Misaada ya Kujifunza
TJS, Mwanzo 15


TJS, Mwanzo 15:9–12. Linganisha na Mwanzo 15:1–6

Ibrahimu anajifunza juu ya Ufufuko na anaona ono la huduma ya Yesu akiwa duniani.

9 Na Abramu akasema, Bwana Mungu, kwa namna gani utanipa nchi hii kuwa urithi usio na mwisho?

10 Naye Bwana akasema, Japokuwa utakuwa umekufa, je, mimi siwezi kukupa?

11 Na kama utakufa, bado wewe utaimiliki, kwani siku yaja, ambayo Mwana wa Mtu ataishi; lakini ataishi namna gani kama hakuwa amekufa? lazima kwanza yeye ahuishwe.

12 Na ikawa, kwamba Abramu akaangalia na kuziona siku za Mwana wa Mtu, na alifurahi, na nafsi yake ikapata pumziko, naye akaamini katika Bwana; na Bwana akamhesabia hilo kuwa haki.