Misaada ya Kujifunza
TJS, Zaburi 24


TJS, Zaburi 24:7–10. Linganisha na Zaburi 24:7–10

Mfalme wa Utukufu atawakomboa watu Wake wakati wa ujio Wake.

7 Inueni vichwa vyenu, Enyi vizazi vya Yakobo; na inukeni; na Bwana ni hodari na mwenye nguvu; Bwana hodari wa vita, ambaye ni mfalme wa utukufu, atakustawisha milele.

8 Naye atazikunja mbingu na atashuka chini kuwakomboa watu wake; na kuwafanya ninyi jina lisilo na mwisho; kuwaweka juu ya mwamba wake usio na mwisho.

9 Inueni vichwa vyenu, Enyi vizazi vya Yakobo; inueni vichwa vyenu, enyi vizazi visivyo na mwisho, na Bwana wa majeshi, mfalme wa wafalme;

10 Hata mfalme wa utukufu atawajia; na atawakomboa watu wake, na atawaweka katika haki. Sela.