Maandiko Matakatifu
Mafundisho na Maagano 131


Sehemu ya 131

Mafundisho ya Joseph Smith Nabii, yaliyotolewa huko Ramus, Illinois, 16 na 17 Mei 1843.

1–4, Ndoa ya selestia ni muhimu kwa kuinuliwa katika mbingu ya juu; 5–6, Jinsi watu wanavyotiwa muhuri kwa uzima wa milele inaelezwa; 7–8, Roho zote ni maada.

1 Katika utukufu wa selestia kuna mbingu au daraja tatu;

2 Na ili kupata la juu zaidi, mwanadamu lazima aingie katika utaratibu huu wa ukuhani [ikimaanisha agano jipya na lisilo na mwisho la ndoa];

3 Na kama hakufanya hivyo, hawezi kulipata.

4 Anaweza kuingia katika nyingine, lakini huo ndiyo mwisho wa ufalme wake; hawezi kuongezeka.

5 (17 Mei 1843.) Neno la unabii lililo imara zaidi linamaanisha kujua kwamba mtu ametiwa muhuri kwa uzima wa milele, kwa njia ya ufunuo na roho wa unabii, kwa kupitia uwezo wa Ukuhani Mtakatifu.

6 Haiwezakani kwa mwanadamu kuokolewa katika ujinga.

7 Hakuna kitu kisichoundwa na maada. Roho yote ni maada, lakini ni angavu zaidi au safi, na yaweza kutambuliwa tu kwa macho yaliyo safi zaidi;

8 Hatuwezi kuiona; lakini wakati miili yetu itakaposafishwa tutaona kwamba yote ni maada.