Misaada ya Kujifunza
TJS, 1 Samweli 16


TJS, 1 Samweli 16:14–16, 23. Linganisha na 1 Samweli 16:14–16, 23; mabadiliko ya aina hiyo hiyo yalifanywa kwa 1 Samweli 18:10 na 19:9

Pepo mchafu ambaye huja juu ya Sauli haji kutoka kwa Bwana.

14 Lakini Roho wa Bwana akaondoka kwa Sauli, na pepo mchafu ambaye hakuwa wa Bwana akamsumbua.

15 Nao watumishi wa Sauli wakamwambia, Tazama sasa, pepo mchafu ambaye si wa Mungu anakusumbua.

16 Bwana wetu sasa na uwaamuru watumishi wako, walioko hapa mbele yako, wamtafute mtu, aliye stadi wa kupiga kinubi; na itakuwa, wakati pepo mchafu, ambaye si wa Mungu, atakapokuwa juu yako, yeye atapiga kinubi kwa mkono wake, nawe utapona.

23 Na ikawa, wakati pepo mchafu, ambaye hakuwa wa Mungu, alipokuwa juu ya Sauli, Daudi akachukua kinubi, na akakipiga kwa mkono wake; naye Sauli akaburudishwa; na akapona, na yule pepo mchafu akamwacha.