2016
Uzazi ni Kazi Takatifu
Septemba 2016


Ujumbe wa Mwalimu Mtembeleaji Septemba 2016

Uzazi ni Kazi Takatifu

Kwa maombi jifunze maneno haya na utafute msukumo wa kujua kitu cha kushiriki. Je, kuelewa “Tangazo kwa Ulimwengu” kutazidisha vipi imani yako katika Mungu na kubariki wale unaowachunga kupitia ualimu wa kutembelea? Kwa taarifa zaidi, nenda kwenye www.reliefsociety.lds.org.

Picha
Nembo ya Muungano wa Usaidizi wa Kina Mama

Imani, Familia, Usaidizi

Baba yetu wa Mbinguni ameanzisha familia ili kutusaidia sisi kufundisha kanuni sahihi katika hali ya upendo. Rais Thomas S. Monson alisema: “Mpe mtoto wako sifa na kumbatio; sema ‘Ninakupenda’ zaidi; kila mara onyesha shukrani. “Kamwe usikubali shida ya kutatuliwa kuwa muhimu zaidi ya mtu anayepaswa kupendwa.”1

Susan W. Tanner, aliyekuwa rais mkuu wa Wasichana, alifundisha: “Baba yetu wa Mbinguni anatoa mfano wa kielelezo tunachotakiwa kufuata. Anatupenda, anatufundisha, ni mvumilivu kwetu, na anatukabidhi uhuru wetu. … Wakati mwingine nidhamu, ambayo ina maana ‘kufundisha,’ inachanganywa na kukosoa. Watoto—pia watu wa umri wote—huimarika tabia kupitia upendo na kutiwa moyo kuliko kutafuta-makosa.”2

“Kama kwa uaminifu tutakuwa na sala ya familia, mafunzo ya maandiko, jioni ya familia ya nyumbani, baraka za ukuhani, na kuitukuza siku ya Sabato,” alisema Mzee Quentin L.Cook wa Akidi ya Mitume Kumi na Wawili, “watoto wetu watakuwa … wamejiandaa kwa makazi ya milele huko mbinguni, bila kujali yanayotokea kwenye ulimwengu mgumu.”3

Maandiko ya Ziada

1 Nefi 8:37; 3 Nefi 22:13; Mafundisho na Maagano 93:40; 121:41

Hadithi Hai

Nilikuwa nasoma gazeti wakati mmoja wa wajukuu zangu alinikaribia,” alisema Mzeer Robert D. Hales wa Akidi ya Kumi na Wawili. “Nikiwa ninasoma, nilifurahishwa kusikia sauti yake nzuri ikiongea kwa nyuma. Fikiria mshangao wangu, muda mchache baadaye, alijipenyeza katikati ya gazeti na mimi. Akichukua uso wangu kwenye mikono yake na akilileta pua lake karibu na langu, aliuliza, ‘Babu! Upo?”

“… Kuwa hapo ina maana kuelewa mioyo ya vijana wetu na kuungana nao. Na kuungana pamoja nao ina maana siyo tu kuongea nao bali kufanya vitu pamoja nao pia. …

Tunapaswa kupanga na kuchukua fursa ya muda wa kufundisha. …

“… Kadiri ninavyoishi, ndivyo kadiri ninavyogundua kwamba muda wa mafundisho katika ujana wangu, hususani yaliyotolewa na wazazi wangu, yamesaidia maisha yangu na kunifanya niwe hivi.”4

Muhtasari

  1. Thomas S. Monson, “Love at Home—Counsel from Our Prophet,” Liahona, Aug. 2011, 4.

  2. Susan W. Tanner, “Did I Tell You … ?” Liahona, Mei. 2003, 74.

  3. Quentin L. Cook, “The Lord is My Light,” Liahona, Mei 2015, 64.

  4. Robert D. Hales, “Our Duty to God: The Mission of Parents and Leaders to the Rising Generation,” Liahona, May 2010, 96, 95.

Zingatia Hili

Kwa nini injili inafundishwa vizuri kwa lugha na mifano ya upendo?