Mkutano Mkuu
Fikiria Selestia!
Mkutano mkuu wa Oktoba 2023


Fikiria Selestia!

Chaguzi zako zitaamua wapi utaishi milele yote, aina ya mwili ambao utafufuka nao na wale ambao utaishi nao milele.

Wapendwa wangu akina kaka na akina dada, nina shukrani za dhati kuzungumza nanyi leo. Katika umri wangu, kila siku mpya huleta vitu vya kupendeza na pia changamoto za kushangaza. Wiki tatu zilizopita, nilijeruhi misuli ya mgongo wangu. Hivyo, nikiwa nimetoa jumbe zaidi ya 100 za mkutano mkuu nikiwa nimesimama, leo nafikiri nitafanya hivyo nikiwa nimekaa. Ninasali kwamba Roho atabeba ujumbe na kupeleka mioyoni mwenu leo.

Hivi karibuni nilisherehekea kumbukizi ya miaka 99 ya kuzaliwa kwangu na hivyo kuanza mwaka wangu wa 100 wa kuishi. Mara nyingi naulizwa siri ya kuishi kwa kipindi chote hicho. Swali bora zaidi lingekuwa “Ni kipi nimejifunza takribani karne moja ya kuishi?”

Muda wa leo hauniruhusu kujibu swali hilo kikamilifu, lakini naweza kushiriki moja ya masomo muhimu zaidi ambayo nimejifunza.

Nimejifunza kwamba mpango wa Baba wa Mbinguni kwetu ni wa kupendeza zaidi, kwamba tunachokifanya kwenye maisha haya kina umuhimu sana, na kwamba Upatanisho wa Mwokozi ndio unaoufanya mpango wa Baba kuwezekana.1

Wakati nikipambana na maumivu makali yaliyosababishwa na jeraha la hivi karibuni, nimehisi hata zaidi shukrani kwa ajili ya Yesu Kristo na zawadi yake ya Upatanisho isiyolinganishwa. Fikiria hilo! Mwokozi aliteseka “maumivu na masumbuko na majaribu ya kila aina”2 ili kwamba Yeye aweze kutufariji, kutuponya, kutuokoa wakati wa uhitaji.3 Yesu Kristo alielezea uzoefu Wake Gethsemane na Kalvari: “mateso ambayo yalimsababisha, hata Mungu, mkuu kuliko yote kutetemeka kwa sababu ya maumivu, na kutokwa damu kwenye kila kinyweleo.”4 Jeraha langu limenisababisha kutafakari tena na tena juu ya “ukuu wa Mtakatifu wa Israeli.”5 Wakati wa uponaji wangu, Bwana amedhihirisha nguvu Zake takatifu katika njia ya amani na ya kweli.

Kwa sababu ya Upatanisho usio na mwisho wa Yesu Kristo, mpango wa Baba yetu wa Mbinguni ni mpango mkamilifu! Uelewa wa mpango wa kupendeza zaidi wa Mungu huondoa dukuduku za maisha na shaka juu ya yajayo. Huturuhusu kila mmoja wetu kuchagua jinsi tutakavyoishi hapa duniani na wapi tutaishi milele. Dhana isiyo na msingi kwamba “tule, tunywe na tusherehekee, kwani kesho tutakufa; na itakuwa sawa kwetu”6 ni moja kati ya uongo wenye upuuzi ulimwenguni.

Hapa kuna habari njema ya mpango wa Mungu: kitu pekee ambacho kitafanya maisha yako ya duniani kuwa bora sana kinaweza kuwa vitu sawa na hivyo ambavyo vitafanya maisha yako yote ya milele kuwa bora sana yanavyoweza kuwa! Leo, ili kuwasaidia kustahili baraka tele ambazo Baba wa Mbinguni anazo kwa ajili yenu, ninawalika kuasili utamaduni wa “kufikiria selestia”! Kufikiria selestia humaanisha kuwa wa kufikiria kiroho. Tunajifunza kutoka kwa Yakobo nabii wa Kitabu cha Mormoni kwamba kufikiri kiroho ni uzima wa milele.”

Maisha ya duniani ni darasa kuu la kujifunza kuchagua vitu vyenye umuhimu mkubwa wa milele. Watu wengi wanaishi kama vile maisha haya ndio pekee kilichopo. Hata hivyo, chaguzi zako za leo zitaamua vitu vitatu: Wapi utaishi milele yote, aina ya mwili ambao utafufuka nao na wale ambao utaishi nao milele. Hivyo, fikiria Selestia.

Kwenye ujumbe wangu wa kwanza kama Rais wa Kanisa, niliwahimiza kuanza na hatma mawazoni. Hii humaanisha kufanya ufalme wa selestia lengo lako la milele na kwa umakini kufikiria wapi kila moja ya uchaguzi wako wakati wa maisha haya ya duniani utakuweka katika ulimwengu ujao.9

Bwana kinagaubaga amefundisha kwamba ni wanaume na wanawake ambao wameunganishwa kama mume na mke kwenye hekalu, na ambao wanashika maagano yao, watakuwa pamoja kwa milele yote. Alisema: “Maagano yote, mikataba, mapatano, ahadi, viapo, nadhiri, utendaji, mahusiano, ushirika, au matarajio, ambayo hayakufanyika na kuingizwa ndani na kufungwa na yule Roho Mtakatifu wa ahadi … huwa na ukomo watu wanapokufa.”10

Hivyo basi, kama bila busara tutachagua kuishi sheria za telestia hivi sasa, tunachagua kufufuka na miili ya telestia . Tunachagua kutoishi na familia zetu milele.

Hivyo basi, wapendwa wangu akina kaka na dada, ni kwa jinsi ipi na wapi na nani ambaye unataka kuishi naye milele? Uchaguzi ni wako.11

Wakati mnapofanya chaguzi, ninawaalika kuwa na mtazamo wa kina—mtazamo wa umilele. Mwekeni Yesu Kristo kwanza, kwa sababu maisha yenu ya milele yanategemea imani yenu Kwake na Upatanisho Wake.12 Maisha yenu pia yanategemea juu ya utiifu wenu wa sheria Zake. Utiifu huandaa njia kwa ajili ya maisha ya furaha kwenu leo hii na zawadi kuu, maisha ya milele kesho.

Wakati unapokumbana na mkanganyiko, fikiria selestia! Wakati unapojaribiwa na jaribu, fikiria selestia! Wakati maisha au wapendwa wako wanapokuangusha, fikiria selestia! Wakati mtu fulani anapofariki kabla ya kuzaliwa, fikiria selestia. Wakati mtu fulani anaposumbuka na ugonjwa wa kukatisha tamaa, fikiria selestia. Wakati shinikizo za maisha zinapokusonga, fikiria selestia! Wakati unapopata nafuu kutoka kwenye ajali au jeraha, kama nilivyo sasa, fikiria selestia!

Wakati unapofokasi kwenye kufikiria selestia, tazamia kukutana na upinzani.13 Miongo kadhaa iliyopita, mtaalamu mwenzangu alinikosoa kwa “upendaji wangu sana wa hekalu” na wasimamizi wangu zaidi ya mmoja walinipa onyo kwa sababu ya imani yangu. Ninashawishika, hata hivyo, kwamba kufikiria selestia kuliiboresha taaluma yangu.

Unapofikiria selestia, moyo wako taratibu utabadilika. Utataka kusali zaidi na kwa dhati. Tafadhali msiache sala zenu kuonekana kama orodha ya manunuzi. Mtazamo wa Bwana unazidi hekima yenu ya kidunia. Mwitikio Wake wa sala zenu unaweza kuwashangaza na utawasaidia kufikiria selestia.

Fikiria mwitikio wa Bwana wa sala ya Joseph Smith wakati aliposihi kwa ajili ya unafuu akiwa jela ya Liberty. Bwana alimfundisha Nabii kwamba kutendwa kwake kusiko kwa kibinadamu kungempa uzoefu na kungekuwa kwa faida yake.14 “Kama utastahimili vyema,” Bwana aliahidi, “Mungu atakuinua juu.”15 Bwana alikuwa akimfundisha Joseph kufikiria selestia na kuvuta taswira ya thawabu ya milele kuliko kufokasi kwenye magumu ya kutisha ya siku. Sala zetu zinaweza kuwa—na zinapaswa kuwa—mjadala endelevu na Baba yetu wa Mbinguni.

Unapofikiria selestia, utajikuta ukiepuka chochote ambacho kinakunyang’anya haki yako ya kujiamulia. Uraibu wowote ule—iwe wa michezo ya video, kamari, madeni, mihadarati, ulevi, hasira, ponografia, ngono au hata chakula—humgadhabisha Mungu. Kwa nini? Kwa sababu matamanio yako huwa mungu wako. Unayategemea yenyewe kuliko Yeye kwa ajili ya msaada. Kama unahangaika na uraibu, tafuta msaada wa kiroho na wa kitaalam unaohitaji. Tafadhali msiache matamanio yawanyang’anye uhuru wa kufuata mpango wa kupendeza zaidi wa Mungu.

Kufikiria selestia pia kutawasaidia kutii amri ya usafi wa kimwili. Kuvunja amri hii takatifu kutafanya haraka maisha yako kuwa magumu kuliko vitu vichache ambavyo vinaweza kufanya hilo. Kwa wale ambao wamefanya maagano na Mungu, zinaa ni moja ya njia za haraka za kupoteza ushuhuda wako.

Mengi ya majaribu yenye nguvu ya mwovu hujumuisha uvunjaji wa usafi wa kimaadili. Nguvu ya kuumba maisha ni fursa moja ya uungu ambayo Baba wa Mbinguni huwaruhusu watoto Wake duniani kuitumia. Hivyo, Mungu aliweka mwongozo wa wazi kwa ajili ya matumizi ya nguvu hii takatifu. Mahusiano ya kimwili ni pekee kwa mwanaume na mwanamke ambao wameoana.

Sehemu kubwa ya ulimwengu haiamini hili, lakini mtazamo wa umma si mamlaka yatoayo ukweli. Bwana ametamka kwamba mtu yeyote mchafu kimaadili hatafikia ufalme wa selestia. Basi, wakati mnapofanya chaguzi kuhusu usafi wa kimaadili, tafadhali fikirieni selestia. Na kama umekuwa mchafu kimaadili, ninakusihi utubu. Njoo kwa Kristo na pokea ahadi Yake ya msamaha kamili wakati unapotubu kwa dhati dhambi zako.16

Unapofikiria selestia, utayatazama majaribu na upinzani katika njia mpya. Wakati mtu umpendaye anapoushambulia ukweli, fikiria selestia, na usitie ushuhuda wako mashaka. Mtume paulo alitoa unabii kwamba “nyakati za mwisho wengi watajitenga na imani, wakisikiliza roho zidanganyazo, na mafundisho ya mashetani.”17

Hakuna mwisho wa uongo wa mwovu. Tafadhali jiandaeni. Kamwe usichukue ushauri toka kwa wale wasioamini. Tafuta mwongozo kutoka sauti unazoweza kuziamini—kutoka kwa manabii, waonaji na wafunuzi na kutoka kwenye mnong’ono wa Roho Mtakatifu, ambaye “atawaonyesha ninyi vitu vyote ambavyo mnastahili kutenda.”18 Tafadhali fanya kazi ya kiroho ya kuongeza uwezo wako wa kupokea ufunuo binafsi.19

Wakati unapofikiria selestia, imani yako itaongezeka. Wakati nilipokuwa mwanafunzi kijana, pato langu lilikuwa dola 15 kwa mwezi. Usiku mmoja, mke wangu Dantzel aliniuliza kama nilikuwa nikilipa zaka toka kipato hicho kidogo. Nilikuwa sifanyi hivyo. Mara moja nilitubu na kuanza kulipa ziada ya dola 1.50 kwenye zaka ya mwezi.

Je, kanisa lilikuwa na tofauti yoyote kwa sababu tuliongeza zaka yetu? Bila shaka hapana. Hata hivyo, kuwa mlipa zaka kamili kulinibadilisha mimi. Hapo ndipo nilijifunza kwamba kulipa zaka ni kuhusu imani na si fedha. Kama mlipa zaka kamili, madirisha ya mbinguni yalianza kufunguka kwa ajili yangu. Ninahusisha matokeo ya fursa za kitaaluma zilizofuata na uaminifu wetu wa ulipaji zaka.20

Kulipa zaka inahitaji imani, na pia hujenga imani katika Mungu na Mwanawe Mpendwa.

Kuchagua kuishi maisha masafi katika ulimwengu unaochochea ngono, kwa siasa hujenga imani.

Kutumia muda zaidi hekaluni hujenga imani. Na huduma na kuabudu kwenu hekaluni vitawasaidia kufikia selestia. Hekaluni ni sehemu ya ufunuo. Humo mnaonyeshwa jinsi ya kukua kuelekea maisha ya selestia. Humo mnasogezwa karibu na Mwokozi na kupewa ufikiaji mkubwa wa nguvu Zake. Humo mnaongozwa katika kutatua matatizo katika maisha yenu, hata matatizo ya kukanganya.

Ibada na maagano ya hekaluni ni ya umuhimu wa milele. Tunaendelea kujenga zaidi mahekalu ili kufanya uwezekano wa ibada hizi tukufu kuwa za uhalisia kwenye kila maisha yenu. Tuna shukrani kutangaza mipango yetu ya kujenga hekalu katika kila sehemu 20 zifuatazo:

  • Savai’i, Samoa

  • Cancún, Mexico

  • Piura, Peru

  • Huancayo, Peru

  • Viña del Mar, Chile

  • Goiânia, Brazil

  • João Pessoa, Brazil

  • Calabar, Nigeria

  • Cape Coast, Ghana

  • Luanda, Angola

  • Mbuji-Mayi, Democratic Republic of the Congo

  • Laoag, Philippines

  • Osaka, Japan

  • Kahului, Maui, Hawaii

  • Fairbanks, Alaska

  • Vancouver, Washington

  • Colorado Springs, Colorado

  • Tulsa, Oklahoma

  • Roanoke, Virginia

  • Ulaanbaatar, Mongolia

Bwana anatuongoza kujenga mahekalu haya ili kutusaidia kufikiria selestia. Mungu yu hai. Yesu ndiye Kristo. Kanisa Lake limerejeshwa ili kuwabariki watoto wote wa Mungu. Ninashuhudia hivyo katika jina takatifu la Yesu Kristo, amina.

Muhtasari

  1. Ona Yohana 6:38.

  2. Alma 7:11.

  3. Ona Alma 7:12.

  4. Mafundisho na Maagano 19:18.

  5. 2 Nefi 9:40.

  6. 2 Nefi 28:7.

  7. Inaweza kuthibitika kuwa rahisi kutubu na kuendelea kiroho hapa duniani, wakati roho yetu imeunganika na mwili wetu, kuliko katika ulimwengu ujao kati ya kipindi cha kuwa tumekufa na kufufuka. Kama vile Amuleki alivyowafunza Wazoramu walioasi, “Maisha haya ndiyo wakati … kujitayarisha kukutana na Mungu” (ona Alma 34:32–35).

  8. 2 Nephi 9:39.

  9. Ona Mosia 4:30, pale Mfalme Benjamini alivyowaasa watu wake: Msipojichunga wenyewe, na mawazo yenu, na maneno yenu, na matendo yenu, na kufuata sheria za Mungu, na kuendelea kwa imani … , lazima mtaangamia.”

  10. Mafundisho na Maagano 132:7; msisitizo umeongezwa.

  11. Bila shaka, haki yako ya kujiamulia haiwezi kuondoa ya mtu mwingine na matokeo yatokanayo na hilo. Nilitaka sana kuunganishwa kwa wazazi wangu. Hata hivyo, Ilinibidi kusubiri mpaka wao wachague kupata endaumenti wakati walipokuwa na zaidi ya umri wa miaka 80. Kisha waliunganishwa kama mume na mke, na sisi watoto tukaunganishwa kwao.

  12. Maandiko yamerudiarudia kushuhudia kwamba zawadi ya uzima wa milele ni kupitia masharti, rehema, na neema ya Mwokozi Yesu Kristo pekee (ona, kwa mfano, Moroni 7:41; ona pia 2 Nefi 2:6–8, 27).

  13. Ona 2 Nefi 2:11.

  14. Ona Mafundisho na Maagano 122:7.

  15. Mafundisho na Maagano 121:8.

  16. Ona Isaya 1:16–18; Mafundisho na Maagano 58:42–43.

  17. 1 Timotheo 4:1. Mstari ufuatao unaendelea, “Wasemao uongo, wakichomwa moto dhamiri zao wenyewe;” (mstari wa 2). Paulo pia alitangaza kwamba wale wote “[wanaoishi] maisha ya utauwa katika Kristo Yesu wataudhiwa.” (2 Timotheo 3:12).

  18. 2 Nefi 32:5; msisitizo umeongezwa. Kama tutaomba, tunaweza “kupokea ufunuo juu ya ufunuo, maarifa juu ya maarifa” (Mafundisho na Maagano 42:61).

  19. Ona Russell M. Nelson, “Ufunuo kwa ajili ya Kanisa, Ufunuo kwa ajili Maisha Yetu,” Liahona, Mei 2018, 96.

  20. Hii haimaanishi dhana ya uhusiano wa chanzo na matokeo. Baadhi ambao hawalipi zaka wanapata fursa za kitaaluma, wakati wale wanaolipa zaka hawapati. Ahadi ni kwamba madirisha ya mbinguni yatafunguliwa kwa mlipa zaka. Asili ya baraka itatofautiana.