2013
Wajibu wetu wa kuokoa
Oktoba 2013


Ujumbe wa Urais wa Kwanza, Oktoba 2013

Wajibu wetu wa Kuokoa

Picha
Rais Thomas S. Monson

Kwa Watakatifu wa siku za mwisho, hitaji la kuokoa ndugu na dada zetu ambao, kwa sababu moja au nyingine, wamepotea kutoka njia ya utendaji Kanisani ni la umuhimu wa milele. Je tunawajua watu kama hawa ambao mwanzo waliikumbatia injili? Kama ndivyo, nini wajibu wetu wa kuwaokoa?

Fikiria waliopotea kati ya wakongwe, wajane, na wagonjwa. Mara kwa mara wanapatikana katika mbuga kame zisizokalika zilizojitenga ziitwazo ukiwa. Wakati ujana unapotoka, wakati afya inapungua, wakati nguvu zinapungua, wakati mwanga wa matumaini ukiwaka kihafifu, wanaweza kusaidiwa na kuidhinishwa kwa mkono unaosaidia na moyo unaojua huruma.

Bila shaka, wapo wengine wanaohitaji kuokolewa. Baadhi wanashindana na dhambi wakati wengine wanatangatanga wakiwa na hofu au hali ya kutojali au ujinga. Kwa sababu yeyote ile, wamejitenga wenyewe kutoka utendaji ndani ya Kanisa. Na kwa uhakika watakuwa bila shaka wamebaki wamepotea kama haitazinduka ndani yetu—washiriki wa Kanisa walio hai—nia ya kukomboa na kuokoa.

Mtu wa Kuonyesha njia

Zamani kidogo nilipokea barua iliyoandikwa na mtu aliyepotoka kutoka Kanisani. Inawakilisha washiriki wetu wengi. Baada ya kuelezea jinsi alivyokosa kuwa mshiriki mkamilifu wa kanisa, aliandika:

Nilikuwa na mengi na sasa nina kidogo, Sina furaha na ninahisi kama ninashindwa katika kila kitu. Injili haijatoka kamwe moyoni mwangu, ingawa imetoka maishani mwangu. Ninaomba sala zako.

Tafadhali usitusahau sisi tulio huku nje—Watakatifu wa siku za mwisho tuliopotea. Najua lilipo Kanisa, lakini mara kwa mara nafikiri nahitaji mtu mwingine anioneshe njia, anishawishi, aniondolee mbali hofu, na anitolee ushuhuda.

Nilipokuwa nikisoma barua hii, mawazo yangu yaligeukia kwenye matembezi niliyofanya kwenye moja ya majumba makubwa ya sanaa ya Ulimwenguni—makumbusho maarufu ya Victoria na Albert yaliyopo London, Uingereza. Pale, ikiwa kwenye fremu kwa ustadi wa hali ya juu, ni mchoro wa utaalamu mkubwa uliochorwa mwaka 1831 na Joseph Mallord William Turner. Mchoro unaonyesha mawingu meusi mazito na bahari iliyochafuka kwa mawimbi makubwa yenye nguvu yakiashiria hatari na kifo. Mwanga toka kwenye meli iliyokwama waonekana kwa mbali. Mbele, mashua kubwa ya uokozi yarushwa juu na mawimbi yanayokuja ya maji yenye mapovu. Wanaume wavuta kwa nguvu makasi wakati mashua ikisukwasukwa katika dhoruba. Ufukoni wamesimama mke na watoto wawili, waliolowa na mvua na kupigwa na upepo. Wanatazama baharini kwa wasiwasi. Ndani ya mawazo yangu nilifupisha jina la mchoro. Kwangu ikawa Kwenda Kuokoa.1

Katika tufani za maisha, hatari inanyemelea. Wanaume na wanawake, wavulana na wasichana wanajikuta wamekwama na wanakabiliwa na maangamizo. Nani ataongoza mashua la uokoaji, akiacha nyuma starehe za nyumbani na familia, na kwenda kuokoa?

Kazi yetu sio kwamba haiwezekani. Tuko kwenye huduma ya Bwana; tunastahili msaada Wake.

Wakati wa huduma ya Bwana, Aliwaita Wavuvi kule Galilaya waache nyavu zao na wamfuate Yeye, akiwaambia wazi, “Nitawafanya nyinyi wavuvi wa watu”2 Na tujiunge na safu ya wavuvi wa wanaume na wanawake, ili tuweze kutoa msaada wowote tunaoweza.

Sisi kazi yetu ni kwenda na kuokoa wale waliacha usalama wa utendaji, ili waweze kuletwa kwenye meza ya Bwana kusherehekea neno Lake, na kufurahia uenzi wa Roho Yake, na kuwa” si wageni tena, wala si watu wa nje; ninyi ni raia pamoja na watu wa Mungu, na ni watu wa jamaa ya Mungu.”3

Kanuni ya Upendo

Nimegundua kwamba sababu mbili kuu za msingi zinaelezea kurudi kwa utendaji na kwa mabadiliko ya mienendo, tabia, na vitendo. Kwanza, mtu binafsi hurudi kwa sababu mtu fulani amewaonesha uwezekano wao wa milele na amewasaidia kuamua kuufanikisha. Watu wasioshiriki kikamilifu kanisani hawawezi kupumzika kwa muda mrefu wakiridhika na hali ya wastani pale wanapoona kwamba uwezo wa kufanya vizuri sana wanao.

Pili, wengine wanarudi kwa sababu wapendwa wao au “raia pamoja na watu wa Mungu” wamefuata maonyo ya Mwokozi,wamewapenda majirani zao kama wajipendavyo wenyewe,4 na wamewasaidia wengine kufanikisha ndoto zao na matakwa yao kutekelezeka.

Kichocheo katika mwenendo huu kilikuwa—na kitaendelea kuwa—ni kanuni ya upendo.

Katika hali ya kweli ya uamuzi, wale watu waliokwama katika bahari ya dhoruba kali ya mchoro wa Turner wako sawa na wengi wa washiriki wenzetu wasioshiriki kikamilifu wanaosubiri kuokolewa na wale wanaoongoza mashua za uokoaji. Mioyo yao inatamani msaada. Akina mama na akina baba wanasali kwa ajili ya wana na binti zao. Wake wanasihi mbingu ili waume zao waweze kufikiwa. Wakati mwingine watoto husali kwa ajili ya wazazi wao.

Ni maombi yangu kwamba tuweze kutamani kuwaokoa wale wasioshiriki kikamilifu na kuwarudisha kwenye furaha ya injili yaYesu Kristo, ili waweze kushirikiana nasi yale yote ambayo ushirika mkamilifu unatoa.

Tuweze kuwafikia na kuwaokoa waliopotea ambao wanatuzunguka: Wazee, Wajane, Wagonjwa, Walemavu, wasioshiriki kikamilifu waliolegea, na wale wasioshika amri. Na tuwanyooshee mkono unaosaidia na moyo unaojua huruma. Kwa kufanya hivyo, tutawaletea furaha miyoni mwao, na tutapata wingi wa ufahamu wa kutosheleza ambao unakuja kwetu tunaposaidia mwingine katika njia iendayo uzima wa milele.

Ufupisho wa taarifa

  1. Jina kamili la mchoro ni Mashua la kuokolea na Vifaa vya kibinadamu vikienda kwenye chombo kilichokwama Kikitoa ishara (Mianga ya Bluu) ya Dhiki.

  2. Matayo 4:19.

  3. Waefeso 2:19.

  4. Angalia Matayo 22:37–39.

Kufundisha kutoka kwa Ujumbe huu

Fikiria kuwauliza watu unaowatembelea kama wanamjua yeyote ambaye amekuwa akisumbuka juu ya kuhudhuria kanisa. Unaweza kuchagua mtu mmoja na umzungumzie njia za kuonyesha upendo, kama kumwalika mume au mke kushiriki katika mkutano wa jioni wa familia nyumbani au aje kwa mlo.