Rafiki
Nini kipo Akilini Mwako?
Januari 2024


“Nini kipo Akilini Mwako?” Rafiki, Januari 2024, 42.

Nini kipo Akilini Mwako?

Ninapoweka malengo, ninaishia kuyasahau. Je ni kwa namna gani ninafikia malengo yangu?

—Kufikia malengo huko Reykjavík

Mpendwa unayetaka kufikia malengo,

Usihofu: linapokuja suala la kuweka na kusahau malengo, hauko peke yako. Hili ni jambo ambalo watu wengi wanapambana nalo. Sisi sote tuko vizuri kwenye kuweka malengo. Hata hivyo kuyafikia malengo hayo—hicho ndicho kipengele kigumu. Hapa kuna baadhi ya mawazo ya kusaidia!

Kwa upendo,

Gazeti la Rafiki

  1. Kuwa na ndoto kubwa lakini anza kidogo kidogo. Ni vizuri kujipa changamoto. Lakini kumbuka kwamba malengo madogo madogo yana nguvu pia. “Kupitia vitu vilivyo vidogo na rahisi vitu vikubwa hutendeka” (Alma 37:6)

  2. Weka malengo mahususi. “Nitasaidia nyumbani.” Hili ni lengo lililo SAWA, lakini halieleweki kwa ufasaha. “Nitasaidia nyumbani kwa kupanga vitu vyangu kila siku.” Hili ni lengo zuri sana. Ni mahususi. Ni mpango.

  3. Shiriki lengo lako. Zungumza na mzazi , mwalimu au rafiki kuhusu lengo lako. Waombe wakusaidie. Nyakati zingine kuwa na mtu wa kukufuatilia na kukupongeza tu ni hamasa unayohitaji.

  4. Tengeneza vitu vya kukukumbusha. Ikiwa unataka kukumbuka malengo yako, yaandike. Weka nakala ya malengo yako mahala ambapo utayaona kila siku. Yawekee rangi na ubunifu!

  5. Kuwa na imani. “Tunapaswa kuwa na imani katika Mungu,” alisema Rais M. Russell Ballard. “Tunapaswa kuwa na imani katika Bwana Yesu Kristo. Na ee, jinsi gani kwa kiasi kikubwa tunapaswa kuwa na imani kwetu sisi wenyewe.”* Unaweza! Mungu atasaidia.

Picha
Alt text

Kielelezo na Shawna J. C. Tenney

  • “Fanya Mambo Yanayoleta Utofauti,” Ensign, Juni 1983, 71.