Misaada ya Kujifunza
TJS, 2 Petro 3


TJS, 2 Petro 3:3–13. Linganisha na 2 Petro 3:3–13

Katika siku za mwisho, watu wengi watamkana Bwana Yesu Kristo. Wakati atakapokuja, majanga mengi ya asili yatatokea. Kama tutavumilia katika haki, tutapokea dunia mpya.

3 Huna budi kujua hili kwanza, kwamba katika siku za mwisho watakuja wafanya dhihaka, wakifuata ashiki zao wenyewe.

4 Wakimkana Bwana Yesu Kristo, na wakisema, Iko wapi ahadi ya kuja kwake? kwani tangu mababa walipolala, vitu vyote lazima viendelee kama vilivyo, na vimeendelea kama vilivyo kutoka mwanzo wa uumbaji.

5 Kwani kwa hili kwa radhi yao ni wajinga wa kile cha mbingu za zamani, na dunia kusimama ndani maji na nje ya maji, ziliumbwa kwa neno la Mungu;

6 Na kwa neno la Mungu, ulimwengu ambao wakati huo ukiwa umefurika na maji uliangamia;

7 Bali mbingu na dunia, ambazo zipo sasa, zinahifadhiwa na neno lilelile, zimehifadhiwa hadi moto dhidi ya siku ya hukumu na kuangamia kabisa kwa watu waovu.

8 Lakini kuhusu ujio wa Bwana, wapendwa, Sitawafanya wajinga wa kitu hiki kimoja, kwamba siku moja kwa Bwana ni sawa na miaka elfu moja, na miaka elfu moja kama siku moja.

9 Bwana sio mzembe kuhusu ahadi yake na ujio wake, katika njia ambayo baadhi ya watu wanafikiri juu ya uzembe; lakini usitahimilivu kuhusu sisi, bila kuwa tayari kwamba yeyote aangamie, bali kwamba wote watubu.

10 Bali siku ya Bwana itakuja kama mwizi usiku, ambapo mbingu zitatikisika, na dunia pia itatetemeka, na milima itayeyuka, na kupotea kwa sauti kuu na vitu vya asili vitajazwa joto kali; dunia pia itajazwa, na matendo maovu ambayo yapo ndani yake yataunguzwa.

11 Kwa hiyo basi kama vitu hivi vyote vitateketezwa, ni aina gani ya watu mnatakiwa muwe katika mwenendo mtakatifu na uungu,

12 Kungojea, na kujitayarisha kwa siku ya ujio wa Bwana katika hili vitu viovu vya mbinguni vikiwa vinawaka, vitayeyushwa, na milima itayeyuka kwa joto kali?

13 Hata hivyo, kama tutavumilia, tutabakizwa kama ilivyo ahadi yake. Na tunangojea mbingu mpya, na dunia mpya ambayo haki yakaa ndani yake.