Mkutano Mkuu
Upendo wa Mungu
Mkutano Mkuu wa Oktoba 2021


Upendo wa Mungu

Baba yetu na Mkombozi wetu wametubariki kwa amri, na katika kutii amri Zao, tunahisi upendo Wao mkamilifu kwa utimilifu na kwa kiasi kikubwa zaidi.

Baba yetu wa Mbinguni anatupenda sote kwa dhati na kwa ukamilifu.1 Katika upendo Wake, Alitengeneza mpango, mpango wa ukombozi na furaha ili kufungua kwetu sisi sote fursa na furaha ambavyo tu radhi kuvipokea, mpaka na ikijumuisha vyote Alivyonavyo na alivyo.2 Ili kufikia haya, Alikuwa hata radhi kumtoa Mwanawe Mpendwa, Yesu Kristo, kama Mkombozi wetu. “Kwa maana jinsi hii Mungu aliupenda ulimwengu, hata akamtoa Mwanawe wa pekee, ili kila mtu amwaminiye asipotee, bali awe na uzima wa milele.”3 Yeye ni upendo halisi wa Baba—kwa wote, na bado binafsi kwa kila mmoja.

Yesu Kristo anashiriki na Baba upendo huu mkamilifu. Awali wakati Baba alipoelezea mpango Wake mkuu wa furaha, Alimwita mmoja kuwa kama Mwokozi ili kutukomboa sisi—sehemu muhimu ya mpango huu. Yesu alijitolea, “Niko hapa, nitume mimi.”4 Mwokozi “hafanyi chochote ila tu kwa manufaa ya ulimwengu; kwani anapenda ulimwengu, hata kwamba anatoa maisha yake ili awavute wanadamu wote kwake. Kwa hivyo, hamwamuru yeyote kwamba asipokee wokovu wake.”5

Upendo huu wa kiungu unapaswa kutupatia sisi faraja tele na kujiamini wakati tunapoomba kwa Baba katika jina la Kristo. Hakuna hata mmoja wetu ambaye ni mgeni Kwao. Hatuhitaji kusita kumlingana Mungu, hata wakati tunapohisi hatustahili. Tunaweza kutegemea katika huruma na sifa za Yesu Kristo ili kusikilizwa.6 Tunapokaa katika upendo wa Mungu, tunategemea kidogo sana kwenye uthibitisho wa wengine ili kutuongoza.

Upendo wa Mungu Hauruhusu dhambi; Bali hutoa Wokovu

Kwa sababu upendo wa Mungu haubagui, wengine huongelea kama usiokuwa na “masharti,” na katika mawazo yao, wanaweza kuweka wazo hilo kumaanisha kwamba baraka za Mungu hazina “masharti,” na kwamba wokovu hauna “masharti.” Si hivyo. Wengine wanapenda kusema, “Mwokozi ananipenda kama nilivyo,” na hakika hii ni kweli. Lakini hawezi kumpeleka mmoja wetu katika ufalme Wake kama tulivyo, “kwani hakuna kitu kichafu kinaweza kuishi kule, au kuishi katika uwepo wake.”7 Dhambi zetu kwanza lazima zisafishwe.

Profesa Hugh Nibley aliwahi kusema kwamba ufalme wa Mungu hauwezi kuwepo ikiwa utajihusisha hata na dhambi ndogo: “Doa dogo la rushwa linamaanisha kwamba ulimwengu mwingine usingekuwa wa kuharibika wala wa milele. Kasoro ndogo kwenye jengo, taasisi, kanuni au tabia vitathibitisha pasipo kupingwa kuwa vya kufisha katika umilele.”8 Amri za Mungu ni “madhubuti”9 kwa sababu ufalme Wake na watu wake wanaweza kusimama tu ikiwa wataendelea kukataa uovu na kuchagua mema, pasipo kubagua.10

Mzee Jeffrey R. Holland alisema, “Yesu alielewa kile ambacho wengi katika utamaduni wetu wa kisasa huonekana kusahau: kwamba kuna tofauti ya muhimu kati ya amri ya kusamehe dhambi (ambayo Anao uwezo usio na mwisho wa kufanya) na onyo dhidi ya kupuuza dhambi (kitu Ambacho Hakuwahi kufanya hata mara moja).”11

Bila kujali kutokamilika kwetu kwa sasa, hata hivyo, tunaweza kutumainia kupata “heshima na cheo,”12 sehemu, katika Kanisa Lake na katika ulimwengu wa selestia. Baada ya kuweka wazi kwamba Hawezi kusamehe au kufumbia macho dhambi, Bwana anatuhakikishia:

“Hata hivyo, yeye anayetubu na kutimiza amri za Bwana huyo atasamehewa.”13

“Na kila mara watu wangu watatubu, nitawasamehe makosa yao dhidi yangu.”14

Toba na neema ya kiungu huondoa mashaka:

“Na kumbuka pia maneno ambayo Amuleki alimzungumzia Zeezromu, katika mji wa Amoniha; kwani alimwambia kwamba Bwana lazima atakuja kuwakomboa watu wake, lakini kwamba hatakuja kuwakomboa katika dhambi zao, lakini kuwakomboa kutoka dhambi zao.

“Na ana uwezo aliopewa kutoka kwa Baba kuwakomboa kutoka kwa dhambi zao kwa sababu ya toba; kwa hivyo ametuma malaika wake kutangaza habari njema ya hali ya toba, ambayo inaleta uwezo wa Mkombozi, katika wokovu wa roho zao.”15

Kwa sharti la toba, Bwana anaweza kutoa rehema bila kuidhulumu haki na “Mungu huendelea kuwa Mungu.”16

Njia ya ulimwengu, kama ujuavyo, ni kinyume na Kristo au “chochote isipokuwa Kristo.” Siku zetu ni mchezo wa marudio wa Kitabu cha Mormoni ambapo watu wenye haiba huweka tawala zisizo za haki juu ya wengine, wakisherehekea uzinzi, na kuweka mbele ulimbikizaji wa mali kama msingi wa maisha yetu. Falsafa zao “huhalalisha katika kutenda dhambi ndogo”17 au hata dhambi nyingi, lakini hakuna hata mmoja awezaye kutoa wokovu. Wokovu huja kupitia damu ya mwanakondoo pekee. Kionekanacho chema cha “chochote isipokuwa Kristo” au “chochote isipokuwa toba” ambacho umati unaweza kutoa ni madai yasiyo na msingi kwamba hakuna dhambi, au kama ipo, hatima yake haina madhara. Sioni kama maelezo haya yanapata mvuto sana katika Hukumu ya Mwisho.18

Hatupaswi kufanya yasiyowezekana katika kujaribu kuhalalisha dhambi zetu. Na katika upande mwingine, hatuna haja ya kufanya yasiyowezekana katika kuondoa madhara ya dhambi kwa sifa zetu wenyewe. Dini yetu si ya uhalalishaji wala dini ya ukamilifu, bali dini ya ukombozi—ukombozi kupitia Yesu Kristo. Kama tu miongoni mwa wenye kujutia, kwa Upatanisho Wake dhambi zetu zetu zinagongelewa msalabani Kwake, na “kwa kupigwa kwake tunaponywa.”19

Upendo walionao Manabii Huendana na Upendo wa Mungu.

Nimefurahishwa kwa muda mrefu na, pia nimehisi, upendo wa kutamani wa manabii wa Mungu katika maonyo yao dhidi ya dhambi. Hawasukumwi na tamaa ya kulaani. Matamanio yao ya kweli huakisi upendo wa Mungu; kimsingi, ni ya upendo wa Mungu. Wanawapenda wale ambao wametumwa kwao, yeyote yule na chochote anachoweza kuwa. Kama alivyo Mwokozi, watumishi Wake hawapendi mtu yeyote apate maumivu ya dhambi na chaguzi zisizo sahihi.20

Alma alitumwa kutangaza ujumbe wa toba na ukombozi kwa watu wenye chuki waliokuwa tayari kuhukumu, kutesa, na hata kuua wanaoamini katika Ukristo, ikijumuisha Alma mwenyewe. Lakini bado aliwapenda na kutamani wokovu wao. Baada ya kutangaza Upatanisho wa Kristo kwa watu wa Amoniha, Alma aliomba: “Na sasa, ndugu zangu, natamani kutoka ndani ya kina cha moyo wangu, ndio, kwa wasiwasi mwingi na hata kwa uchungu, kwamba msikilize maneno yangu, na mtupe dhambi zenu, … Ili kwamba muweze kuinuliwa katika siku ya mwisho na kuingia katika pumziko la [Mungu].”21

Katika maneno ya Rais Russell M. Nelson, “ni kwa sababu kwa dhati tunajali kuhusu watoto wote wa Mungu kwamba tunatangaza ukweli Wake.”22

Mungu Anakupenda; Je Unampenda Yeye?

Upendo wa Baba na Mwana hutolewa bila gharama lakini pia huhusisha matumaini na matarajio. Tena, nikimnukuu Rais Nelson, “sheria za Mungu zinatokana na upendo Wake usio na mwisho kwetu na hamu Yake kwetu ya kuwa vyote tunavyoweza kuwa.”23

Kwa sababu Wanakupenda, Hawataki kukuacha wewe “kama ulivyo.” Kwa sababu Wanakupenda, Wanataka uwe na shangwe na mafanikio. Kwa sababu Wanakupenda, Wanakutaka utubu kwa sababu hiyo ndio njia ya furaha. Lakini ni uchaguzi wako—Wanaheshimu uhuru wako wa kuchagua. Unapaswa kuchagua Kuwapenda, Kuwatumikia, kutii amri Zao. Kisha wanaweza kwa wingi kukubariki wewe pamoja na kukupenda wewe.

Matarajio yao ya msingi kwetu ni kwamba na sisi tupende. “Yeye asiye na upendo hamjui Mungu; kwani Mungu ni upendo.”24 Kama Yohana alivyoandika, “Wapendwa, ikiwa Mungu alitupenda sisi, tunalazimika kupendana sisi kwa sisi.”25

Rais wa zamani wa Shule ya Msingi Joy D. Jones alieleza kwamba kama wanandoa vijana, yeye na mme wake waliitwa kutembelea na kuhudumia familia ambayo haikuwa ikihudhuria kanisani kwa miaka mingi. Ilifahamika kwa uwazi baada ya kuitembelea familia kuwa walikuwa hawatakiwi. Baada ya majaribio kadhaa ya kukatisha tamaa na yaliyoshindwa, na baada ya sala nyingi za dhati na kutafakari, Kaka na Dada Jones walipokea jibu la kwa nini kuhusu huduma yao kutoka katika aya hii ya Mafundisho na Maagano: “Na utampenda Bwana Mungu wako kwa moyo wako wote, kwa nguvu zako, akili, na uweza wako wote; na katika jina la Yesu Kristo utamtumikia yeye.26 Dada Jones alisema:

Tuligundua kwamba tulikuwa tukijaribu kwa uaminifu kuhudumia familia hii na kumtumikia askofu wetu, lakini tulipaswa kujiuliza kama kweli tulihudumu kwa sababu ya upendo kwa Bwana.

Tulianza kutazamia matembezi yetu na familia hii pendwa kwa sababu ya upendo wetu kwa Bwana (ona 1 Nefi 11:22). Tulikuwa tukifanya hivyo kwa ajili Yake. Yeye alifanya mahangaiko kuwa si mahangaiko tena. Baada ya miezi mingi ya kusimama nje ya mlango, familia ilianza kutukaribisha ndani. Hatimaye, tulikuwa na sala za mara kwa mara na mijadala ororo ya injili pamoja. Urafiki wa muda mrefu ukajengeka. Tulikuwa tukimwabudu na kumpenda Yeye kwa kuwapenda watoto Wake.”27

Katika kutambua kuwa Mungu anatupenda kwa dhati, kila mmoja anaweza kuuliza, “Ni kwa jinsi ipi nampenda Mungu? Anaweza kutegemea katika upendo wangu kama mimi ninavyotegemea katika Wake? Je, si matamanio mazuri kuishi ili Mungu aweze kutupenda si tu kutokana na madhaifu yetu lakini pia kwa sababu ya vile tunavyokuwa? Ndio, kwamba anaweza kusema kuhusu wewe na mimi kama Alivyosema kwa Hyrum Smith, kwa mfano, “Mimi, Bwana, nampenda kwa sababu ya uadilifu wa moyo wake.”28 Acha tukumbuke mawaidha ya upendo ya Yohana: “Kwani huu ni upendo wa Mungu, kwamba tushike amri zake: na amri zake sio mbaya.”29

Hakika, amri Zake sio mbaya—bali kinyume chake. Zinaonyesha njia ya uponyaji, furaha, amani, na shangwe. Baba yetu na Mkombozi wetu wametubariki na amri, na katika kutii amri Zao, tunahisi upendo Wao wa dhati kikamilifu na kwa wingi zaidi.30

Hili ni suluhisho kwa ajili ya ugomvi wetu usiokoma kila mara—upendo wa Mungu. Katika nyakati za dhahabu za historia ya Kitabu cha Mormoni kufuatia huduma ya Mwokozi, inaarifiwa kwamba “palikuwa hakuna mabishano katika nchi, kwa sababu ya upendo wa Mungu ambao ulikaa katika mioyo ya watu.”31 Kadiri tunavyojitahidi kuelekea Sayuni, kumbuka ahadi katika Ufunuo: “Wamebarikiwa wale wanaotii amri zake, kwamba waweze kuwa na haki katika mti wa uzima, na waweze kuingia ndani kupitia kwenye malango kuingia mji [mtakatifu].”32

Ninatoa ushuhuda juu ya uhalisia wa Baba yetu wa Mbinguni na Mwokozi wetu, Yesu Kristo, na upendo Wao endelevu, usiokufa. Katika Jina la Yesu Kristo, amina.