2010–2019
Wanawake Shupavu
Aprili 2017


Wanawake Shupavu

Wanawake shupavu ni wafuasi ambao wamejikita kwa Mwokozi Yesu Kristo na wanatumaini kupitia ahadi ya dhabihu yake ya Upatanisho.

Wapendwa dada zangu, tunawapenda sana na tuwashukuru kwa ukarimu wenu na mjibizo wa ujasiri kwa mwaliko wa urais wa Kwanza na juhudi za #IWasAStranger. Tafadhali endeleeni kuomba, kusikiliza minong’ono ya Roho, na kufanyia kazi ushawishi mnaopokea.

Aijalishi ninasafiri nchini au ulimwenguni kote, ni kitu cha kawaida kwa mtu kuuliza, “Unanikumbuka?” Kwa sababu kwa kweli sijakamilika, lazima nikiri kwamba mara nyingi sikumbuki majina. Hata hivyo, nakumbuka upendo ule halisi Baba wa Mbinguni ameniruhusu kuuhisi ninapokutana na mabinti na wanawe wenye thamani.

Hivi karibuni nilipata nafasi ya kutembelea baadhi ya wanawake wapendwa walio gerezani. Tulipopeana kwa heri zilizojaa hisia, mwanamke mmoja mpendwa alitoa ombi, “Dada Burton, tafadhali usitusahau.” Natumai yeye na wengine wanaotaka kukumbukwa watahisi hivyo ninaposhiriki nanyi mawazo machache.

Wanawake Shupavu katika Siku za Mwokozi: Kujikita katika Mwokozi Yesu Kristo

Dada zetu kwa miaka mingi wameonyesha mtindo wa uaminifu wa ufuasi ambao sisi pia tunautafuta. Katika Agano Jipya ina taarifa za wanawake [shupavu], waliotajwa na wasiotajwa, waliotumia imani katika Yesu Kristo, walijifunza na waliishi kufuatana na mafundisho Yake, na walishuhudia huduma Yake, miujiza Yake, na ukuu Wake. Wanawake hawa wakawa wafuasi wa mfano mwema na mashahidi muhimu katika kazi ya wokovu.1

Picha
Wanawake Shupavu

Kumbuka matukio haya katika kitabu cha Luka. Kwanza, wakati wa huduma ya Mwokozi:

“Na ikawa … kwamba [Yesu] alikuwa akizunguka zunguka katika miji na vijiji, akihubiri na kutangaza habari njema ya ufalme wa Mungu: na thenashara walikuwa pamoja naye,

“Na wanawake shupavu,  … Mariamu aitwaye Magdalene, … na Yoana … , na Susana, na wengine wengi waliokuwa wakimhudumia.”2

Pili, kufuatia Ufufuko Wake:

“Na wanawake shupavu  …waliokwenda kaburini asubuhi na mapema;

“…Wasiuone mwili wake, wakaja, wakasema, ya kwamba  … wametokewa na malaika, waliosema kwamba yu hai.”3

Nimesoma na kupitia maelezo yanayoonekana yasiyo ya ajabu “wanawake shupavu,” mara nyingi kabla, lakini hivi karibuni nilipotafakari kwa makini, maneno hayo yalionekana kujitokeza kwenye ukurasa. Fikiria mifanano hii ya maana moja ya neno shupavu kama likiunganishwa na waaminifu wanawake shupavu:waaminifu: “walioshawishika,” “chanya,” “wajasiri,” “imara,” “wenye msimamo,” “wa uhakika,” na “wa kutegemewa.”4

Nilipotafakari vielezo hivyo vyenye nguvu, Nilikumbuka wawili kati ya wanawake shupavu wa Agano Jipya ambao walitoa shuhuda chanya, za ujasiri, imara, hakika za Mwokozi. Japo wao, kama sisi, hawakuwa wakamilifu, ushahidi wao huvuvia.

Kumbuka mwanamke msamaria pale kisimani aliyewaalika watu kuja na kuona alichojifunza kuhusu Mwokozi? Alitoa ushahidi wa hakika kwa njia ya swali: “Huyu siye Kristo?”5 Ushuhuda wake na mwaliko wake ulikuwa na msukumo kwamba “wengi … walimwamini Kristo.”6

Picha
Martha anatoa ushuhuda juu ya Mwokozi.

Kufuatia kifo cha kaka yake, Lazaro, Martha, mfuasi mpendwa na rafiki wa Bwana, alitangaza kwa kile huenda kingekuwa hisia kali, “Bwana, kama ungalikuwepo hapa, ndugu yangu hangalikufa.” Fikiria uhakika wake alipoendelea, “Lakini hata sasa najua ya kuwa yoyote utakayomwomba Mungu, Mungu atakupa.” Baadaye alishuhudia, “Nimesadiki ya kwamba wewe ndiye Kristo, mwana wa Mungu, Yule ajaye ulimwenguni.”7

Tunajifunza kutoka kwa kina dada hawa kwamba wanawake shupavu ni wafuasi waliojikita kwa Mwokozi Yesu Kristo na wanatumaini kupitia ahadi ya dhabihu yake ya upatanisho.

Wanawake Shupavu wa Urejesho Watunzao Maagano: Tayari Kujitolea

Zamani wanawake shupavu walijitolea wakati waliposhuhudia na kuishi mafundisho ya Yesu. Wanawake shupavu katika siku za mwanzo za urejesho pia walifanya hivyo. Drusilla Hendricks na familia yake walikuwa kati ya hao ambao kama waongofu wapya, waliumia wakati wa mateso ya watakatifu huko Wilaya ya Clay Missouri. Mumewe alikuwa amepooza kabisa wakati wa Mapigano ya Mto Crooked. Aliachwa kumtunza vilevile kukidhi familia yake.

“Katika wakati mmoja wa dhiki, wakati familia haikuwa na chakula, alikumbuka kwamba sauti ilimwambia, ‘vumilia, kwani Bwana atatoa.’

Wakati mwanae alipotakiwa kujitolea kwenye Batalioni ya Wamormoni, mwanzo Drusilla alikataa na alihangaika katika sala kwa Baba wa Mbinguni mpaka “ilikuwa kama sauti ilimwambia, ‘Je unataka utukufu wa juu?’ Alijibu kiuhalisia, ‘Ndiyo,’ na sauti iliendelea, ‘unafikiria kuupataje isipokuwa kupitia kujitolea kwa hali ya juu?’”8

Tunajifunza kutoka kwa huyu mwanamke shupavu kwamba ufuasi unaotunza maagano huhitaji utayari wetu wa kujitolea.

Wanawake Shupavu Leo: Kukumbuka na Kujiandaa Kusherehekea Kurudi Kwake.

Nimewataja wanawake shupavu katika siku za Mwokozi na katika siku za mwanzo za Urejesho wa injili. Vipi kuhusu mifano ya wafuasi na shuhuda za wanawake shupavu katika siku yetu wenyewe?

Picha
Dada Burton akiwa na kina dada huko Asia

Katika jukumu langu la hivi majuzi huko Asia, nilipatiwa msukumo tena na wengi wa wanawake shupavu niliokutana nao. Nilivutiwa hasa na kizazi cha kwanza cha waumini huko India , Malaysia, na Indonesia, ambao hujitahidi kuishi utamaduni wa injili katika nyumba zao, wakati mwingine kwa kujitolea sana sababu kuishi injili mara nyingi hukinzana na tamaduni za familia na nchi. Vizazi vingi vya wanawake shupavu wa Hong Kong na Taiwan huendelea kubariki maisha ya familia zao, waumini wa kanisa, na jamii kwa kubaki wamejikita kwa Mwokozi na kujitolea kwa hiari kutunza maagano. Wanawake shupavu kama hao wapo kote kanisani. .

Picha
Dada Burton akiwa na kina dada huko Asia

Mwanamke shupavu mwingine ambaye amebariki maisha yangu kwa miongo amepigana kwa miaka 15 iliyopita dhidi ya ugonjwa wa kudhoofisha, mgumu na endelevu uitwao ugonjwa wa kudhoofisha mwili. Japo hatoki kwenye kiti chake cha magurudumu, anajitahidi kuwa mwenye shukrani na hutunza “Orodha ya Naweza Naweza”: orodha endelevu ya vitu anavyoweza kufanya, kama vile naweza kupumua, naweza kumeza, naweza kusali, na naweza kuhisi upendo wa Mwokozi. Hutoa ushahidi wake wa hakika wa Mwokozi karibu kila siku kwa familia na marafiki.

Hivi karibuni nimesikia hadithi ya Jenny. Ni mmisionari aliyerudi ambaye wazazi wake waliachana alipokuwa akitumikia misheni. Alisema jinsi mawazo ya kurudi nyumbani “yalimwogopesha sana.” Lakini mwisho wa misheni yake huko Italia, alipopita kwenye nyumba ya misheni akielekea nyumbani Marekani, mwanamke shupavu , mke wa rais wa misheni, kwa upole alimhudumia kwa kuchana tu nywele zake.

Miaka kadhaa baadaye, mwanamke shupavu mwingine, Terry—rais wa kigingi wa Muungano wa Usaidizi wa Kina Mama na mfuasi wa Yesu Kristo—alibariki maisha ya Jenny wakati Jenny alipoitwa kama rais wa kata wa Muungano wa Usaidizi wa Kina Mama. Wakati ule, Jenny alikuwa akishughulikia tasnifu yake kwa ajili ya shahada yake ya udaktari. Siyo tu kwamba Terry alitumikia kama mnasihi kwa Jenny kama kiongozi, lakini pia alikaa nae masaa 10 hospitalini wakati Jenny alipopata utambuzi wa kutia hofu wa ugonjwa wa damu. Terry alitembelea hospitalini na kumpeleka Jenny kwenye miadi. Jenny alikiri, “nadhani nilitapika mara nyingi ndani ya gari yake.”

Bila kujali ugonjwa wake Jenny aliendele kutumikia kwa ujasiri kama rais wa kata wa Muungano wa Usaidizi wa Kina Mama. Hata katika wakati mgumu, alipiga simu, alituma ujumbe mfupi na barua pepe akiwa kitandani kwake, na aliwaalika kina dada waje kumuona. Alituma kadi na barua kwa watu, akiwapenda dada zake kutoka mbali. Wakati Kata yake ilipoomba picha ya urais wake kwa ajili ya historia ya kata, hiki ndicho walichopata. Kwa sababu Jenny mwenyewe ni mwanamke shupavu , aliwaalika wote kushiriki mizigo ya wengine, ikiwemo wa kwake mwenyewe.

Picha
Urais wa kata wa Muungano wa Usaidizi wa Kina Mama ukiwa umevalia kofia

Kama mwanamke shupavu Jenny alishuhudia: “Sio tu kwamba tuko hapa kuokoa wengine bali kujiokoa sisi wenyewe. Na wokovu huo huja kwa kuwa washirika na Yesu Kristo; kwa kuelewa neema Yake na Upatanisho Wake na hisia Zake za upendo kwa wanawake wa Kanisa. Hilo hutokea kupitia vitu vidogo kama kumchana mtu nywele; kutuma barua yenye ujumbe wa ufunuo wenye uvuvio, wa wazi wa tumaini na neema, au kuruhusu wanawake watutumikie.”9

Akina dada tunapokuwa tumevurugwa, wenye shaka, tumekata tamaa, tumetenda dhambi, wenye huzuni au kuzidiwa kinafsi, hebu tukubali mwaliko wa Mwokozi wa kunywa maji yaliyo hai kama alivyofanya mwanamke shupavu pale kisimani, tukiwaalika wengine kufanya vivyo hivyo tunapotoa ushahidi wetu wa uhakika : “Huyu siye Kristo?”

Wakati maisha yanapoonekana si sawa, kama ambavyo ingeonekana kwa Martha kwenye msiba wa kaka yake—tunapopitia maumivu ya moyo ya upweke, ugumba, kupoteza wapendwa wetu, kupoteza nafasi tulizokosa za kuolewa na familia, mifarakano, kukata tama, msongo wa mawazo, ugonjwa wa mwili au akili, kuonewa, mfadhaiko, wasiwasi, uraibu, ugumu wa pesa au mengine kama hayo—hebu tumkumbuke Martha na tutangaze ushahidi wetu wa hakika : “Lakini najua  …[na] nasadiki ya kwamba wewe ndiwe Kristo, Mwana wa Mungu.

Picha
Wanawake kote

Hebu tukumbuke wanawake shupavu wengi ambao wamekataa kumuacha Mwokozi wetu mwenye thamani wakati wa uzoefu wa mateso alipoteseka msalabani na baadae walipata fursa ya kuwa mashahidi wa kwanza wa uhakika wa Ufufuko Wake wa utukufu. Hebu tukutwe tupo karibu naye katika sala na kusoma maandiko. Acha tusogee karibu nae kwa kujiandaa na kupokea ishara takatifu ya upatanisho Wake kila wiki wakati wa ibada ya sakramenti na tunapotunza maagano kwa kuwatumikia wengine wakati wanapokuwa na uhitaji. Labda hivyo tutakuwa sehemu ya wanawake shupavu wafuasi wa Yesu Kristo,  ambao watasherehekea kurudi kwake kwa utukufu wakati atakaporudi tena.

Picha
Mwokozi katika Ujio wa Pili

Kina dada, ninashuhudia juu ya Wazazi wa Mbinguni wenye upendo; juu ya Mwokozi wetu, Yesu Kristo; na juu ya Upatanisho Wake usio na mwisho kwa niaba yetu. Ninajua Nabii Joseph Smith alitawazwa toka mwanzo kama nabii wa Urejesho. Ninajua Kitabu cha Mormoni ni cha kweli na kilitafsiriwa kwa uweza wa Mungu. Tumebarikiwa kwa nabii anayeishi katika siku zetu wenyewe, Rais Thomas S. Monson. Kwa kweli hizi nina uhakika! Katika jina la Yesu Kristo, amina.

Muhtasari: Mnamo Aprili 1, 2017, Dada Esplin alipumzishwa kama mshauri wa kwanza katika urais mkuu wa Msingi.