Maandiko Matakatifu
Mafundisho na Maagano 16


Sehemu ya 16

Ufunuo uliotolewa kupitia Joseph Smith Nabii kwa Peter Whitmer Mdogo, huko Fayette, New York, Juni 1829. (ona kichwa cha habari cha sehemu ya 14). Peter Whitmer Mdogo baadaye alikuja kuwa mmoja wa Mashahidi Wanane wa Kitabu cha Mormoni.

1–2, Mkono wa Bwana u juu ya ulimwengu wote; 3–6, Kuhubiri injili na kuokoa nafsi ni jambo la thamani kubwa.

1 Sikiliza, mtumishi wangu Peter, na usikilize maneno ya Yesu Kristo, Bwana wako na Mkombozi wako.

2 Kwani tazama, ninasema nawe kwa ukali na kwa nguvu, kwani mkono wangu u juu ya ulimwengu wote.

3 Na nitakuambia wewe yale ambayo hapana mtu ajuaye isipokuwa mimi na wewe pekee—

4 Kwani mara nyingi umetamani kujua kutoka kwangu kwamba ni kipi ambacho kitakuwa na thamani kubwa kwako.

5 Tazama, umebarikiwa wewe kwa jambo hili, na kwa kusema maneno yangu ambayo nimekupa kulingana na amri zangu.

6 Na sasa, tazama, ninakuambia, kwamba jambo ambalo litakuwa na thamani kubwa kwako ni kutangaza toba kwa watu hawa, ili uweze kuzileta nafsi hizo kwangu, na kwamba uweze kupumzika pamoja nao katika ufalme wa Baba yangu. Amina.

      • Tazama M&M 15 kwa ajili ya rejeo linalofanana na hili.