2012
Kuhudumu katika Hekalu
Agosti 2012


Vijana

Kuhudumu katika Hekalu

Nilipofika umri wa 17, nilianza kufikiria kwa makini juu ya maisha yangu ya baadaye, na niliomba kwa Baba wa Mbinguni juu ya kile ambacho ningefanya ili kujitayarisha kwenda kwenye misheni na kupokea Ukuhani wa Melkizedeki. Nilihisi kuwa nilihitajika kwenda hekaluni kila mara kwa sababu ni nyumba ya Bwana na ingekuwa mahali ambako ningejisikia karibu na Baba yangu wa Mbinguni.

Hivyo niliweka lengo la kufanya ubatizo 1,000 kwa mwaka. Amakweli nilihisi haja ya kuweka lengo hili; nilifunga ili kujua kama hili ndilo nililopaswa kufanya. Baba yetu wa Mbinguni alinijibu, na nikaanza kwenda kwenye Hekalu la Tampico Mexico kila Jumamosi.

Baada ya kufanya ubatizo 500, niliweka lengo la kufanya utafiti wa historia ya familia ya mababu zangu, na nikapenda kufanya utafiti sana kiasi kwamba singeweza kulala kwa sababu nilikuwa nikitafuta majina. Nilipata majina 50 na vizazi vinane vya historia ya familia yangu; nilisaidia kufanya kazi ya hekalu kwao wote.

Niliweza kufanya zaidi ya ubatizo 1,300, na nikahitimu kutoka seminari, nikapokea Ukuhani wa Melkizedeki, na sasa ninahudumu kama missionari wa muda wote, ambao ilikuwa ni moja wa malengo yangu makubwa katika maisha.