2010–2019
Kuwa na Imani na Mungu Bila Kuyumba
Aprili 2017


Kuwa na Imani na Mungu Bila Kuyumba

Kama tutakuwa thabiti na hatuna shaka katika imani yetu, Bwana ataongeza uwezo wetu wa kujiinua juu ya changamoto za maisha.

Wapendwa akina kaka na akina dada, nataka kuanza ujumbe wangu leo kwa kushuhudia kwamba najua kwamba Rais Thomas S. Monson ni nabii wa Mungu katika siku yetu leo. Washauri wake katika Urais wa Kwanza na Mitume Kumi na Wawili nao pia kwa kweli, ni manabii, waonaji, na wafunuaji. Wanamwakilisha Bwana Yesu Kristo na wana haki kutangaza nia na mapenzi Yake kama yanavyofunuliwa kwao. Ninashuhudia kwamba kuna usalama katika kufuata ushauri wao. Bwana anawatia moyo kusisitizia kuimarisha imani yetu kwa Baba yetu wa Mbinguni na Mwanae, Yesu Kristo, na upatanisho Wake ili kwamba tusije tukayumba wakati tunapokabiliana na changamoto za siku zetu.

Katika Kitabu cha Mormoni tunasoma kuhusu mtu alieitwa Amoni aliyetumwa kutoka nchi ya Zarahemla kwenda nchi ya Lehi-Nephi kuuliza kuhusu ndugu zake. Pale aliwakuta Mfalme Limhi na watu wake, waliokuwa utumwani chini ya Walamani. Mfalme Limhi alitiwa moyo na mambo ambayo Amoni alishiriki kuhusu watu wake katika Zarahemla. Moyo wa Mfalme Limhi ulijawa na matumaini makubwa mno na furaha kwamba alikusanya watu wake kwenye hekalu na kusema:

“Kwa hiyo, inueni vichwa vyenu, na mshangilie, na wekeni imani yenu katika Mungu. 

“… Kama mtamrudia Bwana kwa moyo wa lengo moja, … na kumwamini, na kumtumikia kwa bidii yote akilini, … yeye atawaokoa, kutoka utumwani, kulingana na nia yake na mapenzi yake.”1

Imani ya watu wa Mfalme Limhi iliathirika kwa undani sana kwa maneno ya Amoni kiasi kwamba waliweka agano kwa Mungu kumhudumia na kutii amri Zake, bila kujali hali yao ngumu. Kwa sababu ya imani yao, walikuwa na uwezo wa kubuni , mpango  wa kutoroka kutoka mikono mwa Walamani.2

Kina kaka na kina dada, tafadhali fikirieni umuhimu wa mwaliko wa Mfalme Limhi alioutoa kwa watu wake na uhusiano wake kwetu. Alisema “Inueni vichwa vyenu, na mshangilie, na wekeni imani yenu katika Mungu.” Kwa maneno haya, Limhi aliwaalika watu wake kuangalia siku za usoni kupitia macho ya imani; kubadili woga wao na kuwa na matumaini mema yanayokuja kama matokeo ya kuwa na imani; na kutoyumba katika kuweka imani yao katika Mungu bila kujali hali ya mambo.

Maisha ya duniani ni muda wa kujaribiwa ambako tutathibitishwa kuona kama tutafanya vitu vyote ambavyo Bwana Mungu wetu atatuamuru.3 Hii itahitaji imani isiyoyumba katika Kristo hata katika muda wa matatizo makubwa. Itahitaji kwamba tutasonga mbele na imani thabiti katika Kristo, tukiongozwa na Roho, na kutumaini kwamba Mungu atakidhi mahitaji yetu.4

Katika hitimisho la huduma Yake ya kidunia, punde kabla hajachukuliwa mfungwa, Mwokozi aliwafundisha wafuasi Wake: “Ulimwenguni mtapata dhiki; lakini jipeni moyo; mimi nimeushinda ulimwengu.”5

Tafakarini pamoja na mimi kwa muda mfupi—Yesu Kristo, Mwana Pekee wa Mungu, aliishi maisha yasiyo na dhambi na alishinda majaribu yote, maumivu, changamoto, na mateso ya ulimwengu. Alitokwa na matone ya damu Gethsemane; Aliteseka maumivu makali yasiyoelezeka. Alijichukulia juu Yake mwenyewe maumivu na magonjwa yetu. Yuko tayari kusaidia—kumsaidia kila mmoja wetu—kwa kila mzigo Kupitia maisha Yake, mateso, kifo na Ufufuko, aliondoa kila kizuizi cha shangwe yetu na kupata amani kwenye dunia hii. Faida za dhabihu Yake ya upatanisho zimetolewa kwa wale wanaomkubali na kujinyima wenyewe na kwa wale wanaojitwika msalaba Wake na kumfuataYeye kama wafuasi Wake wa kweli.6 Kwa hiyo, tunapofanya imani katika Yesu Kristo na Upatanisho Wake, tutaimarishwa, mizigo yetu itapunguzwa , na kupitia Yeye tutaushinda ulimwengu.

Akina Kaka na akina dada, tunapotafakari kuhusu nguvu na tumaini ambalo tunaweza kupokea kutoka kwa Mwokozi, tuna sababu ya kuinua vichwa vyetu na kushangilia, kuweka imani yetu katika Mungu na kusonga mbele bila kuyumba, “maana mwenye shaka ni kama wimbi la bahari lililochukuliwa na upepo, na kupeperushwa huku na huku. … Mtu wa nia mbili husita-sita katika njia zake zote.”7

Mfalme Limhi vilevile alisisitiza,“mwamini, na kumtumikia kwa bidii yote ya akilini, kama mtafanya hivi, yeye atawaokoa, kutoka utumwani, kulingana na nia yake na mapenzi yake.”8

Sikiliza maneno ya Mwokozi mwenyewe wakati anapotusihi sisi:

“Msifadhaike mioyoni mwenu; mnamwamini Mungu, niaminini na mimi. 

“Mkinipenda, mtazishika amri zangu. …

“Yeye aliye na amri zangu, na kuzishika, yeye ndiye anipendaye; naye anipendaye atapendwa na Baba yangu; nami nitampenda na kujidhihirisha kwake.”9

Mungu anatubariki kulingana na imani yetu.10 Imani ni chanzo cha kuishi na azma takatifu na taswira ya milele. Imani ni kanuni ya utendaji ambayo inahimiza bidii. Ni nguvu muhimu, nguvu hai dhahiri katika mtizamo wetu chanya na tamaa ya hiari kufanya kila kitu ambacho Mungu na Yesu Kristo wanatutaka tufanye. Inatusababisha sisi kupinga magoti na kumwomba sana Bwana kwa uongozi na kuinuka, na kufanya kwa matumaini kutimiza vitu thabiti vinavyolingana na mapenzi Yake.

Miaka mingi iliyopita wakati nikihudumu kama rais wa misheni, nilipokea simu kutoka kwa wazazi wa mmoja wapo wa Wamisionari wetu wapendwa ikinifahamisha kuhusu kifo cha dada yake. Nakumbuka, katika wakati ule maalumu, mmisionari yule na mimi tulijadili mpango wa wokovu wa ajabu wa Mungu kwa ajili ya watoto Wake na jinsi uelewa huu ungempa faraja.

Ingawa alistushwa na kuhuzunishwa na dhiki hiyo, mmisionari huyu—kupitia machozi yake na pamoja na imani katika Mungu—alishangilia katika maisha ya dada yake. Alionyesha imani isiyoyumba katika huruma laini ya Bwana. Kwa ushupavu, aliniambia kwamba angeendelea kuhudumu misheni yake kwa imani na bidii yote ili aweze kuwa anayestahili ahadi ambazo Mungu alikuwa nazo kwa ajili yake na familia yake Katika wakati huu wa shida, mmisionari yule mwaminifu alimgeuzia Mungu moyo wake, aliweka imani yake yote Kwake, na akaweka upya msimamo wake kumhudumia Bwana kwa imani na bidii yote.

Kina kaka na kina dada, kama hatuna imani thabiti katika Mungu na hamu ya kumtumikia, uzoefu wa maumivu ya maisha unaweza kutuelekeza tuhisi kama vile tuna mzigo tuliobebeshwa na nira nzito;na tunaweza kupoteza motisha kuishi injili kikamilifu. Bila imani, tutaishia kupoteza uwezo wa kufurahia mipango hiyo ya Mungu wetu kuhusu vitu ambavyo vitatokea baadaye katika maisha yetu.11

Katika nyakati hizi za majaribu, adui—ambaye wakati wote yuko macho—anajaribu kutumia mantiki yetu na hoja dhidi yetu. Anajaribu kutushawishi kwamba haina maana kuishi kanuni za injili. Tafadhali kumbukeni kwamba mantiki ya mwanadamu wa tabia ya asili “hayapokei mambo ya Roho wa Mungu; maana kwake huyo ni upuzi.”12 Kumbuka kwamba Shetani “ni adui wa Mungu, na hupigana dhidi yake siku zote, na hukaribisha na hushawishi kufanya dhambi, na kufanya kile kilicho kiovu siku zote.”13 Sisi sharti tusimruhusu kutudanganya; kwani tutakapofanya hivyo, tunajikwaa katika imani yetu na kupoteza uwezo kupata baraka za Mungu na nguvu.

Kama tupokuwa thabiti na hatuna shaka katika imani yetu, Bwana ataongeza uwezo wetu wa kujiinua juu ya changamoto za maisha. Tutawezeshwa kuthibiti shauku hasi na tutajenga uwezo wa kushinda, hata kile kinachoonekana kuwa, kizuizi kikali. Hiki ndicho kilichowawezesha watu wa Mfalme Limhi kufanya utorokaji wa kustaajabisha kutoka utumwani wao chini wa Walamani

Kina kaka na kina dada, ninawaalikeni kuweka imani yenu yote katika Mungu na katika mafundisho ya manabii Wake. Ninawaalikeni mfanye upya maagano yenu na Mungu, kumhudumu kwa moyo wenu wote, bila kujali ugumu wa hali za maisha yenu. Ninashuhudia kwamba kwa uwezo wa imani yenu isiyoyumba katika Kristo, mtakuwa huru na utumwa wa dhambi, shaka, kutoamini, huzuni, kuteseka; na mtapokea baraka zote zilizoahidiwa kutoka kwa Baba yetu wa Mbinguni mwenye upendo.

Nashuhudia kwamba Mungu ni halisi. Yeye yu Hai. Anatupenda. Yeye husikia maombi yetu katika wakati wetu wa furaha na katika wakati wetu wa shaka, huzuni, na kukata tamaa. Nashuhudia kwamba Yesu Kristo ni Mwokozi wa ulimwengu. Yeye ni Mkombozi.

Ninafunga hutoba yangu leo kwa maneno ya wimbo “Siyo Sasa Bali katika Miaka Ijayo,” unaopatikana katika nyimbo za Kireno.

Kama mawingu badala ya jua yanatandaza vivuli juu ya moyo wetu,

Kama maumivu yanatutesa, usijali; hivi karibuni tutajua wewe ni Nani.

Yesu anatuongoza kwa mkono Wake, na Yeye atatuambia kwa nini;

Kama tutasikiliza sauti yake, Yeye atatuambia kidogo kidogo.

Kuweni na imani katika Mungu bila kuyumba, na acheni Yeye atuidhinishe;

Imbeni utukufu Wake bila kikomo, kwani baadaye Yeye ataeleza.14

Nasema mambo haya katika jina takatifu la Yesu Kristo, amina.