Misaada ya Kujifunza
TJS, Zaburi 11


TJS, Zaburi 11:1–5. Linganisha na Zaburi 11:1–5

Katika siku za mwisho wenye haki watakimbilia kwenye mlima wa Mungu. Wakati Bwana atakapokuja, atawaangamiza waovu na atawaokoa wenye haki.

1 Katika siku ile utakayo kuja, Ee Bwana; na nitakutegemea wewe. Utawaambia watu wako, kwani sikio langu limesikia sauti yako; utamwambia kila mtu, Kimbilia mlimani kwangu; na wenye haki watakimbia kama ndege aliyeachiwa kutoka kwenye mtego wa mwindaji.

2 Kwani waovu hupinda upinde; Tazama, na huweka tayari mishale yao katika upote, ili waweze kuwapiga kwa siri wenye haki katika mioyo, kuangamiza misingi yao.

3 Lakini misingi ya waovu itaangamizwa, na watafanya nini?

4 Kwani Bwana, atakapokuja katika hekalu lake takatifu, akiwa amekaa kwenye kiti cha enzi cha Mungu mbinguni, macho yake yatawaona watu wote waovu.

5 Tazama kope zake zitawapeleleza watoto wa wanadamu, na atawakomboa wenye haki, na watajaribiwa. Bwana anawapenda wenye haki, lakini waovu, na yeye anayependa fujo, nafsi yake anaichukia.