2018
Kujiandaa Kusikia Sauti ya Mungu.
March 2018


Vijana

Kujiandaa Kusikia Sauti ya Mungu.

Rais Uchtdorf anaelezea ni kwa jinsi gani kitu cha kwanza Mungu alichofanya baada ya kumuumba mwanaume na mwanamke ilikuwa kuzungumza nao na kuwapa taarifa na maelekezo ya thamani. Tunapata baraka kama hiyo ifikapo Aprili na Oktoba wakati wa mkutano mkuu, wakati viongozi wa Kanisa wanapotuhutubia na kutupatia ushauri ambao Bwana anataka tusikie.

Je umewahi kusikia sauti ya Mungu kupitia watumishi Wake wakati wa mkutano mkuu? Je umewahi kujisikia kama ujumbe mmoja mahususi ambao umekupa jibu ulilokuwa ukitafuta? Katika shajara, ungeweza kuandika uzoefu huo na jinsi ulivyokusaidia. Basi jiandae kusikia sauti ya Bwana katika mkutano huu ujao kwa kuandika maswali uliyonayo na kujifunza maswali hayo wakati wa usomaji wako wa maandiko. Omba kwa Baba wa Mbinguni, ukiomba kupokea majibu na utambuzi wakati wa mkutano. Unapowasikiliza watumishi wa Bwana, fokasi kwenye ushawishi binafsi unaopokea. Umejifunza nini? Je ni kwa namna gani ulijisikia kusukumwa kubadilika? Andika juu ya kushawishika huko kwa sababu huyo ni Roho anaongea nawe!

Daima kumbuka kwamba Baba wa Mbinguni anakupenda na atakuongoza katika mwelekeo sahihi. Kadiri unavyojitahidi kusikia sauti Yake kupitia watumishi Wake, utabarikiwa na kujengeka.