Maandiko Matakatifu
2 Nefi 28


Mlango wa 28

Makanisa mengi ya bandia yatajengwa katika siku za mwisho—Yatafundisha mafundisho ya uwongo, yasiyofaidi, na ya kipumbavu—Ukengeufu utaendelea kwa sababu ya walimu wa bandia—Ibilisi atavuma katika mioyo ya wanadamu—Atafundisha kila aina ya mafundisho ya uwongo. Karibia mwaka 559–545 K.K.

1 Na sasa, tazameni, ndugu zangu, nimewazungumzia, kulingana na vile Roho ameniongoza; kwa hivyo, najua kwamba kwa kweli lazima yatimizwe.

2 Na vitu ambavyo vitaandikwa kutoka kwenye akitabu hicho vitakuwa vya bdhamana kuu kwa watoto wa watu, na hasa kwa uzao wetu, ambayo ni baki la nyumba ya Israeli.

3 Kwani itakuwa kwamba katika siku ile amakanisa ambayo yamejengwa, na siyo kwa Bwana, wakati mmoja italiambia nyingine: Tazama, Mimi, Mimi ni wa Bwana; na jingine litasema: Mimi, Mimi ni wa Bwana; na kila mmoja aliyejenga makanisa, yasiyo ya Bwana atasema hivyo—

4 Na watabishana mmoja na mwingine; na makuhani wao watabishana mmoja na mwingine, na watafundisha kulingana na aelimu yao, na watamkana Roho Mtakatifu, anayetoa maneno.

5 Na awanakana bnguvu za Mungu, yule Mtakatifu wa Israeli; na kuwaambia watu: Tusikilizeni sisi, na sikiliza mawaidha yetu; kwani tazama chakuna Mungu leo, kwani Bwana na Mkombozi ametenda kazi yake, na amewapatia wanadamu uwezo wake;

6 Tazameni, sikilizeni mawaidha yangu; kama watasema kuna muujiza uliotendwa kwa mkono wa Bwana, msiamini; kwani leo yeye sio Mungu wa amiujiza; ametenda kazi yake.

7 Ndiyo, na kutakuwa na wengi ambao watasema: aKuleni, kunyweni, na mshangilie, kwani kesho tutakufa; na sisi tutakuwa salama.

8 Na kutakuwa pia na wengi ambao watasema: Kuleni, kunyweni na mshangilie; walakini, mwogopeni Mungu—aataturuhusu kutenda dhambi kidogo; ndiyo, bdanganya kidogo, tumieni wengine kwa sababu ya maneno yao, mchimbie jirani yako cshimo; hakuna hatia kwa haya; na mtende vitu hivi vyote, kwani kesho tutakufa, na kama tutakuwa na hatia, Mungu atatuadhibu kwa mijeledi michache, na mwishowe tutaokolewa katika ufalme wa Mungu.

9 Ndiyo, na kutakuwa na wengi watakaofundisha kwa namna hii, uwongo na yasiyofaa na amafundisho ya bkipumbavu, na watajifurisha mioyoni mwao, na watajitahidi kumfichia Bwana mashauri yao; na matendo yao yatakuwa gizani.

10 Na adamu ya watakatifu italia kutoka chini dhidi yao.

11 Ndiyo, wote wamepotea anjia; bwameharibika.

12 Kwa sababu ya akiburi, na kwa sababu ya walimu bandia, na mafundisho ya bandia, makanisa yao yameharibika, na makanisa yao yamejiinua; kwa sababu ya kiburi yamefura.

13 aWanawapora bmaskini kwa sababu ya makutaniko yao mazuri; wanawapora maskini kwa sababu ya mavazi yao mazuri; na kuwatesa walio wapole na maskini katika moyo, kwa sababu katika ckiburi chao wamefura.

14 aWanakaza shingo zao na kufanya vichwa vyao kuwa na kiburi; ndiyo, na kwa sababu ya kiburi, na uovu, na machukizo, na uasherati, wote bwamepotea ila tu wachache, ambao ni wafuasi wanyenyekevu wa Kristo; walakini, wanaongozwa, na inakuwa kwamba katika wakati mwingi wanakosea kwa sababu wanafundishwa kwa mawaidha ya wanadamu.

15 Ee wenye ahekima, na walioelimika, na matajiri, ambao wanajivuna kwa bkiburi cha roho zao, na wale wote wanaofundisha mafundisho ya bandia, na wale wote wanaofanya uasherati, na kupindua njia zilizo sawa za Bwana, cole, ole, ole ni kwao, asema Bwana Mungu Mwenyezi, kwani watatupwa jehanamu!

16 Ole kwa wale awanaokataa la haki kwa kitu kisichofaa na kushutumu kilicho chema, na kusema kwamba hakina thamani! Kwani siku inafika ambapo Bwana Mungu ataadhibu wakazi wa dunia kwa haraka; na katika siku ile ambayo watakuwa wameiva bkabisa katika maovu wataangamia.

17 Lakini tazama, kama wakazi wa dunia watatubu uovu wao na machukizo hawataangamizwa, asema Bwana wa Majeshi.

18 Lakini tazama, kanisa lile kuu la machukizo, yule akahaba wa ulimwengu wote, lazima baporomoke duniani, na kubwa utakuwa muanguko wake.

19 Kwani ufalme wa ibilisi lazima autetemeke, na wale ambao ni wake lazima wavurugwe hadi watubu, au bibilisi atawafunga kwa cminyororo yake isiyo na mwisho, na wavurugwe, kwa hasira na waangamie.

20 Kwani tazama, katika siku ile aatavuma mioyoni mwa watoto wa watu, na awavuruge wakasirikie yale ambayo ni mema.

21 Na wengine aatawapatanisha, na awapatie usalama wa kimwili, kwamba watasema: Yote yako salama Sayuni; ndiyo, Sayuni inafanikiwa, yote ni mema—na hivyo bibilisi anadanganya roho zao, na kuwapeleka kwa makini hadi jehanamu.

22 Na tazama, wengine atawadanganya, na kuwaambia kwamba hakuna ajehanamu; na kuwaambia: Mimi sio ibilisi, kwani hakuna yeyote—na anawanongʼonezea hivyo masikioni mwao, hadi awashike na bminyororo yake miovu, kutoka ambapo hakuna ukombozi.

23 Ndiyo, wamefungwa na mauti, na jehanamu; na mauti, na jehanamu, na ibilisi, na wale wote ambao wameshikwa na hao lazima watasimama mbele ya kiti cha enzi cha Mungu, na awahukumiwe kulingana na matendo yao, na kutoka hapo lazima waende mahali walipotayarishiwa, hata kwenye bziwa la moto na kiberiti, ambayo ni mateso yasiyo na mwisho.

24 Kwa hivyo, ole kwa yule anayestarehe Sayuni!

25 Ole kwa yule anayetangaza: Yote yako salama!

26 Ndiyo, ole kwa yule aanayetii mawaidha ya wanadamu, na kukana nguvu za Mungu, na kipawa cha Roho Mtakatifu!

27 Ndiyo, ole kwa yule anayesema: Tumepokea, na ahatuhitaji zaidi!

28 Na mwishowe, ole kwa wale wote wanaotetemeka, na awanakasirika kwa sababu ya ukweli wa Mungu! Kwani tazama, yule ambaye amejengwa katika bmwamba huyapokea kwa furaha; na yule aliyejengwa kwenye msingi wa mchanga hutetemeka asije akaanguka.

29 Ole kwa yule atakayesema: Tumepokea neno la Mungu, na ahatuhitaji bmengine zaidi ya maneno ya Mungu, kwani tuna ya kutosha!

30 Kwani tazama, hivyo ndivyo asemavyo Bwana Mungu: Nitawapatia watoto wa watu mstari juu ya mstari, aamri juu ya amri, hapa kidogo na pale kidogo; na heri wale wanaosikiliza kanuni zangu, na kutegea sikio mashauri yangu, kwani watajifunza bhekima; kwani kwa yule ambaye chupokea nitampatia dzaidi; na kutoka kwa wale watakaosema, Tuna ya kutosha, watapokonywa hata kile walichonacho.

31 Amelaaniwa yule ambaye anaweka aimani yake kwa mwanadamu, au amfanyaye kuwa mkono wake, au kusikiliza kanuni za wanadamu, isipokuwa kanuni zao zitolewe na nguvu ya Roho Mtakatifu.

32 aOle kwa Wayunani, asema Bwana Mungu wa Majeshi! Ingawa nitawanyoshea bmkono wangu siku kwa siku, watanikana; walakini, nitawarehemu, asema Bwana Mungu, kama watatubu na kunijia mimi; kwani mkono wangu umenyooshwa siku yote, asema Bwana Mungu wa Majeshi.