2018
Yusufu Anauzwa Misri
April 2018


Hadithi za Maandiko

Yusufu Anauzwa Misri

Kutoka Mwanzo 37–41.

Picha
Joseph Is Sold into Egypt 1
Picha
Joseph Is Sold into Egypt 2
Picha
Joseph Is Sold into Egypt 3

Yusufu alikuwa na kaka 11 Baba yake alimpa koti zuri, lenye rangi mbalimbali. Mungu alimwambia Yusufu kwamba angewaongoza kaka zake.

Kaka wakubwa wa Yusufu walikasirika. Hawakutaka Yusufu awe kiongozi wao! Walimuuza kwa watu waliokuwa wakienda Misri, na akawa mtumwa.

Yusufu alifanya kazi kwa bidii. Alifanya chaguzi nzuri, hata pale ambapo watu walisema uongo kumhusu yeye na kumweka gerezani.

Hata katika nyakati ngumu, Yusufu alimtumaini Mungu. Na Mungu alikuwa pamoja na Yusufu. Yusufu akawa kiongozi Misri! Alipokuwa mkubwa, alisaidia kuongoza familia yake, kama ambavyo Mungu alisema.

Ninaweza kumuamini Mungu kama Yusufu. Ninaweza kuchagua mema. Mungu, atakuwa pamoja nami katika hali yo yote.