo chochote mtakachofanya, mfanye katika jina langu; kwa hivyo mtaliita kanisa katika jina langu; na mtalingana Baba katika jina langu ili aweze kubariki kanisa kwa ajili yangu.

8 Na linawezaje kuwa kanisa langu isipokuwa liitwe kwa jina langu? Kwani kanisa likiitwa kwa jina la Musa, hapo litakuwa kanisa la Musa; au likiitwa kwa jina la mtu, basi litakuwa kanisa la yule mtu; lakini likiitwa katika jina langu, hapo basi litakuwa kanisa langu, ikiwa kwamba watajengwa juu ya injili yangu.

9 Kweli, nawaambia kwamba mmejengwa juu ya injili yangu; kwa hivyo mtaita vitu vyovyote mtakavyoita katika jina langu; kwa hivyo ikiwa mnalingana kwa Baba, kwa kanisa, ikiwa katika jina langu, Baba atawasikia.

10 Na ikiwa itakuwa hivyo kwamba kanisa limejengwa juu ya injili yangu hapo Baba atafichua kazi yake ndani yake.

11 Lakini ikiwa haitajengwa juu ya injili yangu, na imejengwa kwa vitendo vya watu, au juu ya vitendo vya ibilisi, amin, nawaambia wana shangwe katika vitendo vyao kwa muda, na karibuni mwisho unakuja, na wataangushwa chini na kutupwa kwenye moto, kutoka mahali ambapo hakuna kurudi nyuma.

12 Kwani vitendo vyao huwafuata, kwani ni kwa sababu ya vitendo vyao kwamba wanaangushwa chini; kwa hivyo kumbuka vitu ambavyo nimewaambia.

13 Tazama, nimewapatia injili yangu, na hii ndiyo injili ambayo nimewapatia—kwamba nilikuja kwenye ulimwengu kufanya mapenzi ya Baba, kwa sababu alinituma.

14 Na Baba yangu alinituma ili nipate kuinuliwa juu kwenye msalaba; na baada ya kuinuliwa juu kwenye msalaba, kwamba ningeleta watu wote kwangu, kwamba kama nilivyoinuliwa juu na watu, hata hivyo watu wainuliwe juu na Baba, kusimama mbele yangu, na kuhukumiwa kwa vitendo vyao, ikiwa vitakuwa vizuri au ikiwa vitakuwa viovu.

15 Na kwa sababu hii nimeinuliwa juu; kwa hivyo, kulingana na uwezo wa Baba, nitawaleta watu wote kwangu, ili wapate kuhukumiwa kulingana na vitendo vyao.

16 Na itakuwa kwamba yeyote atakayetubu na kubatizwa katika jina langu atajazwa; na ikiwa atavumilia hadi mwisho, tazama, yeye hatahukumiwa kuwa na hatia mbele ya Baba yangu kwenye ile siku wakati nitakaposimama kuhukumu ulimwengu.

17 Na yule ambaye hatavumilia hadi mwisho, mtu huyo huyo ndiye ataangushwa chini na kutupwa kwenye moto, mahali ambapo hawawezi kurudi nyuma, kwa sababu ya haki ya Baba.

18 Na hili ndilo neno ambalo amewapatia watoto wa watu. Na kwa sababu hii yeye hutimiza maneno ambayo ameyatoa, na hasemi uwongo bali hutimiza maneno yake yote.

19 Na hakuna kitu kichafu kinachoweza kuingia kwenye ufalme wake; kwa hivyo hakuna chochote ambacho huingia kwenye pumziko lake isipokuwa wale ambao wameosha nguo zao ndani ya damu yangu kwa sababu ya imani yao, na kutubu kwa dhambi zao zote, na uaminifu wao hadi mwisho.

20 Sasa hii ndiyo amri: Tubuni ninyi nyote katika sehemu zote za dunia, na mje kwangu na mbatizwe katika jina langu kwamba muweze kutakaswa kwa kupokea Roho Mtakatifu, ili msimame mbele yangu bila mawaa katika siku ya mwisho.

21 Kweli, kweli, nawaambia, hii ni injili yangu; na mnajua vitu ambavyo mnahitajika kufanya katika Kanisa langu; kwani vitendo ambavyo mmeniona nikifanya, hivyo pia mtafanya; kwani yale ambayo mmeniona nikifanya hata hivyo ninyi mtafanya;

22 Kwa hivyo mkifanya hivi vitu heri kwenu, kwani mtainuliwa juu katika ile siku ya mwisho.

23 Andikeni vitu ambavyo mmeona na kusikia, isipokuwa vile ambavyo vimekatazwa.

24 Andikeni vitendo vya hawa watu, ambavyo vitakuwa, hata kama vilivyoandikwa, ya yale ambayo yamekuwepo.

25 Kwani tazama, kutoka kwenye vitabu ambavyo vimeandikwa, na ambavyo vitaandikwa, hawa watu watahukumiwa, kwani kutoka kwa hivyo vitabu vitendo vyao vitajulikana kwa wanadamu.

26 Na tazama, vitu vyote vimeandikwa na Baba; kwa hivyo kutoka kwenye hivyo vitabu ambavyo vitaandikwa, dunia itahukumiwa.

27 Na mjue kwamba ninyi mtakuwa waamuzi wa watu hawa, kulingana na hukumu ambayo nitawapatia ambayo itakuwa haki. Kwa hivyo mnapaswa kuwa watu wa aina gani? Amin, nawaambia, hata vile nilivyo.

28 Na sasa naenda kwa Baba. Na amin, nawaambia, vitu vyovyote mtakavyomuuliza Baba katika jina langu, vitatolewa kwenu.

29 Kwa hivyo, ombeni na mtapokea; bisheni na mtafunguliwa; kwani yule ambaye huuliza hupokea; na kwa yule ambaye hubisha, itafunguliwa.

30 Na sasa tazama, shangwe yangu ni kubwa, hata kwenye utimilifu, kwa sababu yenu, na pia kwa sababu ya kizazi hiki; ndiyo, na hata Baba hufurahi, na pia malaika watakatifu, kwa sababu yenu na hiki kizazi; kwani hakuna mmoja wao aliyepotea.

31 Tazama, ningetaka kwamba muelewe; kwani ninaamanisha hao ambao sasa ni wazima wa hiki kizazi; na hakuna hata ambaye amepotea; na kwa sababu yao, nina utimilifu wa shangwe.

32 Lakini tazama, inanihuzunisha kwa sababu ya kizazi cha nne kutoka kwa hiki kizazi, kwani wameongozwa mbali kama mateka na yeye, hata kama vile mwana wa upotevu; kwani wataniuza kwa fedha, na dhahabu, na kwa hiyo ambayo nondo huharibu na ambayo wezi huvunja na kuingia na kuiba. Na katika ile siku, nitawaadhibu, hata katika kugeuza vitendo vyao juu ya vichwa vyao.

33 Na ikawa kwamba wakati Yesu alipokuwa amemaliza maneno haya, aliwaambia wanafunzi wake: Ingieni ndani ninyi kupitia mlango uliosonga; kwani mlango umesonga na njia ni nyembamba, ambayo inaenda kwa maisha, na kuna wachache ambao huipata; lakini mpana ni mlango, na pana ni njia iendayo kwenye kifo, na kuna wengi ambao huisafiria, mpaka usiku unakuja ambapo hakuna mtu atakayeweza kufanya kazi.