Rafiki
Kumfuata Yesu huko Thailand
Januari 2024


“Kumfuta Yesu huko Thailand,” Rafiki, Jan. 2024, 6–7.

Kumfuata Yesu huko Thailand

Kutana na Panya

Picha
alt text

Jinsi Panya Anavyomfuata Yesu

Panya anamwalika binamu yake aende kanisani pamoja naye. Binamu anapokuja, Panya anamsaidia ahisi kukaribishwa. Anamsaidia akutane na watoto wengine katika Msingi na kupata marafiki.

Nyumbani, Panya anasaidia kwa kusafisha chombo cha chakula na viatu vyake. “Ninaburudika wakati ninaposaidia,” Panya anasema. Anaishi na shangazi na bibi yake na anapenda kuwasaidia. Pia hukunja blanketi lake kila asubuhi.

Mama yake Panya amefariki karibuni. Wakati Panya anapomkumbuka mama yake, shangazi yake humsaidia asali kwa Baba wa Mbinguni. Anahisi kupendwa baada ya kusali. “Ninaposali, ninahisi kama vile Yesu yupo nami,” anasema.

Picha
alt text

Panya akiwa na bibi na shangazi yake.

Kuhusu Panya

Picha
alt text

Umri Miaka: 7

Anatokea: Nonthaburi, Thailand

Lugha: Kithai

Lengo: Kuwa mbunifu wa ndani na kupamba vyumba katika nyumba na majengo.

Mambo ya kupitisha muda: Dansi, kuendesha baiskeli, kujifunza kinanda, kuogelea, kusoma na taekwondo

Familia: Panya, shangazi na bibi

Mambo Ayapendayo Panya

Hadithi za Yesu: Wakati alipobatizwa (ona Mathayo 3:13–17)

Mapumziko au utamaduni wa familia: Krismasi na safari za familia

Tunda na mboga: zabibu za kijani na matango

Rangi: Zambarau

Wimbo wa Msingi: “I Love to See the Temple” (Kitabu cha Nyimbo za Watoto, 95)

Picha
PDF ya hadithi