2012
Kuitwa na Mungu na Kukubaliwa na Watu
Juni 2012


Ujumbe wa Urais wa Kwanza, Juni 2012

Kuitwa na Mungu na Kukubaliwa na Watu

Picha
Rais Henry B. Eyring

Kama washiriki wa Kanisa, tunaalikwa kila mara kuwakubali watu katika wito ya kuhudumu. Miaka iliyopita mwanafunzi wa miaka 18 alinionyesha kile kinachomaanisha kukubali watumishi wa Bwana. Mimi bado nimebarikiwa na mfano wake wa unyenyekevu.

Yeye alikuwa ameanza tu mwaka wake wa kwanza katika chuo. Yeye alikuwa amebatizwa chini ya mwaka mmoja kabla ya kuondoka nyumbani kwenda kuanza masomo yake katika chuo kikuu kikubwa. Huko mimi nilihudumu kama askofu wake.

Mwaka wa masomo ulipoanza, nilipata kuwa na mahojiano mafupi naye katika ofisi ya askofu. Nakumbuka kidogo juu ya mazungumzo ya kwanza bali kwamba aliongea juu ya changamoto zake katika eneo jipya lakini sitasahau mazungumzo yetu ya pili.

Yeye aliomba kuniona mimi katika ofisi yangu. Nilishangazwa aliposema, “Tunaweza kuomba pamoja, na naomba mimi niombe?” Nilikuwa karibu kusema kwamba nilikuwa tayari nimeomba na nilitarajia kwamba yeye alikuwa ameshafanya vivyo hivyo. Badala yake nilikubali.

Yeye alianza maombi yake kwa ushuhuda kwamba yeye alijua askofu aliitwa na Mungu. Yeye alimuuliza Mungu kuniambia kile yeye atafanya juu ya swala la athira kuu ya kiroho. Kijana huyu alimwambia Mungu kwamba alikuwa na hakika askofu tayari anajua mahitaji yake na atatoa ushauri anahitaji kusikia.

Alipokuwa akiongea, zile hatari mahususi ambazo angekumbana nazo zilinijia akilini. Ushauri wangu ulikuwa rahisi lakini uliotolewa kwa uwazi mkuu: omba daima, tii amri, na usiwe na hofu.

Huyo kijana, mwaka mmoja katika Kanisa, alifunza kwa mfano wa kile Mungu anaweza kufanya na kiongozi anayekubaliwa na imani na maombi ya wale ameitwa kuongoza. Huyo kijana alionyesha kwangu uwezo wa sheria ya hiari ya umma katika Kanisa (ona M&M 26:2). Ingawaje Bwana huwaita watumishi Wake kwa ufunuo, wanaweza kutenda tu baada kukubaliwa na wale walioitwa kuhudumia.

Kwa kura yetu ya kukubali, tunafanya ahadi takatifu. Tunaahidi kuwaombea watumishi wa Bwana na kwamba Yeye atawaongoza na kuwaimarisha (ona M&M 93:51). Tunaahidi kwamba tutatafuta na kutarajia kuhisi maongozi kutoka kwa Mungu katika ushauri wao na wanapotenda katika wito wao (ona M&M 1:38).

Hilo agano litahitaji kufanywa upya katika mioyo yetu kila mara. Mwalimu wako wa Shule ya Jumapili atajaribu kufunza kwa Roho, lakini kama mnavyoweza kufanya, mwalimu wenu anaweza kufanya makosa mbele za darasa. Ninyi, hata hivyo, mnaweza kuamua kusikiliza na kutafuta nyakati ambapo mtaweza kuhisi maongozi yakija. Katika wakati mtaona makosa machache na ushahidi zaidi wa kila mara kwamba Mungu anamhimili huyo mwalimu.

Tunapoinua mkono kukubali mtu, tunaweka ahadi ya kutekeleza madhumuni yoyote ya Bwana ambayo huyo mtu ameitwa kukamilisha. Wakati watoto wetu walipokuwa wadogo, mke wangu aliitwa kufunza watoto wadogo katika kata yetu. Sio tu kwamba niliinua mkono wangu kumkubali, bali pia nilimwombea na kisha nikauliza ruhusa ya kumsaidia yeye. Masomo niliyopata ya ufahamu wa kile wanawake hufanya na juu ya upendo wa Bwana kwa watoto bado hubariki familia yangu na maisha yangu.

Majuzi niliongea na yule mvulana ambaye alimkubali askofu wake miaka mingi iliopita. Nilifahamu kwamba Bwana na watu walikuwa wamemkubali yeye katika wito wake kama mmisionari, kama rais wa kigingi, na kama baba. Alisema wakati mazungumzo yetu yalipokamilika, “Bado huwa nakuombea kila siku.”

Tunaweza kufanya azimio la kumwombea mtu kila siku aliyeitwa na Mungu ili kutuhudumia sisi. Tunaweza kumshukuru mtu ambaye ametubariki sisi kwa huduma yake. Tunaweza kuamua kusonga mbele wakati mtu ambaye tumemkubali anapotuuliza watu wa kujitolea.1

Wale ambao wanawahimili watumishi wa Bwana katika ufalme Wake watahimiliwa na nguvu Zake zisizo na kifani. Tunahitaji hizi baraka zote.

Muhtasari

  1. Ona Teachings of Presidents of the Church: Joseph F. Smith (1998), 211–12.

Kufundisha kutoka kwa Ujumbe huu

Baada ya kushiriki huu ujumbe, fikiria kusoma dondoo ifuatayo: “Bwana atakufanya wewe kuwa chombo katika mikono Yake kama utakuwa mnyenyekevu, mwaminifu, na mwenye bidii. Mtapokea nguvu za ziada mnapokubaliwa na mkusanyiko na kutengwa” (Teaching, No Greater Call [1999], 20). Ita familia kukusanyika karibu na chombo kizito na umwulize mmoja kujaribu kukiinua. Ukiongeza mtu mmoja zaidi kwa wakati, waulize wanafamilia kusadia kuinua chombo. Zungumzieni kile kinachofanyika wakati kila mmoja anaposaidia. Fikiria kutia mkazo ushauri wa Rais Eyring kuhusu njia busara ambazo tunaweza kukubali wengine katika wito wao.