2010
Kuongeza Imani na Wema wa Kibinafsi
Agosti 2010


Ujumbe wa Mwalimu Mtembelezi, Agosti 2010

Kuongeza Imani na Wema wa Kibinafsi

Soma kifaa hiki, na kama inavyostahili kizungumzie pamoja na kina dada unaowatembelea. Tumia maswali ili kukusaidia kuwaimarisha dada zako na kuufanya Muungano wa Usaidizi wa Kina Mama kuwa sehemu hai ya maisha yako mwenyewe.

Picha
Relief Society seal

Imani • Familia • Hudumaw

Kutoka kwa Maandiko

Isaya 2:2–3; M&M 109:22–23; 110:8–10

Jukumu Letu la Kuwa Wastahiki kwa Ibada za Hekalu

“Maagano tunayofanya na ibada zinazoambatana tunazopokea katika hekalu huwa vibali vya kukubaliwa katika uwepo wa Mungu. Maagano haya yanatuinua sisi zaidi ya mipaka ya uwezo wetu na mtazamo wetu wenyewe. Tunapofanya maagano tunaonyesha kujizatiti kwetu kwa kujenga ufalme. Tunakuwa watu wa agano kwa vile tunawekwa chini ya agano kwa Mungu. Baraka zote zinazoahidiwa ni zetu kupitia uaminifu wetu kwa maagano haya. …

“Wanawake wa Kanisa wanaweza kufanya nini ili kupata baraka za hekalu?

“Kupitia manabii Wake, Bwana anawaalika wale ambao bado hawajapokea baraka za hekalu kufanya chochote kilichokuwa kinahitajika kuhitimu kuzipokea. Anawaalika wale ambao tayari wameshapokea hizi baraka kurudi tena mara kwa mara inavyowezekana kufurahia tena uzoefu huu, kuongezea maono yao na ufahamu juu ya mpango Wake wa milele.

“Acheni tuwe wastahiki ili kuwa na kibali cha sasa cha hekalu. Acheni tuende hekaluni kufunganishwa na familia zetu milele Acheni turudi tena hekaluni mara kwa mara jinsi hali inavyotuwezesha Acheni tuwapatie jamii yetu iliokufa nafasi ya kupokea ibada za kuinuliwa. Acheni tuweze kufurahia nguvu za kiroho na ufunuo tunaopokea tunavyohudhuria hekalu kila mara. Acheni tuwe waaminifu na kufanya na kuweka maagano ya hekalu na kupokea baraka kamili za Upatanisho”1

Silvia H. Allred, mshauri wa kwanza katika urais mkuu wa Muungano wa Usaidizi wa akina Mama.

Kutoka kwa Historia Yetu

Rais Gordon B. Hinckley (1910–2008) alifunza kwamba Muungano wa Usaidizi wa Kina Mama ulikua kutokana na hamu ya kina dada ya kuabudu hekaluni:

“Wakati wa ujenzi wa Hekalu la Kirtland wanawake waliulizwa kusaga kauli zao kichina vipande vidogo vichanganywe na simiti na kutumika kwenye kuta za hekalu, ambazo zingeshika mwanga wa jua na mwezi na kufanyiza huu mwanga kurembesha sura la jengo hili.

“Katika siku hizo, wakati kulikuwa na hela kidogo sana lakini wingi wa imani, wafanyakazi walitoa nguvu zao na mali yao ili kujenga nyumba ya Bwana. Wanawake waliwaletea chakula, kilicho bora vile wangeweza kutayarisha. Edward W. Tullidge aliandika kwamba wakati wanawake walikuwa wakishona pazia za hekalu, Joesph Smith, akiwatazama, alisema, ‘Vyema, kina dada, mpo tayari wakati wowote. Kina dada uwa wa kwanza kila mara na ni muhimu katika kazi zote njema. Mariamu alikuwa wa kwanza kwenye ufufuko; kina dada sasa ndio wa kwanza kufanya kazi ndani ya hekalu.’ …

“Tena katika Nauvoo, wakati hekalu lilipokuwa linaendelea kujengwa, wanawake wachache waliungana pamoja kuwashonea wafanyakazi mashati. Ni kutokana na hali hizi kwamba ishirini ya wao walikusanyika Alhamisi ya, tarehe 17 Machi 1842, katika chumba cha juu cha duka la Nabii”2 Basi Muungano wa Usaidizi wa Kina Mama Ukaanza.

Tunaweza Kufanya Nini?

  1. Ni usaidizi gani ninaoweza kutoa kuwasaidia dada zangu kujitayarisha kwa na kushiriki hekaluni?

  2. Nawezaje kuonyesha vipi mfano wa urithi wa kina dada wa hapo zamani wa kujitolea ili kupokea baraka za hekalu?

  3. Nawezaje kustahili baraka za hekalu?

Muhtasari

  1. Silvia H. Allred, “Holy Temples, Sacred Covenants,” Liahona, Nov. 2008, 113, 114.

  2. Gordon B. Hinckley, “Ambitious to Do Good,” Ensign, Mar. 1992, 2.