Maandiko Matakatifu
Moroni 4


Mlango wa 4

Namna wazee na makuhani wanavyohudumia sakramenti ya mkate inaelezwa. Karibia mwaka 401–421 B.K.

1 Njia ya wazee wao na makuhani wakibariki mwili na damu ya Kristo kwa washiriki; na waliubariki kulingana na amri za Kristo; kwa hivyo tunajua njia ni ya kweli; na mzee au kuhani aliibariki—

2 Na walipiga magoti chini na washiriki, na kuomba kwa Baba katika jina la Kristo, wakisema:

3 Ee Mungu, Baba wa Milele, tunakuomba katika jina la Mwanao, Yesu Kristo, ubariki na utakase mkate huu kwa roho za wale wote watakaoula, ili waweze kuula kwa ukumbusho wa mwili wa Mwanao, na wakushuhudie, Ee Mungu, Baba wa Milele, kwamba wako radhi kujichukulia juu yao jina la Mwanao, na daima kumkumbuka, na kushika amri zake ambazo amewapa, ili daima Roho wake apate kuwa pamoja nao. Amina.