2013
Kushiriki na Rafiki
Februari 2013


Vijana

Kushiriki na Rafiki

Siku moja nilipokuwa ninasoma kwa ajili ya darasa langu la seminari, nilipata ushawishi mzuri na dhahiri. Nilipokuwa nikisoma somo la siku iliyofuata, niliona uso wa rafiki kutoka shuleni na nikawa na hisia ya nguvu kwamba ninapaswa kushiriki ushuhuda wangu naye.

Licha ya uwazi wa ushawishi huo, niliogopa. Nilikuwa na wasiwasi kuwa rafiki yangu angenikataa, zaidi hasa kwa sababu hakuonekana kuwa msichana wa aina ambaye angetaka kujiunga na Kanisa.

 Niliwazia hotuba ya Dada Mary N. Cook wa urais mkuu wa Wasichana ambapo alitupa changamoto kutia bidii na kuwa wajasiri.1 Nilitaka kuwa hivyo, basi nikamwandikia msichana huyu barua na kushuhudia ukweli wa Kanisa na upendo wangu wa Kitabu Cha Mormoni. Siku iliyofuata niliwekelea polepole nakala ya Kitabu cha Mormoni , pamoja na barua langu, katika mkoba wake.

 Kwa mshangao wangu, rafiki yangu alikuwa mpokevu sana kwa injili. Kuanzia siku hiyo, angeniambia kuhusu kile alichojifunza katika kujifunza kwake kwa Kitabu cha Mormoni. Wiki chache baadaye, nilimjulisha kwa wamisionari karibu mara moja, alipokea hakikisho kutoka kwa Roho Mtakatifu kuwa alichokuwa akijifunza kilikuwa cha kweli. Wamisionari nami tulilia alipokuwa akituambia kuhusu hisia zake. Rafiki yangu punde alibatizwa, na wazazi wake walistaajabu kuona mabadiliko ambayo yalikuwa yametendeka kwake.

 Ninafurahia sana niliweza kushinda uoga wangu na kusaidia kuleta injili katika maisha yake.

Muhtasari

  1. Ona Mary N. Cook, “Never, Never, Never Give Up!” Liahona, May 2010, 117–19.