Misaada ya Kujifunza
TJS, Mwanzo 19


TJS, Mwanzo 19:9–15. Linganisha na Mwanzo 19:8–10

Lutu anajizuia na uovu wa Sodoma, na malaika wanamlinda.

9 Nao wakamwambia, Ondoka hapa. Na walikuwa wamemkasirikia.

10 Na wakasemezana wao kwa wao, Mtu huyu mmoja amekuja kwetu kuketi miongoni mwetu, naye kumbe sasa anataka kujifanya kuwa mwamuzi; basi sasa tutamtenda yeye vibaya kuliko hao.

11 Kwa hiyo wao wakamwambia huyu mtu, Tutawachukua wanaume hao, na binti zako pia; nasi tutawafanya kadiri tupendavyo.

12 Sasa hii ilikuwa kulingana na uovu wa Sodoma.

13 Na Lutu akasema, Tazameni sasa, mimi ninao mabinti wawili ambao hawajamjua mume; niacheni, ninakusihini, ninyi ndugu zangu kwamba nisiwatoe kwenu; nanyi mkawafanyia wao kama muonavyo kuwa vyema machoni penu;

14 Kwani Mungu hatamhesabia haki mtumishi wake katika jambo hili; kwa hiyo, acheni ninawasihini ninyi ndugu zangu, kwa mara hii moja tu, kwamba kwa watu hawa msiwatende lolote, ili wapate kuwa na amani katika nyumba yangu; kwani kwa sababu hiyo wamekuja chini ya kivuli cha paa la nyumba yangu.

15 Na wakamkasirikia Lutu na wakasogea karibu ili kuuvunja mlango, lakini malaika wa Mungu ambao walikuwa watu watakatifu, wakanyoosha mikono yao na kumvuta Lutu kwao ndani ya nyumba, na wakafunga mlango.