Maandiko Matakatifu
Moroni 2


Mlango wa 2

Yesu aliwapa wale wanafunzi kumi na wawili Wanefi uwezo wa kutoa kipawa cha Roho Mtakatifu. Karibia mwaka 401–421 B.K.

1 Maneno ya Kristo, aliyowazungumzia awanafunzi wake, kumi na wawili ambao alikuwa amewateua, wakati alipowawekea mikono yake juu yao—

2 Na aliwaita kwa majina, akisema: Mtamwita Baba katika jina langu, katika sala ya nguvu; na baada ya kufanya hivi mtakuwa na auwezo kwamba kwa yule ambaye mtamwekea bmikono yenu, cmtampa Roho Mtakatifu; na katika jina langu mtamtoa, kwani hivyo ndivyo mitume wangu hufanya.

3 Sasa Kristo alisema maneno haya kwao wakati wa kwanza wa kuonekana kwake; na umati haukusikia, lakini wanafunzi walisikia; na kwa wengi ambao awaliwawekea mikono yao, Roho Mtakatifu aliwashukia.