Kwa Ajili ya Nguvu kwa Vijana
Mimi ni Mfuasi wa Yesu Kristo
Januari 2024


“Mimi ni Mfuasi wa Yesu Kristo,” Kwa Ajili ya Nguvu kwa Vijana, Jan 2024.

Kauli Mbiu ya Vijana 2024

Mimi Ni Mfuasi wa Yesu Kristo

Unaweza Kumfuata Mwokozi na kueneza neno Lake kwa wengine.

Picha
Nembo ya Kauli Mbiu ya Vijana 2024

Ulishawahi kujiuliza kwa nini, baada ya kuponya watu, Yesu aliwaambia baadhi yao kutomweleza mtu yeyote (ona Marko 7:36)? Sababu mojawapo huenda ikawa ni aina ya wafuasi aliowahitaji Yeye. Ungeweza kufikiri kwamba kama watu wangeongea kuhusu uponywaji wao ingekuwa njia nzuri ya Yesu kuwavutia waliomfuata. Hata hivyo, Yesu hakuhitaji watu kumfuata tu. Alihitaji wafuasi.

Yesu alimwambia Petro na Andrea, “Nifuate” (Mathayo 4:19). Tafsiri ya Joseph Smith ya mstari huo inasomeka, “Mimi ndiye ambaye iliandikwa na manabii; nifuate mimi” (Tafisiri ya Joseph Smith, Mathayo 4:18 [katika Mathayo 4:19, tanbihi a]). Mwaliko haukuwa wa kufuatana Naye kwa muda. Alitaka wawe wafuasi Wake milele.

Hakutaka wakae wakimuangalia akifundisha watu, kuwapenda watu na kutenda miujiza. Aliwataka nao kufanya vivyo hivyo. Alitaka kazi Yake kuwa kazi yao. Kumchagua Kristo ilimaanisha kutumikia kama Yeye alivyotumikia na kufikiri kama Alivyofikiri. Wangejifunza kuishi kama Alivyoishi, na Angewafundisha na kuwapa msaada ambao wangehitaji kuwa kama Yeye.

Picha
Yesu Kristo

Neno la Kigiriki limaanishalo ufuasi ni mathetes. Inamaanisha zaidi ya ufuasi au uanafunzi. Hutafsiriwa mara kwa mara kama mwanafunzi. Katika siku za Kristo, wafuasi walimchagua bwana kutoka yule waliyetaka kujifunza kutoka kwake wakiwa na malengo ya wao nao pia kuja kuwa waalimu. Kristo hakufuata mfumo huu. Aliubadilisha na badala yake Yeye ndiye aliyetafuta wafuasi Wake. Siku hizi, Kristo anatuita twende Kwake. Anatuita tuwe wanafunzi Wake na kutangaza neno lake kati ya watu Wake ili waweze kuwa na maisha ya milele (ona 3 Nefi 5:13).

Binti mmoja kutoka Haiti huko Caribbean alionyesha nia yake ya kuwa mfuasi wa Kristo kwa kumualika rafiki yake ambaye hakuwa muumini wa Kanisa kuja naye kwenye mkutano wa KNV. Mwanzoni baba wa rafiki yake hakutaka kumpa binti yake ruhusa ya kwenda. Viongozi wa Kanisa walielezea uzoefu mzuri uliokuwa unamsubiri pamoja na mshauri mzuri wa vijana ambaye atakuwa mwangalizi wake. Baba alitoa ruhusa kwa binti yake kuhudhuria, na baada ya kuona utofauti ulioletwa katika maisha yake, alimpa pia ruhusa kuhudhuria mikutano ya Kanisa na—miezi sita baadae—alibatizwa.

Mvulana mmoja mdogo kutoka Argentina Amerika ya Kusini alionyesha nia yake ya kuwa mfuasi wa Kristo kwa kumgawia rafiki yake baadhi ya peremende zake walipokuwa kwenye basi kwenda shule. Alipofikia kwenye sehemu yenye ladha ya kahawa, alimwelezea kuwa hajawahi kupata ladha ya viungo kama vile kwani hakuna hata mmoja katika familia yake anayekunywa kahawa. Hii ilipelekea mazungumzo kuhusu Kanisa, ambapo ilipelekea mwaliko wa kuja kwenye mikutano, ambayo hatimaye ilimuongoza rafiki yake kujiunga na Kanisa na kutumikia misheni huko Chile.

Si kila mtu unayeongea naye kuhusu Kanisa au kumwalika kwenye shughuli ya Kanisa atataka kujiunga. Hiyo ni SAWA. Si kila mmoja ambaye Kristo aliongea naye wakati wa huduma Yake duniani alijiunga pia. Bado, tunapochagua kuwa wafuasi wa Yesu Kristo na kutangaza neno Lake, Atatupa ujasiri na msaada wa kiungu. Tutajifunza kuwa zaidi kama Yeye, na hivi ndivyo wafuasi hufanya.