2012
Mafundisho ya Wakati Wetu
Mei 2012


Mafundisho ya Wakati Wetu

Mafundisho ya Jumapili ya nne kwa Ukuhani wa Melkizedeki na Muungano wa Usaidizi wa Kina Mama yatatengwa kwa “Mafundisho ya Wakati Wetu” Kila somo linaweza kutayarishwa kutoka kwa hotuba moja au zaidi za mkutano mkuu wa hivi majuzi (ona chati hapa). Marais wa vigingi na wilaya wanaweza kuchagua hotuba zitakazotumiwa, au wanaweza kuwapa majukumu maaskofu na marais wa matawi. Viongozi wanafaa kusisitiza umuhimu wa ndugu za Ukuhani wa Melkizediki na akina dada wa Muungano wa Usaidizi wa Kina Mama kusoma hotuba sawa katika Jumapili hizo.

Wale wanaohudhuria mafundisho ya Jumapili ya nne wanahimizwa kusoma na kuleta madarasani toleo la gazeti la mkutano mkuu la hivi karibuni.

Mapendekezo ya Kutayarisha Somo kutoka kwa Hotuba

Omba kwamba Roho Mtakatifu awe nawe unaposoma na kufundisha hotuba hizi. Unaweza kushawishika kutayarisha masomo kwa kutumia vifaa vingine, lakini hotuba za mkutano mkuu ni mtaala ulioidhinishwa. Jukumu lako ni kuwasaidia wengine kujifunza na kuishi kulingana na injili kama ilivyofundhishwa katika mkutano mkuu wa Kanisa wa hivi majuzi.

Rejelea upya hotuba hizi, ukitafuta kanuni na mafundisho yanayolingana na mahitaji ya washiriki wa darasa. Pia, tafuta hadithi, marejeleo ya maandiko, na matamko kutoka kwa hotuba ambazo zitakazokusaidia kufundisha kweli hizi.

Tayarisha umbo la jinsi ya kufundisha kanuni na mafundisho. Fikiria kujumuisha maswali ambayo yatawasaidia washiriki wa darasa:

  • Angalia kanuni na mafundisho katika hotuba.

  • Tafakari juu ya maana yake.

  • Shiriki mawazo, tajiriba, uzoefu na shuhuda.

  • Tumia kanuni na mafundisho haya katika maisha yao.

Miezi Masomo Yatapofunzwa

Vifaa vya Mafundisho ya Jumapili ya Nne

Aprili 2012–Oktoba 2012

Hotuba zilizotolewa katika mkutano mkuu wa Aprili 2012*

Oktoba 2012–Aprili 2013

Hotuba zilizotolewa katika mkutano mkuu wa Oktoba 2012*

  • Kwa Masomo ya Jumapili ya Nne ya Aprili na Oktoba, hotuba zinaweza kuchaguliwa kutoka kwa mkutano mkuu wa awali au kutoka kwa mikutano ya majuzi sana. Hotuba hizi zinapatikana (katika lugha nyingi) katika conference.lds.org.