2010–2019
Maneno ya Utangulizi
Oktoba 2018


Maneno ya Utangulizi

Sasa ni wakati wa Kanisa linalolenga Nyumbani, likisaidiwa na kile kinachotendeka ndani ya majumba ya matawi yetu, kata zetu na vigingi vyetu.

Ndugu na dada zangu wapendwa, tunatazamia kukusanyika pamoja nanyi tena katika huu mkutano mkuu wa Oktoba wa Kanisa. Tunawakaribisheni kila mmoja wenu kwa moyo mkunjufu. Tunashukuru sana kwa ajili ya sala zenu zenye kuhimili. Tunaweza kuhisi athari zake. Asanteni!.

Tunashukuru kwa ajili ya juhudi zenu katika kufuata ushauri uliotolewa miezi katika mkutano mkuu miezi sita iliyopita. Urais wa vigingi kote ulimwenguni umetafuta ufunuo unaohitajika kutengeneza upya akidi za wazee. Wanaume wa akidi hizi pamoja na kina dada waliojitolea wa Muungano wa Usaidizi wa Kina Mama kwa bidii wamewahudumia kaka na dada zao kwa njia ya juu zaidi, na takatifu. Tumeinuliwa na juhudi zenu za wema na za ajabu kuleta upendo wa Mwokozi kwa familia zenu, jirani zenu, na marafiki na kuwahudumia kama vile Yeye angewahudumia.

Tangu mkutano mkuu wa Aprili, Dada Nelson pamoja nami tumekutana na waumini kwenye mabara manne na kwenye visiwa ya bahari. Kutoka Yerusalemu hadi Harare, kutoka Winnipeg hadi Bangkok, tumeona imani yenu kuu na nguvu za shuhuda zenu.

Tumefuraishwa sana na idadi ya vijana wetu ambao wemejiunga na kikosi cha vijana cha Bwana kukusanya Israeli iliyotawanyika.1 Tunanawashukuru! Mnapoendelea kufuata mialiko yangu niliyotoa katika ibada ya vijana ulimwenguni kote, mnaweka viwango kwetu wote kufuata. Ni mafanikisho jinsi gani ninyi vijana mmefanya!

Katika miaka ya hivi karibuni, sisi katika mabaraza simamizi ya Kanisa tumehangaika sana na swala la kimsingi: Je, tunweza kupeleka vipi injili katika urahisi wake, na ibada zake kwa ufanisi wa milele, kwa watoto wote wa Mungu?

Kama Watakatifu wa Siku za Mwisho, tumezoea kufikiria “kanisa” kama kitu ambacho hutokea katika majumba yetu ya mikutano, kikisaidiwa na kile kinachotendeka nyumbani. Tunahitajika kufanya marekebisho kwenye huu mpangilio. Sasa ni wakati wa Kanisa linalolenga Nyumbani, likisaidiwa na kile kinachotendeka ndani ya majumba ya matawi yetu, kata zetu na vigingi vyetu.

Jinsi vile Kanisa linaendelea kupanuka kote ulimwenuni, waumini wengi wanaishi kule ambako hamna majumba ya ibada—na kuna uwezekano yasiwepo hivi karibuni. Nakumbuka familia ambayo, kwa sababu ya hali kama hiyo, walihitajika kukutana nyumbani kwao. Nilimuuliza mama jinsi alivyopendelea kwenda kanisa katika nyumba yake mwenyewe. Alijibu, “Mini ninapenda hivyo! Mume wangu hutumia lugha bora nyumbani sasa, akijua kwamba atabariki sakramenti hapa kila Jumapili.”

Kusudi la muda mrefu la Kanisa ni kuwasaidia waumini wote kuongeza imani yao katika Bwana wetu Yesu Kristo na Upatanisho Wake, kuwasaidia wao katika kufanya na kushika maagano yao na Mungu, na kuimarisha na kufunganisha familia zao. Katika hii dunia changamani, hili si rahisi. Adui anaongezea mashambulizi yake kwenye imani na juu yetu na familia zetu kwa kiwango kikubwa sana. Ili kunusurika kiroho, tunahitaji mikakati ya kukinza na mipango hai. Vuvyo hivyo, sisi sasa tunataka kufanya marekibisho ya kitaasisi ambayo itawaimarisha waumini wetu zaidi pamoja na familia zao.

Kwa miaka mingi, viongozi wa Kanisa wakekuwa wakifanyia kazi Mtalaa mseto wa kuimarisha familia na watu binfasi kupitia mpango wa kulenga-nyumbani na kusaidiwa na-Kanisa ili kujifunza mafundisho, kuimarisha imani, na kudumisha kuabudu binafsi. Juhudi zetu katika hii miaka ya hivi karibuni za kutasaka Sabato—zinafanya iwe furaha na ishara binafsi kwa Mungu ya upendo wetu Kwake—ikisaidiwa na marekebisho tunayoleta sasa.

Asubuhi hii tutatangaza mapatano mapya na muunganiko kati ya maelekezo ya injili nyumbani na Kanisani. Kila mmoja wetu hana jukumu kwa ukuaji wetu wa kiroho binafsi. Na maandiko ni wazi kwamba wazazi wana jukumu la kimsingi la kuwafundisha watoto wao mafundisho.2 Ni jukumu la Kanisa kumsaidia kila muumini katika hili lengo takatifu la kuongezea elimu ya injili mwenyewe.

Mzee Quentin L. Cook sasa ataelezea haya marekebisho muhimu. Washiriki wote wa Urais wa Kwanza na Akidi ya Mitume Kumi na Wawili wameungana katika kuunga mkono ujumbe huu. Kwa shukrani tanatambua mwongozo kutoka kwa Bwana ambao umeshawishi utengenezaji wa mipango na taratibu ambazo Mzee Cook atawasilisha.

Kina kaka na dada zangu wapendwa, mimi najua kwamba Mungu yu hai! Yesu ndiye Kristo! Hili ni Kanisa Lake, analoliongoza kwa unabii na ufunuo kupitia watumishi Wake wanyenyekevu. Mimi nashuhudia hivyo katika jina la Yesu Kristo, amina.