2011
Wewe ni wa maana Kwake
Novemba 2011


Wewe ni wa maana Kwake

Bwana hutumia mizani tofauti sana na ya ulimwengu kupima thamani ya nafsi.

Musa mmoja wa manabii wakuu ambao dunia imewahi kufahamu, alilewa na bintiye Farao na akatumia miaka 40 ya kwanza ya maisha yake katika kumbi za enzi za Misri. Alielewa kwa njia ya kibinafsi utukufu na ufahari wa ufalme huo wa kale.

Miaka baadaye, juu ya mlima wa mbali, mbali na fahari na uzuri wa Misri yenye nguvu, Musa alisimama katika uwepo wa Mungu na kunena naye uso kwa uso kama vile mtu hunena na rafiki yake.1 Katika mkondo wa matembeleo haya, Mungu alimwonyesha Musa kazi ya mikono yake, akimpa tazamo la mara moja la kazi na utukufu wake. Wakati maono yalipoisha, Musa alianguka chini mchangani kwa muda wa masaa mengi. Wakati nguvu zake ziliporejea, aligundua jambo fulani, ambalo kwa miaka yake yote katika kitala cha Farao, lilikuwa kamwe halijamtokea hapo mbeleni.

“Ninajua,” alisema, “kwamba mwanadamu si kitu”2

Sisi tu Wapungufu kuliko Tunavyodhani

Tunanvyojifunza zaidi kuhusu Ulimwengu, ndivyo zaidi tunavyoelewa, ingawa kwa sehemu ndogo—kile ambacho Musa alikijua. Ulimwengu ni mkubwa sana, usivyofahamika, na mtukufu kwamba haieleweki katika akili ya binadamu. “Na dunia zisizo na idadi nimeziumba,” Mungu akamwambia Musa.3 Maajabu ya anga ya usiku ni ushuhuda mzuri wa ukweli huu.

Kuna vitu vichache vinavyonijaza na staha isiyo kifani kama kusafiri kwa ndege kwenye weusi wa usiku kuvuka bahari na bara na kuona nje ya dirisha la chumba changu cha rubani kutazama utukufu usiokoma wa mamilioni ya nyota.

Wanasayansi wa sayari wamejaribu kuhesabu idadi ya nyota katika Ulimwengu. Kikundi kimoja cha wanasayansi wamekadiria kuwa idadi ya nyota katika upeo wa darubini zetu kuwa mara 10 zaidi ya chembe zote za mchanga zinazopatikana katika pwani na majangwa yote ulimwenguni.4

Hitimisho hili lina mfanano wa kuvutia na matamko ya nabii wa kale Henoko: “Na kama ingeliwezekana mwanadamu aweze kuhesabu vipande vya dunia, ndiyo, mamilioni ya dunia kama hii, isingelikuwa mwanzo wa idadi ya viumbe vyako.”5

Kulingana na upana wa viumbe vya Mungu, si ajabu mfalme mkuu Binyamini aliwashauri watu wake “na kila wakati mshikilie ukumbusho, wa ukuu wa Mungu, na unyonge wenu.”6

Sisi tu Wakuu kuliko Tunavyodhani

Lakini hata ingawa binadamu ni mnyonge, ninajawa na staha na kustajabu kufikiri kuwa “thamani ya nafsi ni kubwa mbele za Mungu.”7

Na huku tunapoweza kutazama upana mkubwa wa Ulimwengu na kusema, “Mtu ni nini kulingana na utukufu wa viumbe?” Mungu mwenyewe alisema sisi ndio sababu yake kuumba Ulimwengu! Kazi Yake na utukufu—dhamira ya ulimwengu huu tukufu—ni kuokoa na kutukuza mwanadamu.8 Kwa maneno mengine, upana mkubwa wa milele, utukufu na siri za anga isiyo na mipaka na nyakati zote zimejengwa kwa faida ya watu wa kawaida kama mimi na wewe. Baba yetu wa Mbinguni aliumba Ulimwengu ili tuweze kufikia uwezo wetu usiodhihirika kama wana na binti zake.

Huu ni ukweli kinza kwa mtu: akilinganishwa na Mungu, mtu si kitu, na hali sisi ni kila kitu kwa Mungu. Katika muktadha wa uumbaji usio na mipaka tunaweza kuonekana kuwa si kitu, tuna spaki ya moto wa milele ukiwaka ndani ya vifua vyetu. Tuna ahadi isiyoeleweka ya kuinuliwa—dunia bila mwisho—katika mfiko wetu. Na ni ari kubwa ya Mungu kutusaidia kuifikia.

Upumbavu wa Kiburi

Mdanganyifu mkuu anajua kuwa mojawapo wa vifaa vyake vyenye nguvu katika kuwapotosha watoto wa Mungu ni kuvutia upeo wa kweli kinza ya mtu. Kwa wengine anavutia mwelekeo wao wa kiburi, akiwafurisha na kuwatia moyo kuamini katika utungaji wao wa taswira ya umuhimu wao wa kibinafsi na kutoshindika kwao. Anawaambia wamepita yale ya kawaida na hiyo kwa sababu ya uwezo, haki ya kuzaliwa, au hadhi, wametengwa kutokana na kipimo cha kawaida cha wote walio karibu nao. Anawaongoza kuamua kuwa kwa sababu hiyo hawako chini ya sheria yoyote na wasisumbuliwe na shida za mtu mwingine yeyote.

Abraham Lincoln anasemekana kuwa alipenda shairi ambalo lililosema:

Kwa nini roho ya mtu huwa na kiburi?

Kama kimondo kinachoruka, kama wingu linalopaa kwa upesi,

Mwasho wa radi, kuvunjika kwa mawimbi,

Mtu huaga kutoka kwa uhai hadi mapumziko yake katika kaburi.9

Wanafunzi wa Yesu Kristo wanaelewa kuwa kulinganishwa na milele, kuwepo kwetu katika tufe hili la muda ni “muda mdogo sana” katika uwanda na wakati.10 Wanafahamu kuwa thamani ya kweli ya mtu haihusiani na yale ambayo dunia inathamini. Wanajua kuwa ungeweza kurundika fedha zilizokusanywa za dunia nzima na hazingeweza kununua mkate katika uchumi wa mbinguni.

Wale watakao “kurithi ufalme wa Mungu”11 ni kwa wale wanaokuwa “kama mtoto, mtiifu, mpole, mnyenyekevu, mvumilivu, mwenye upendo tele.”12 “Kila ajikwezaye atadhililishwa; naye ajidhililishaye atakwezwa.”13 Wanafunzi kama hawa pia uelewa kuwa “mnapowatumikia wanadamu wenzenu mnamtumikia tu Mungu wenu.”14

Sisi Hatujasahaulika

Njia nyingine ambayo Shetani anatumia kudanganya ni kupitia kwa kuvunjika moyo. Anajaribu kuelekeza kuona kwetu katika uhafifu wetu hadi tunapoanza kushuku kuwa tuna thamani yoyote. Anatuambia kuwa sisi ni wadogo kwa yeyote kututambua, kwamba tumesahaulika—hasa na Mungu.

Hebu nishiriki nanyi uzoefu wa kibinafsi unaoweza kuwa wa usaidizi kwa wale wanaohisi kuwa hafifu, wamesahaulika au wapweke.

Miaka mingi iliyopita, nilihudhuria mafunzo ya urubani katika Jeshi la Angani la Marekani. Nilikuwa mbali na nyumbani, kijana askari wa Ujerumani Magharibi, aliyezaliwa Czechoslovakia, ambaye alikuwa amekulia Ujerumani Mashariki na kuzungumza Kiingereza kwa ugumu mno. Nakumbuka kwa njia dhahiri safari yangu kwenda katika kituo cha mafunzo cha jeshi huko Texas. Nilikuwa katika ndege, nikiwa nimeketi karibu na abiria aliyekuwa na athari nzito ya lafudhi ya Kusini. Ningeelea kwa shida sana neno alilosema. Nilishangaa kama nilikuwa nimefundishwa lugha kimakosa wakati huu wote. Nilihofu kwa fikira kuwa ningeshindania nafasi za juu katika mafunzo ya urubani dhidi ya wanafunzi ambao walikuwa wazungumzaji wa asili wa Kiingereza.

Nilipowasili katika kituo cha wanahewa katika mji mdogo wa Big Spring, Texas, nilitafuta na kupata tawi la Watakatifu wa Siku za Mwisho, lililokuwa na washiriki wachache wa ajabu waliokuwa wakikutana katika vyumba vilivyokodiwa katika kituo cha wanahewa. Washiriki walikuwa katika mpango wa kujenga jumba dogo la mikutano ambalo lingetumika kama mahali pa kudumu pa Kanisa. Siku hizo, washiriki walifanya ujenzi wa majengo mapya.

Siku baada ya siku nilihudhuria mafunzo yangu ya urubani nilisoma kwa bidii kadiri nilivyoweza na kutumia wakati wangu wa akiba nikifanya kazi katika jumba jipya la mikutano. Pale nilijifunza kwamba mbili-mara-nne si mtindo wa densi bali ni kipande cha mbao. Nilijifunza pia maarifa ya kuishi ya kukwepa gumba wakati wa kipigalia msumari.

Nilitumia wakati mwingi kufanya kazi katika jumba la mikutano hadi Rais wa tawi—ambaye pia alikuwa mmoja wa wakufunzi wetu wa urubani—akadhihirisha wasiwasi kuwa huenda ingekuwa bora kuwa ningetumia wakati zaidi nikisoma.

Marafiki zangu na wanafunzi wenzangu pia walijihusisha na shughuli za wakati wa akiba ingawa nafikiri ni bora kusema kuwa baadhi ya shughuli hizo hazingefungamana na kijitabu cha hivi leo cha For the Strength of Youth. Kwa upande wangu, nilifurahia kuwa sehemu ya tawi la magharibi Texas, kutumia maarifa yangu mapya ya useremala na kuboresha Kiingereza nilipokuwa nikitimiza miito yangu kufundisha katika jamii ya wazee na katika shule ya Jumapili.

Wakati huo, Big Spring, licha ya jina lake, palikuwa pahali padogo, pasipoonekana wala kujulikana. Na Mara nyingi nilihisi hivyo kuhusu mimi mwenyewe—nisiyeonekana asiyejulikana na mpweke kabisa Hata hivyo, sikushangaa kama Bwana alikuwa amenisahau au kama angeweza kunipata huko. Nilijuwa haikuwa jambo kwa Baba wa Mbinguni popote nilipokuwa, mahali niliorodheka na wengine katika mafunzo yangu urubani au ni nini mwito wangu Kanisani. Kilichokuwa muhimu kwake ni kuwa nilikuwa nikifanya bidii jinsi nilivyoweza, na kwamba nilikuwa niko radhi kuwasaidia wale waliokuwa karibu nami. Nilijua kuwa ningetenda vyema ninavyoweza, yote yangekuwa mema.

Na yote yalikuwa mema.15

Wa Kwanza Watakuwa wa Mwisho

Kwa Bwana haijalishi hata kidogo ikiwa tutatumia siku zetu tukifanya kazi kwenye kumbi za mawe au katika vibanda vya wanyama. Anafahamu tulipo, haijalishi jinsi ya hali zetu za unyonge. Atatumia—kwa njia yake na kwa makusudi yake matakatifu—wale ambao mioyo yao inaelekea kwake.

Mungu anafahamu kuwa baadhi ya nafsi kuu waliowahi kuishi ni wale ambao hawatawahi kuonekana katika kumbukumbu za historia. Ni wale waliobarikiwa,wanyenyekevu wanaofuata mfano wa Mwokozi na kutumia siku za maisha yao wakitenda mema.16

Wachumba wa mfano kama huu, wazazi wa rafiki yangu, walinionyesha kwa mfano kanuni hii Mume alifanya kazi katika kiwanda cha chuma huko Utah. Wakati wa chakula cha mchana angetoa maandiko yake au jarida la Kanisa na kusoma. Wafanyi kazi wengine walipoona haya walimkejeli na kupinga imani yake. Walipofanya hivyo, aliwazungumzia kwa hisani na kwa ujasiri. Hakukubali ukosefu wao wa heshima kumkasirisha wala kumvuruga.

Miaka baadaye, mmoja wa wale waliomkejeli aliyesikika zaidi akawa mgonjwa sana. Kabla ya kufa aliuliza kuwa huyu mtu mnyenyekevu azungumze katika mazishi yake—ambavyo alifanya.

Huyu mshiriki mwaminifu wa Kanisa kamwe hakuwa na mengi kwa staha ya kijamii au mali, lakini ushawishi wake ulienea ndani kwa wale wote waliomjua. Alikufa katika ajali ya kiwandani wakati alipokuwa amesimama kumsaidia mfanyakazi mwingine aliyekuwa amekwama kwenye theluji.

Katika muda wa mwaka mmoja, mjane wake alifanyiwa upasuaji wa ubongo ambao umemfanya kukosa kuweza kutembea Lakini watu wanapenda kuja kukaa naye kwa sababu anasikiliza. Anakumbuka. Anajali. Kwa kuwa hawezi kuandika, anakariri nambari za simu za watoto wake na za wajukuu wake Kwa upendo anakumbuka siku za kuzaliwa kwao na siku za maadhimisho.

Wale wanaomtembelea wanatoka huko wakihisi vyema zaidi juu ya maisha na kujihusu wenyewe. Wanahisi upendo wake. Wanajua kuwa anajali. Kamwe halalamiki lakini anatumia siku zake akibariki maisha ya wengine. Mmoja wa marafiki zake alisema mwanamke huyu alikuwa mmoja wa watu wachache aliowafahamu ambao kwa kweli walionyesha kwa mfano wa upendo na maisha ya Yesu Kristo.

Wachumba hawa wangekuwa wa kwanza kusema hawakuwa na umuhimu sana hapa duniani. Lakini Bwana hutumia mizani tofauti sana na ile ya dunia ili kupima thamani ya nafsi. Anafahamu wachumba hawa waaminifu; Yeye anawapenda. Matendo yao ni ushuhuda hai wa imani yao yenye nguvu katika Yeye.

Wewe ni wa Maana Kwake

Akina ndugu na dada zangu wapendwa, inaweza kuwa kweli kwamba mtu si kitu kulingana na ukubwa wa Ulimwengu. Wakati mwingine, tunaweza kuhisi kutokuwa na umuhimu, kutoonekana, wapweke au kusahaulika. Lakini daima kumbuka—wewe ni wa maana Kwake! Ikiwa utawahi kushuku kuwa wewe ni wa maana kwake, fikiria kanuni hizi nne za kiungu:

Kwanza, Mungu anawapenda wanyenyekevu na wapole kwani wao ndio “walio wakuu katika ufalme wa Mbinguni.”17

Pili, Bwana amekabidhi “utimilifu wa injili [Yake] uweze kutangazwa na watu walio dhaifu na wa kawaida hata mwisho wa dunia.”18 Amechagua “mambo dhaifu ya dunia [yata] kuja kuyavunja yale yaliyo makubwa na yenye nguvu.”19 kuyatia aibu “mambo yaliyo makuu.”20

Tatu, haijalishi unakoishi, haijalishi unyonge wako, uduni wa kazi yako, uhaba wa vipawa vyako, sura yako kuwa ya kawaida, au jinsi mwito wako Kanisani ulivyooneka kuwa mdogo, wewe si wa kutoonekana kwa Baba wa Mbinguni. Anakupenda. Anafahamu moyo wako mnyenyekevu na matendo yako ya upendo na hisani. Pamoja yanaunda ushuhuda wa kudumu wa uaminifu wako na imani.

Nne, na la mwisho, tafadhali elewa kuwa kile unachoona na kupata uzoefu sasa si yote ambayo utakuwa milele. Hautahisi upweke, huzuni, uchungu na kuvunjika moyo milele. Tuna ahadi ya uaminifu ya Mungu kuwa yeye hatasahau wala kuwaacha wale wanaoelekeza mioyo yao Kwake.21 Kuwa na matumaini na imani katika ahadi hiyo. Jifunze kumpenda Baba yako wa Mbinguni na kuwa mwanafunzi wake kwa maneno na matendo.

Muwe na hakika kuwa ukivumilia, kumwamini na kubaki mwaminifu katika kuweka amri zake, siku moja utapata uzoefu wako binafsi wa ahadi zilizofunuliwa kwa Mtume Paulo: “Jicho halikuyaona wala sikio halikuyasikia wala hayakuingia katika moyo wa mwanadamu mambo ambayo Mungu aliwaandalia wampendao.”22

Akina ndugu na dada, Kiumbe aliye na nguvu zaidi katika Ulimwengu ni Baba wa roho yako. Anakufahamu. Anakupenda kwa upendo mkamilifu.

Mungu anakuona, si kama mtu wa maisha ya muda katika sayari ndogo anayeishi kwa muda mfupi—Yeye anakuona kama mtoto Wake. Anakuona kama mtu unayeweza kuwa kile ulichopangiwa kuwa. Anataka ujue kuwa wewe ni wa maana Kwake.

Acha daima tuamini, tukubali na tulinganishe maisha yetu ili tuelewe thamani yetu ya milele na uwezo wetu. Na tuwe wa kustahili baraka za thamani ambazo Baba yetu wa Mbinguni ametuwekea ni ombi langu katika jina la Mwanawe, hata Yesu Kristo. Amina.