Misaada ya Kujifunza
TJS, Mwanzo 48


TJS, Mwanzo 48:5–11. Linganisha na Mwanzo 48:5–6

Efraimu na Manase wanakuwa makabila ya Israeli. Kama vile Yusufu wa kale alivyoiokoa familia yake kimwili, uzao wake utaiokoa Israeli kiroho katika siku za mwisho.

5 Na sasa, juu ya wana wako wawili, Efraimu na Manase, ambao walizaliwa kwako katika nchi ya Misri, kabla sijaja kwako Misri; tazama, hao ni wangu na Mungu wa baba zangu atawabariki; hata kama vile Reubeni na Simeoni watabarikiwa, kwa maana hao ni wangu; kwa sababu hiyo hao wataitwa kwa jina langu. (Kwa hiyo waliitwa Israeli.)

6 Na wazao wako utakao wazaa baada ya hawa, watakuwa wako, na wataitwa kwa jina la ndugu zao katika urithi wao, katika makabila; kwa hiyo hao waliitwa makabila ya Manase na Efraimu.

7 Na Yakobo akamwambia Yusufu, Wakati Mungu wa baba zangu aliponitokea katika luzu, katika nchi ya Kaanani; aliapa kwangu, kwamba yeye atanipa mimi, na kwa uzao wangu, nchi kwa ajili ya milki isiyo na mwisho.

8 Kwa hiyo, Ee mwanangu, yeye amenibariki kwa kukuinua wewe kuwa mtumishi kwangu, kwa kuiokoa nyumba yangu kutokana na mauti;

9 Kwa kuwakomboa watu wangu, ndugu zako, kutokana na njaa ambayo ilikuwa kali katika nchi; kwa sababu hiyo Mungu wa baba zako atakubariki, na matunda ya viuno vyako, kwamba yatabarikiwa kuliko ya ndugu zako, na kuliko ya nyumba ya baba yako;

10 Kwa maana wewe umeshinda, na nyumba ya baba yako imekupigia magoti, hata kama ilivyooneshswa kwako kabla ya wewe hujauzwa Misri kwa mkono wa ndugu zako; kwa sababu hiyo ndugu zako watakupigia magoti, kutoka kizazi hadi kizazi, kwa tunda la viuno vyako milele;

11 Kwa maana wewe utakuwa nuru kwa watu wangu, kuwakomboa katika siku za kukamatwa kwao, kutoka utumwani; na kuwaletea wokovu, wakati wakiwa kabisa wamepiga magoti chini ya dhambi.