2010–2019
Kuwa Watakatifu wa Siku za Mwisho Wenye Kuonyesha Mifano Bora
Oktoba 2018


Kuwa Watakatifu wa Siku za Mwisho Wenye Kuonyesha Mifano Bora

Ninawaachieni upendo na baraka zangu juu yenu,Ili muweze kusherehekea neno la Bwana na kutenda mafundisho Yake maishani mwenu.

Huu umekuwa ni mkutano wenye kutia msukumo na wa kihistoria. Tunatazama mbele kwa shauku. Tumetiwa msukumo kufanya vizuri zaidi na kuwa wazuri zaidi. Jumbe za ajabu zilizotolewa kutoka kwenye mimbari hii na Viongozi wetu Wakuu wenye Mamlaka na Maafisa Wakuu na muziki vimekuwa adhimu! Ninawaomba msome jumbe hizi, kuanzia wiki hii.1 Zinaonyesha nia na mapenzi ya Bwana kwa ajili ya watu Wake, leo.

Mtaala mpya unaolenga nyumbani, unaosaidiwa na Kanisa na uliofanywa sawa una uwezo wa kufungulia nguvu za familia, pale kila familia inapofuatilia kwa makini na uangalifu ili kubadilisha nyumba zao kuwa kimbilio la imani. Ninakuahidi ya kwamba utakapofanya bidii kupanga upya nyumba yako kuwa kituo cha kujifunza injili, baada ya muda Siku zako za Sabato zitakuwa takatifu sana. Watoto Wako watafurahia kujifunza na kuishi mafunzo ya Mwokozi, na ushawishi wa adui katika maisha yako na nyumbani kwako utapungua. Mabadiliko katika familia yako yatakuwa ya ajabu na ya kudumu.

Katika mkutano huu tumeimarisha nia yetu ya kufanya juhudi muhimu za kumheshimu Bwana Yesu Kristo kila wakati tunapozungumzia Kanisa Lake. Ninawaahidi kwamba uangalifu wetu wa dhati katika matumizi sahihi ya jina la Kanisa la Mwokozi na waumini wake utapelekea kuwepo kwa ongezeko la imani na kupatikana kwa nguvu zaidi za kiroho kwa waumini wa Kanisa Lake.

Sasa hebu tuzungumzie mada ya mahekalu. Tunajua ya kwamba muda wetu katika hekalu ni muhimu kwa wokovu na kuinuliwa kwetu pamoja na wokovu na kuinuliwa kwa familia zetu.

Baada ya kupokea ibada zetu za hekaluni na kufanya maagano matakatifu na Mungu, kila mmoja wetu anahitaji kuimarishwa kiroho kunakoendelea na kufundishwa ambako kunawezekana tu katika nyumba ya Bwana. Na mababu zetu wanatuhitaji kuhudumu kama mawakala wao.

Fikiria rehema kuu na usawa wa Mungu, ambaye, kabla ya misingi ya ulimwengu, aliweka njia ya kutoa baraka za hekaluni kwa wale ambao walifariki bila ufahamu wa injili. Ibada hizi takatifu za hekalu ni za kale. Kwangu mimi mambo haya ya kale ni ya kusisimua na ushuhuda mwingine wa uhalisia wake.2

Akina kaka na dada zangu wapendwa, mashambulizi ya adui yanaongezeka kwa kasi, kwa ukali na namna nyingi.3 Hitaji letu la kuwa hekaluni mara kwa mara halijawahi kuwa kubwa kiasi hiki. Ninawasihi mtazame kwa sala jinsi mnavyotumia muda wenu. Wekeza muda katika siku zako zijazo na zile za familia yako. Ikiwa unaweza kufika hekaluni, ninakusihi utafute njia ya kuweka ahadi ya mara kwa mara na Bwana—kuwa katika nyumba Yake takatifu—na kisha tunza ahadi hiyo bila ya kuchelewa na kwa shangwe. Ninawaahidi kwamba Bwana ataleta miujiza anayojua mnahitaji mnapofanya dhabihu ya kuhudumu na kuabudu hekaluni Mwake.

Kwa sasa tunayo mahekalu 159 yaliyowekwa wakfu. Uangalizi mzuri na utunzaji wa mahekalu hayo ni muhimu sana kwetu. Muda unapokuwa umepita, mahekalu lazima yatahitaji kufanywa upya na kutengenezwa. Kwa kusudi hilo, mipango sasa inafanywa kurekebisha na kufanya upya Hekalu la Salt Lake na mahekalu mengine ya kizazi cha waanzilishi. Maelezo ya miradi hii yatatolewa pale yatakapofafanuliwa.

Leo tunafurahia kutangaza mipango ya kujenga mahekalu 12 zaidi. Mahekalu hayo tyatajengwa katika maeneo yafuatayo: Mendoza, Argentina; Salvador, Brazil; Yuba City, California; Phnom Penh, Cambodia; Praia, Cape Verde; Yigo, Guam; Puebla, Mexico; Auckland, New Zealand; Lagos, Nigeria; Davao, Philippines; San Juan, Puerto Rico; na Washington County, Utah.

Ujenzi na utunzaji mahekalu vinaweza visibadilishe maisha yako, lakini kutumia muda hekaluni bila shaka kutafanya hivyo. Kwa wale ambao hawajafika hekaluni kwa kipindi kirefu, ninawahimiza mjitayarishe na kurudi haraka iwezekanavyo. Kisha ninawaalika kuabudu hekaluni na kusali kuhisi kwa dhati upendo wa Mwokozi usio na kifani kwa ajili yenu, kwamba kila mmoja wenu aweze kupata ushuhuda wake mwenyewe kwamba Mwokozi anaongoza kazi hii takatifu na ya milele.4

Akina kaka na akina dada, ninawashukuru kwa imani yenu na juhudi zenu za kuidhinisha. Ninawaachieni upendo na baraka zangu juu yenu,Ili muweze kusherehekea neno la Bwana na kutenda mafundisho Yake maishani mwenu. Ninawahakikishia ya kwamba ufunuo unaendelea Kanisani na utaendelea hadi “malengo ya Mungu yatakapotimizwa, na Yehova Mkuu atasema kazi imekamilika.”5

Ninawabariki kwa ongezeko la imani ndani Yake na kazi Yake takatifu, kwa imani na subira kuvumilia changamoto binafsi katika maisha. Ninawabariki muwe Watakatifu wa Siku za Mwisho Wenye Kuonyesha Mifano Bora. Ninawabariki hivyo na kutoa ushuhuda wangu kwamba Mungu yu hai! Yesu ndiye Kristo! Hili ni Kanisa Lake. Sisi ni watu Wake, katika jina la Yesu Kristo, amina.

Muhtasari

  1. Ona jumbe za mkutano mkuu mtandaoni kwenye LDS.org katika Gospel Library app. Zitachapishwa katika Ensign na Liahona. Magazeti ya Kanisa, ikijumuisha New Era na Friend, yanayosambazwa kupitia sanduku la posta au kupakuliwa kutoka mtandaoni, ni sehemu muhimu ya mtalaa wako wa ijili unaolenga nyumbani.

  2. Ona, kwa mfano, Kutoka 28; 29; Mambo ya Walawi 8.

  3. Ona Mosia 4:29.

  4. Ona Wilford Woodruff, “Sheria ya Kuwa Wana,” mahubiri yaliyotolewa katika mkutano mkuu wa Kanisa, Apr. 8, 1894. Rais Woodruff alisema: “Hatujamaliza kupokea ufunuo. Hatujamaliza kazi ya Mungu. … Hakutakuwa na mwisho kwa kazi hii hadi ikamilishwe” (Deseret Evening News, Apr. 14, 1894, 9).

  5. Mafundisho ya Marais wa Kanisa: Joseph Smith (2007), 142.