Misaada ya Kujifunza
TJS, Kutoka 34


TJS, Kutoka 34:1–2, 14. Linganisha na Kutoka 34:1–2, 14; M&M 84:21–26

Mungu anaandika tena juu ya mbao za mawe zilizotayarishwa na Musa lakini anaondoa Ukuhani wa Melkizedeki na ibada zake kutoka kwa wana wa Israeli. Anawapa sheria za amri za kimwili badala yake.

1 Na Bwana akamwambia Musa, Chonga mbao mbili nyingine za mawe, mfano wa zile za kwanza, nami nitaandika juu yake pia, maneno ya torati, kama yalivyokuwa yameandikwa mara ya kwanza juu ya mbao hizo ulizozivunja; lakini haitakuwa sawa sawa na za kwanza; kwa maana nitauondoa ukuhani kutoka katikati yao; kwa hiyo mfano wangu mtakatifu, na ibada zake, hazitakwenda mbele yao; kwani uwepo wangu hautakuwepo katikati yao, nisije nikawaangamiza.

2 Lakini nitawapa wao torati kama vile mwanzo, lakini itakuwa kulingana na torati ya amri ya kimwili; kwani nimeapa katika hasira yangu, kwamba hawataingia katika uwepo wangu, rahani mwangu, katika siku ya kusafiri kwao. Kwa hiyo fanya kama nilivyokuamuru, nawe uwe tayari asubuhi, na asubuhi ukwee katika mlima Sinai, na hudhurisha nafsi yako kwangu, huko katika kilele cha mlima.

Yehova ni jina ambalo kwalo watu wa Agano la Kale walimjua Bwana Yesu Kristo.

14 Maana usiabudu miungu wengine, kwani Bwana, ambaye jina lake ni Yehova, ni Mungu mwenye wivu.