2022
Zaburi Inafundisha kuhusu Yesu Kristo
Agosti 2022


“Zaburi Inafundisha kuhusu Yesu Kristo” Ujumbe wa Kila Mwezi wa Gazeti la Rafiki Agosti 2022

“Zaburi Inafundisha kuhusu Yesu Kristo”

Ujumbe wa Kila Mwezi wa Gazeti la Rafiki Agosti 2022

Zaburi Inafundisha kuhusu Yesu Kristo

Picha
Daudi akiwa na kinubi

Vielelezo na Apryl Stott

Zaburi ni nyimbo takatifu. Watu katika Biblia waliandika zaburi ili kumsifu Mungu. Nyingi za zaburi zao zinafundisha kuhusu Yesu Kristo. Hapa kuna kile ambacho baadhi ya zaburi kutoka katika Biblia hufundisha.

Picha
Yesu Kristo amesimama juu ya mwamba

Mimi nampenda Bwana. Yeye ni mwamba wangu na nguvu yangu. Nitamtumainia Yeye. Nitamsifu Yeye.

Picha
Yesu amemshikilia kondoo

Bwana ndiye Mchungaji wangu. Yeye huniongoza kwenye majani mabichi. Yeye huniongoza kwenye maji ya utulivu. Sitaogopa.

Picha
Yesu ameshikilia taa

Bwana ndiye nuru yangu. Sitaogopa. Nitakuwa na ujasiri. Ataufanya moyo wangu kuwa thabiti.

Picha
watu kanisani

Nampenda Yesu Kristo, na Yeye ananipenda. Ninaweza kumsifu Yeye wakati ninapojifunza na kuimba kumhusu Yeye.

Ukurasa wa Kupaka Rangi

Bwana Ndiye Mchungaji Wangu

Picha
Yesu Kristo amembeba mwana kondoo

Bofya kwenye picha ili kupakua.

Kielelezo na Apryl Stott

Unahisi vipi kuhusu upendo wa Yesu?