Maandiko Matakatifu
Alma 37


Mlango wa 37

Mabamba ya shaba nyeupe na maandiko mengine yamehifadhiwa ili kuongoza nafsi kwenye wokovu—Wayaredi waliangamizwa kwa sababu ya uovu wao—Viapo vyao vya siri na maagano lazima yaondolewe mbali kutoka kwa watu—Shauriana na Bwana kwa matendo yako yote—Kama Liahona ilivyowaongoza Wanefi, kadhalika neno la Kristo huwaongoza watu kwenye uzima wa milele. Karibia mwaka 74 K.K.

1 Na sasa, mwana wangu Helamani, ninakuamuru kwamba uchukue maandishi ambayo nilikabidhiwa;

2 Na pia ninakuamuru kwamba uandike maandishi ya hawa watu, kulingana na vile nilivyofanya, kwenye mabamba ya Nefi, na uhifadhi vitu hivi vyote vitakatifu ambavyo nimehifadhi, hata kama vile nilivyovihifadhi; kwani ni kwa sababu ya busara kwamba zimewekwa.

3 Na mabamba haya ya shaba nyeupe, ambayo yana michoro, ambayo yana kumbukumbu ya maandiko matakatifu juu yake, ambayo yana nasaba ya babu zetu, hata kutoka mwanzoni—

4 Tazama, unabii umetolewa na babu zetu, kwamba zihifadhiwe na kutolewa kutoka kwa kizazi kimoja hadi kingine, na ziwekwe na kulindwa na mkono wa Bwana mpaka ziwafikie kila taifa, kabila, lugha, na watu, kwamba wafahamu siri zilizomo.

5 Na sasa tazama, ikiwa zitahifadhiwa lazima ziweke mngʼaro wao; ndiyo, na zihifadhi mngʼaro wao; ndiyo, na pia mabamba yote ambayo yana maandiko matakatifu.

6 Sasa labda unadhani kwamba huu ni upuuzi ndani yangu; lakini tazama nakwambia, kwamba kupitia kwa vitu vilivyo vidogo na rahisi vitu vikubwa hutendeka; na njia ndogo mara nyingi hufadhaisha wenye hekima.

7 Na Bwana Mungu hutumia njia zake ili kutimiza kusudi lake kuu na la milele; na kwa njia ndogo sana Bwana hufawadhaisha wale werevu na kutimiza wokovu wa roho nyingi.

8 Na sasa, mpaka sasa imekuwa hekima ndani ya Mungu kwamba vitu hivi vihifadhiwe; kwani tazama, vimeongeza ufahamu wa watu hawa, ndiyo, na kuwasadikisha wengi kuhusu makosa ya njia zao, na kuwaleta kwenye ufahamu wa Mungu wao hadi kwa wokovu wa nafsi zao.

9 Ndiyo, nakwambia wewe, isingekuwa vitu hivi ambavyo maandishi haya yanayo, ambavyo viko kwenye mabamba haya, Amoni na ndugu zake hawangesadikisha maelfu wengi hivyo wa Walamani kuhusu desturi zisizo sawa za baba zao; ndiyo, haya mandishi na maneno yao yaliwaleta kwenye toba; yaani, yaliwaleta kwenye ufahamu wa Bwana Mungu wao, na kufurahi katika Yesu Kristo Mkombozi wao.

10 Na nani anajua lakini kwamba watakuwa njia ya kuwaleta maelfu wengi wao, ndiyo, na pia maelfu wengi wa ndugu zetu wenye shingo ngumu, Wanefi, ambao sasa wanashupaza mioyo yao kwenye dhambi na uovu, kwa ufahamu wa Mkombozi wao?

11 Sasa siri hizi hazijafahamishwa kwangu kabisa; kwa hivyo sitaongea tena.

12 Na ingetosha kwangu kusema zimehifadhiwa kwa kusudi la busara, kusudi ambalo linajulikana na Mungu; kwani yeye hushauri kwa hekima juu ya kazi yake yote, na njia zake ni nyoofu, na mwenendo wake ni ule usiobadilika.

13 Ee kumbuka, kumbuka, mwana wangu Helamani, jinsi amri za Mungu zilivyo kali. Na alisema: Ikiwa utatii amri zangu utafanikiwa nchini—lakini kama huwezi kutii amri zake utatolewa kutoka uwepo wake.

14 Na sasa kumbuka, mwana wangu, kwamba Mungu amekukabidhii vitu hivi, ambavyo ni vitakatifu, ambavyo amevifanya vitakatifu, na pia ambavyo ataviweka na kuvihifadhi kwa nia ya busara ambayo anajua, ili aweze kuonyesha uwezo wake kwa vizazi vijavyo.

15 Na sasa tazama, nakwambia kwa roho ya unabii, kwamba ikiwa utavunja amri za Mungu, tazama, vitu hivi ambavyo ni wakfu vitaondoshwa kutoka kwako kwa uwezo wa Mungu, na utatolewa kwa Shetani, kwamba aweze kukuchunga kama kapi mbele ya upepo.

16 Lakini kama utatii amri za Mungu, na ufanye vitu hivi ambavyo ni vitakatifu kulingana na yale ambayo Bwana amekuamuru ufanye, (kwani lazima uombe msaada wa Bwana kwa vitu vyote ambavyo unataka kuvitumia) tazama, hakuna nguvu za ardhini au jehanamu, zinazoweza kuvichukua kutoka kwako, kwani Mungu ni mwenye uwezo kwa kutimiza maneno yake yote.

17 Kwani atatimza ahadi zake zote ambazo atakuahidi, kwani ametimiza ahadi zake ambazo amewaahidi babu zetu.

18 Kwani aliwaahidi kwamba atahifadhi vitu hivi kwa kusudi la busara kwake, kwamba angeweza kuonyesha nguvu yake kwa vizazi vijavyo.

19 Na sasa tazama, kusudi moja ametimiza, hata kwa kurudisha maelfu wengi wa Walamani kwenye ufahamu wa ukweli; na ameonyesha tena uwezo wake kwao, na pia ataonyesha uwezo wake tena ndani yao kwa vizazi vijavyo; kwa hivyo vitahifadhiwa.

20 Kwa hivyo ninakuamuru, mwana wangu Helamani, kwamba uwe na bidii kwa kutimiza maneno yangu yote, na kwamba uwe na bidii kwa kutii amri za Mungu kama zilivyoandikwa.

21 Na sasa, nitaongea na wewe kuhusu yale mabamba ishirini na nne, kwamba uyahifadhi, ili siri na vitendo viovu, na kazi zao za siri, au kazi za siri za wale watu ambao wemeangamizwa, zingeonyeshwa kwa watu hawa; ndiyo, mauaji yao yote, na wizi, na utekaji nyara wao, na maovu na machukizo yao yote, yangejulikana kwa hawa watu; ndiyo, na kwamba uzihifadhi vitafsiri hivi.

22 Kwani tazama, Bwana aliona kwamba watu wake walianza kufanya kazi gizani, ndiyo, walifanya mauaji ya siri na machukizo; kwa hivyo Bwana alisema, ikiwa hawangetubu wangeamizwa kutoka usoni mwa dunia.

23 Na Bwana akasema: Nitamtayarisha mtumishi wangu Gazelemu, jiwe, ambalo litamulika mwangaza gizani, kwamba niwafahamishe watu wangu ambao wananihudumia, kwamba ningewafahamisha kazi za ndugu zao, ndiyo, kazi zao za siri, kazi zao za gizani, na uovu wao na machukizo yao.

24 Na sasa mwana wangu, hivi vitafsiri zilitayarishwa kwamba neno la Mungu lingetimizwa, ambalo alizungumza, akisema:

25 Nitatoa nje kutoka gizani hadi kwenye mwanga kazi zao za siri na machukizo yao; na wasipotubu nitawaangamiza kutoka uso wa dunia; na nitaleta kwa mwangaza siri zao zote na machukizo yao, kwa kila taifa ambalo kutoka sasa kuendelea litamiliki nchi.

26 Na sasa, mwana wangu, tunajua kwamba hawakutubu; kwa hivyo wameangamizwa, na hivyo neno la Mungu limetimizwa; ndiyo, siri zao za machukizo zimetolewa gizani na kujulikana kwetu.

27 Na sasa, mwana wangu, ninakuamuru uweke viapo vyao, na maagano yao, na mapatano yao ya siri zao za machukizo; ndiyo, na ishara zao zote na miujiza ya hila utaficha kutoka kwa hawa watu, ili wasiyajue, isiwe ikawa waanguke gizani pia na waangamizwe.

28 Kwani tazama, kuna laana juu ya nchi hii yote, kwamba maangamizo yatafika juu ya wale wote wanaofanya kazi gizani, kulingana na uwezo wa Mungu, wakati watakuwa wameiva; kwa hivyo natamani kwamba hawa watu wasiangamizwe.

29 Kwa hivyo utaweka hii mipango yao ya siri za viapo na maagano yao kutoka kwa hawa watu, na tu maovu yao na mauaji yao na machukizo yao yatajulishwa kwao; na utawafundisha kuchukia maovu na machukizo na mauaji kama hayo, na utawafundisha pia kwamba hawa watu waliangamizwa kwa sababu ya uovu wao na machukizo na mauaji yao.

30 Kwani tazama, waliwaua manabii wote wa Bwana ambao walikuja miongoni mwao kutangaza kwao kuhusu uovu; na damu ya wale ambao waliwaua ililia kutoka ardhini kwa Bwana Mungu wao kulipiza kisasi kwa wale ambao waliwaua; na hivi hukumu ya Mungu iliwajia hawa wafanyikazi wa giza na makundi maovu ya siri.

31 Ndiyo, na nchi ilaaniwe milele na milele kwa wale wafanyikazi wa gizani na makundi ya siri, hata kwenye maangamizo, isipokuwa watubu kabla ya kuwa waovu kabisa.

32 Na sasa, mwana wangu, kumbuka maneno ambayo nimekuzungumzia; usiamini ile mipango ya siri kwa watu hawa, lakini uwafundishe chuki isiyo na mwisho dhidi ya dhambi na uovu.

33 Wahubirie toba, na imani kwa Bwana Yesu Kristo; wafundishe kujinyenyekeza na kuwa wapole, na wanyenyekevu moyoni; wafundishe kushindana na kila jaribio la ibilisi, na imani yao kwa Bwana Yesu Kristo.

34 Wafundishe wasichoke na kazi nzuri daima, lakini kuwa wapole na wanyenyekevu moyoni; kwani kama hawa watapata mapumziko kwa nafsi zao.

35 Ee, kumbuka, mwana wangu, na ujifunze hekima katika ujana wako; ndiyo, jifunze katika ujana wako kutii amri za Mungu.

36 Ndiyo, na mlilie Mungu kwa usaidizi wako wote; ndiyo, acha vitendo vyako vyote viwe kwa Bwana, na popote uendapo acha iwe kwa Bwana; ndiyo, acha fikira zako zote zielekezwe kwa Bwana; ndiyo, acha mapenzi ya moyo wako yaelekezwe kwa Bwana milele.

37 Shauriana na Bwana kwenye matendo yako yote, na atakuongoza kwa yale mema; ndiyo, unapolala usiku lala katika Bwana, ili akulinde usingizini mwako; na ukiamka asubuhi hebu moyo wako ujazwe na shukrani kwa Mungu; na ukifanya vitu hivi, utainuliwa katika siku ya mwisho.

38 Na sasa, mwana wangu, nina machache ya kuzungumza kuhusu kitu ambacho babu zetu wanaita mpira, au mwelekezi—au baba zetu waliita Liahona, ambayo, inaamanisha dira; na Bwana aliitayarisha.

39 Na tazama, hakungekuwa na mtu ambaye angetengeneza kitu cha mtindo aina hii. Na tazama, ilitayarishwa kuwaonyesha babu zetu njia ambayo wangesafiria katika nyika.

40 Na iliwatumikia kulingana na imani yao kwa Mungu; kwa hivyo, kama walikuwa na imani kuamini kwamba Mungu angesababisha hivyo vijiti vingeonyesha njia ambayo wangefuata, tazama, ilifanyika; kwa hivyo walikuwa na muujiza huu, na pia miujiza mingine mingi iliyofanyika kwa uwezo wa Mungu, siku hadi siku.

41 Walakini, kwa sababu hiyo miujiza ilitendeka kupitia kwa njia rahisi iliwaonyesha kazi ya kushangaza. Walikuwa wavivu na walisahau kutumia imani yao na bidii na baadaye zile kazi za ajabu zilikoma, na hawakuendelea kwenye safari yao;

42 Kwa hivyo, walikaa nyikani, au hawakusafiri kwa njia nyoofu, na waliteswa na njaa na kiu, kwa sababu ya makosa yao.

43 Na sasa, mwana wangu, ningependa uelewe kwamba vitu hivi haviko bila mfano wa maana; kwani kwa jinsi babu zetu walivyokuwa wavivu kufuata hii dira (sasa vitu hivi vilikuwa vya muda) hawakufanikiwa; hata hivyo ndivyo ilivyo na vitu ambavyo ni vya kiroho.

44 Kwani tazama, ni rahisi kama kutii neno la Kristo, ambalo litakuonyesha njia nyoofu kwa raha ya milele, kama vile ilivyokuwa kwa babu zetu kutii hii dira, ambayo ingewaonyesha njia nyoofu kuelekea nchi ya ahadi.

45 Na sasa nasema, hakuna mfano wa kitu hiki? Kwani kwa hakika vile mwongozo huu ulivyowaleta babu zetu kwa kufuata njia yake, kuelekea nchi ya ahadi, hivyo maneno ya Kristo, ikiwa tutafuata mwelekeo wake, yatatuvukisha hili bonde la huzuni hadi mbali kwenye nchi bora ya ahadi.

46 Ee mwana wangu, usiache tuwe wavivu kwa sababu ya urahisi wa njia; kwani hivyo ndivyo ilivyokuwa kwa babu zetu; kwani hivyo ndivyo ilivyotayarishwa kwao, kwamba ikiwa wangeangalia kwake wangeishi; hata hivyo ndivyo ilivyo kwetu sisi. Njia imetayarishwa, na ikiwa tutaangalia tutaishi milele.

47 Na sasa, mwana wangu, uwe na hakika kwamba unalinda vitu hivi vitakatifu, ndiyo, ona kwamba umeelekeza jicho kwa Mungu na uishi. Waendee hawa watu na kutangaza neno, na uwe na busara. Mwana wangu, kwaheri.