Mkutano Mkuu
Yesu Kristo Ni Nguvu ya Vijana
mkutano mkuu wa Oktoba 2022


Yesu Kristo Ni Nguvu ya Vijana

Weka tumaini lenu katika Yesu Kristo. Yeye atawaongoza katika njia sahihi. Yeye ni nguvu yenu.

Katika kujiandaa na ujumbe huu leo, nimehisi msukumo wenye nguvu kuzungumza na wasichana na wavulana.

Pia ninazungumza na wale ambao hapo awali walikuwa wadogo, hata na wale ambao hawakumbuki tena.

Na ninazungumza na wote ambao wanawapenda vijana wetu na wanaotaka wafanikiwe.

Kwa kizazi chipukizi, nina ujumbe mahususi kwenu kutoka kwa Mwokozi, Yesu Kristo.

Ujumbe wa Mwokozi Kwako

Rafiki zangu vijana wapendwa, kama Mwokozi angekuwepo hapa sasa hivi, Je, Yeye angesema nini kwenu?

Ninaamini angeanza kwa kuonyesha upendo Wake wa dhati kwenu. Angeusema kwa maneno, lakini pia ungetiririka kwa kasi—kutoka uwepo Wake—kwamba isingekuwa ya kutoeleweka, ukifika kwa kina mioyoni mwenu, ukijaza nafsi yenu!

Lakini bado, kwa sababu sote tu wadhaifu na tusio kamili, baadhi ya dukuduku zingekuja mawazoni mwenu. Mngeweza kukumbuka makosa mliyoyafanya, nyakati ambazo mlishindwa na jaribu, vitu ambavyo mngetamani msingevifanya—au ambavyo mngevifanya vizuri.

Mwokozi angehisi hilo, na naamini Angewahakikishia kwa maneno Aliyoyasema kwenye maandiko:

“Usiogope.”1

“Usiwe na shaka.”2

“Jipeni moyo.”3

“Msifadhaike mioyoni mwenu.”4

Sidhani kama Angehalalisha makosa yenu. Asingeyafumbia macho. Hapana, angewataka mtubu—kuziacha dhambi zenu, kubadilika, ili kwamba Awasamehe. Angewakumbusha kwamba miaka 2,000 iliyopita Alizichukua dhambi hizo juu Yake ili kwamba muweze kutubu. Hiyo ni sehemu ya Mpango wa furaha tuliopewa zawadi kutoka kwa Baba mpendwa wa Mbinguni.

Yesu angesema wazi kwamba maagano yenu na Yeye—yaliyofanywa wakati mnabatizwa na kufanywa upya kila mara mpokeapo sakramenti—huwapa muunganiko maalum na yeye. Muunganiko ambao maandiko yanaufafanua kama kuvikwa nira pamoja ili kwamba, kwa msaada Wake, muweze kubeba mzigo wowote.5

Ninaamini Mwokozi Yesu Kristo angewataka muone, kuhisi na kujua kwamba Yeye ni nguvu yenu. Kwamba kwa msaada Wake, kusiwe na mwisho wa kile mnachoweza kutimiza. Kwamba uwezekano wenu wa kuwa ni usio na mwisho. Angewataka mjione kama vile Awaonavyo. Na hiyo ni tofauti na jinsi ulimwengu uwaonavyo.

Mwokozi angetamka, kwa virai dhahiri, kwamba wewe ni binti au mwana wa Mungu Mwenyezi. Baba yako wa Mbinguni ni mtukufu zaidi ya wote katika ulimwengu, mwingi wa upendo, furaha, usafi, utakatifu, nuru, rehema na ukweli. Na siku moja Anataka ninyi mrithi vyote Alivyonavyo.6

Ni kwa sababu hii ninyi mko hapa duniani—kujifunza, kukua na kuendelea na kuwa vile ambavyo Baba yenu wa Mbinguni alikusudia muwe pale alipowaumba.

Ili kuwezesha hili, Alimtuma Yesu Kristo kuwa Mwokozi wenu. Hilo ni dhumuni la mpango Wake mkuu wa furaha, Kanisa Lake, ukuhani Wake, maandiko—na vingine vyote.

Hiyo ndiyo takdiri yenu. Hiyo ndiyo kesho yenu. Huo ni uchaguzi wenu!

Ukweli na Chaguzi

Kiini cha mpango wa Mungu kwa ajili ya furaha yenu ni katika nguvu yenu ya kufanya chaguzi.7 Bila shaka, Baba yenu wa Mbinguni hutaka mchague furaha ya milele pamoja Naye, na Atawasaidia kuifikia hilo, lakini kamwe Asingelazimisha hilo juu yenu.

Hivyo anawaruhusu mchague: Mwanga au kiza? Wema ua uovu? Furaha au huzuni? Uzima wa milele au kifo cha kiroho?8

Inaoneka kama uchaguzi rahisi, sivyo? Lakini kwa kiasi fulani, hapa duniani, huonekana ni mgumu kuliko ambavyo ungetakiwa kuwa.

Tatizo ni kwamba si mara zote tunaviona vitu kiuhalisia kama vile ambavyo vingetakiwa kuonekana. Mtume Paulo alilinganisha hili kama kuangalia “kwa kioo kwa njia ya fumbo.”9 Kuna mkanganyiko sana kwenye ulimwengu kuhusu kilicho chema na kiovu. Ukweli unapindishwa kufanya uovu kuonekana wema na wema kuonekana uovu.10

Lakini wakati kwa dhati mnapoutafuta ukweli—wa milele, ukweli usiobadilika—chaguzi zenu huwa dhahiri zaidi. Ndio, bado mna majaribu na changamoto. Vitu viovu bado hutokea. Mambo ya kukanganya. Mambo ya kuhofisha. Lakini bado mnaweza kustahimili wakati mnapojua ninyi ni akina nani, kwa nini mko hapa, na wakati mnapomwamini Mungu.

Hivyo basi wapi mnaupata ukweli?

Unapatikana katika injili ya Yesu Kristo. Na utimilifu wa injili hiyo unafundishwa katika Kanisa la Yesu Kristi la Watakatifu wa Siku za Mwisho.

Yesu Kristo alisema, “Mimi ndimi njia, na kweli, na uzima; mtu haji kwa Baba, ila kwa njia ya mimi.”11

Wakati una chaguzi muhimu za kufanya, Yesu Kristo na injili Yake ya urejesho ni uchaguzi bora zaidi. Unapokuwa na maswali, Yesu Kristo na injili Yake ya urejesho ni jibu bora zaidi. Unapohisi dhaifu, Yesu Kristo ni nguvu yako.

Yeye huwapa nguvu waliodhoofu; na kwa wale wahisio kukosa nguvu, Huwaongezea nguvu.

Wale ambao humngojea Bwana watafanywa upya kupitia nguvu Zake.12

Kwa Ajili ya Nguvu Kwa Vijana

Ili kuwasaidia kuipata Njia na kuwasaidia kufanya mafundisho ya Kristo kuwa mwongozo wenye ushawishi katika maisha yenu, Kanisa la Yesu Kristo la Watakatifu wa Siku za Mwisho limeandaa nyenzo mpya, iliyopitiwa upya ya Kwa Ajili ya Nguvu Kwa Vijana.

Picha
Muhtasari wa Kwa Ajili ya Nguvu kwa Vijana

Kwa zaidi ya miaka 50, Kwa Ajili ya Nguvu Kwa Vijana imekuwa mwongozo kwa vijana Watakatifu wa Siku za Mwisho. Mara zote naweka nakala kwenye mfuko wangu, na ninashiriki na watu ambao wanadadisi kuhusu viwango vyetu. Imefanywa upya na kutiwa nguvu ili kukidhi vyema changamoto na majaribu ya siku zetu. Toleo jipya la Kwa Ajili ya Nguvu Kwa Vijana sasa linapatikana katika lugha 50 tofauti na itakuwa msaada mkubwa kwa ajili ya kufanya chaguzi maishani mwenu. Litakuwa msaada mkubwa kwa ajili ya kufanya chaguzi maishani mwenu. Tafadhali likumbatieni kama ni lenu wenyewe na lishiriki na rafiki zenu.

Picha
Muhtasari wa Kwa Ajili ya Nguvu kwa Vijana

Toleo hili jipya la Kwa Ajili ya Nguvu Kwa Vijana limepewa kicha cha habari saidizi Mwongozo wa Kufanya Chaguzi.

Nikiweka wazi, mwongozi bora kushinda wote mnaoweza kuwa nao katika kufanya chaguzi ni Yesu Kristo. Yesu Kristo ni nguvu ya vijana.

Hivyo dhumuni la Kwa Ajili ya Nguvu kwa Vijana ni kuwaelekeza Kwake. Huwafundisha kuhusu kweli za milele za injili Yake iliyorejeshwa—kweli kuhusu ninyi ni nani, Yeye ni nani, na kile mnachoweza kutimiza kupitia nguvu Zake. Huwafundisha jinsi ya kufanya chaguzi njema kulingana na kweli hizo za milele.13

Pia ni muhimu kujua kile Kwa Ajili ya Nguvu Kwa Vijana haikifanyi. Haifanyi chaguzi kwa ajili yenu. Haiwapi “ndio au “hapana” kuhusu kila uchaguzi ambao mnaweza kukutana nao. Kwa Ajili ya Nguvu Kwa Vijana inafokasi kwenye msingi kwa ajili ya chaguzi zenu. Inafokasi kwenye maadili, kanuni na mafundisho badala ya kila tabia maalum.

Bwana, kupitia manabii Wake, kila mara amekuwa akituongoza katika mwelekeo huo. Anatusihi tuongeze uwezo [wetu] wa kiroho wa kupokea ufunuo.”14 Anatualika “Tumsikilize Yeye.”15 Anatuita kumfuata katika njia za haki na takatifu.16 Na tunajifunza katika njia sawa na hiyo kila wiki katika Njoo, Unifuate.

Nadhani mwongozo ungekupa orodha ndefu ya nguzo za kutovaa, maneno ya kutosema na video za kutoangalia. Lakini je, hiyo itasaidia kwenye kanisa la ulimwenguni kote? Je, njia hiyo kweli ingewaandaa ninyi kwa ajili ya maisha yote ya kama Kristo?

Joseph Smith alisema “Ninawafundisha kanuni sahihi, na wanajiongoza wenyewe.”17

Na mfalme Benjamini aliwaambia watu wake kwenye Kitabu cha Mormoni, “siwezi kuwaelezea vitu vyote ambavyo vinaweza kuwasababisha kutenda dhambi; kwani kuna njia nyingi na mbinu nyingi sana hata kwamba siwezi kuzihesabu.”18

Mfalme Benjamini aliendelea kwa kusema, “Lakini kwa haya naweza kuwaambia hivi, … mjichunge wenyewe, na mawazo yenu, na maneno yenu, na matendo yenu, na mfuate sheria za Mungu, na kuendelea kwa imani … kwa Bwana wetu, hadi mwisho wa maisha yenu.”19

Picha
Mwokozi Yesu Kristo

Je, ni vibaya kuwa na sheria? Hapana. Sote tunazihitaji kila siku. Lakini ni vibaya kufokasi kwenye sheria pekee badala ya kufokasi kwa Mwokozi. Mnahitaji kujua kwa nini na jinsi, na kisha kufikiria matokeo ya chaguzi zenu. Mnahitaji kuweka tumaini lenu kwa Yesu Kristo. Yeye atawaongoza katika njia sahihi. Yeye ni nguvu yenu.20

Nguvu ya Mafundisho ya Kweli

Kwa Ajili ya Nguvu Kwa Vijana ni shupavu katika kutangaza mafundisho ya Yesu Kristo. Ni shupavu kwenye kuwaalika kufanya chaguzi kulingana na mafundisho ya Kristo. Na ni shupavu kwenye kuelezea baraka Yesu Kristo huwaahidi wale wanaofuata Njia Yake.21

Rais Russell M. Nelson alifundisha: “Wakati hamu yako kuu inapokuwa kumwacha Mungu ashinde [maishani mwenu] … maamuzi mengi yanakuwa rahisi. … Matatizo mengi yanakuwa si matatizo tena! Unajua namna bora ya kujiandaa mwenyewe! Unajua nini cha kuangalia na kusoma, wapi pa kutumia muda wako, na nani wa kuhusiana naye. Unajua kile unachotaka kutimiza. Unajua ni aina gani ya mtu … unataka kuwa.”22

Kiwango cha Juu

Yesu Kristo ana viwango vya juu sana kwa wafuasi Wake. Na mwaliko wa dhati kutafuta mapenzi Yake na kuishi kulingana na kweli Zake ni kiwango cha juu kinachowezekana!

Maamuzi muhimu ya kimwili na kiroho hayapaswi kuwa tu ni mapendeleo binafsi, au kile ambacho ni kawaida kwetu au maarufu.23 Bwana hasemi, “Fanya utakavyo.”

Anasema, “Acha Mungu Ashinde.”

Anasema, “Njoo, unifuate.”24

Anasema, “Ishi katika njia takatifu, ya juu na ya kukubalika.”

Anasema, “Zishike amri Zangu.”

Yesu Kristo ni mfano wetu mkamilifu, na tunajitahidi kwa nguvu zetu zote kumfuata.

Rafiki zangu wapendwa, acha nirudie, kama Mwokozi angesimama hapa leo, Angeonyesha kwenu upendo Wake usio na mwisho, imani Yake yote kwenu. Angewaambia kuwa mnaweza kufanya hili. Mnaweza kujenga maisha ya shangwe na furaha kwa sababu Yesu Kristo ni nguvu yenu. Mnaweza kupata kujiamini, amani, usalama, furaha, na kuhisi kupendwa sasa na milele, kwa sababu mtapata yote katika Yesu Kristo, injili Yake, na kwenye Kanisa Lake.

Juu ya hili natoa ushuhuda wangu wa dhati kama Mtume wa Bwana Yesu Kristo na kuwaachia baraka za dhati kwa shukrani na upendo kwenu, katika jina la Yesu Kristo, amina.

Muhtasari

  1. Luka 5:10; 8:50; 12:7; Mafundisho na Maagano 38:15; 50:41; 98:1.

  2. Mafundisho na Maagano 6:36.

  3. Mathayo 14:27; Yohana 16:33; Mafundisho na Maagano 61:36; 68:6; 78:18.

  4. Yohana 14:1, 27.

  5. Ona Mathayo 11:28–30.

  6. Ona Mafundisho na Maagano 84:38.

  7. Ungeweza kusema mpango wa Baba uliasisiwa ili kukuruhusu kuonyesha matamanio yako kupitia chaguzi zako, ili kwamba uweze kupokea matokeo kamili ya kile unachotamani. Kama Mzee Dale G. Renlund alivyofundisha, “Lengo la Baba yetu wa Mbinguni katika malezi siyo kufanya watoto Wake kutenda kile kilicho sahihi; ni kufanya watoto Wake wachague kufanya kile kilicho sahihi na hatimaye kuwa kama Yeye.” (“Chagueni Hivi Leo,” Liahona, Nov. 2018, 104).

  8. Ona 2 Nefi 2:26–27.

  9. 1 Wakorintho 13:12.

  10. Ona Isaya 5:20.

  11. Yohana 14:6.

  12. Ona Isaya 40:29–31.

  13. Kama Watakatifu wa siku za Mwisho, mara nyingi tunajulikana kwa kile tukifanyacho na tusichofanya—tabia zetu. Hili linaweza kuwa zuri, lakini ni vizuri zaidi kujilikana kwa kile tukijuacho (kweli ambazo huongoza tabia zetu) na kwa nani tunayemjua (Mwokozi—na kwa jinsi gani upendo wetu Kwake huathiri tabia zetu).

  14. Russell M. Nelson, “Ufunuo kwa ajili ya Kanisa, Ufunuo kwa ajili ya Maisha Yetu,” Liahona,. Mei 2018, 96.

  15. Ona Russell M. Nelson, “Msikilize Yeye,” Liahona,, Mei 2020, 88–92.

  16. Njia mpya ijikitayo kwenye kanuni kwenye nyenzo mpya ya kwa Ajili ya Nguvu Kwa Vijana ina randana na mambo ya hivi karibuni yaliyotambulishwa na Kanisa la Mwokozi ikijumuisha Hubiri Injili Yangu, kuhudumu, mtaala wa Njoo, Unifuate , Programu ya Watoto na Vijana, Kufufundisha Katika Njia ya Mwokozi, na Kitabu cha Maelekezo. Bila shaka, Bwana anaujenga uwezo wetu wa kiroho. Anaonyesha uaminifu zaidi kwa watu Wake wa agano katika siku za mwisho.

  17. Teachings of Presidents of the Church: Joseph Smith (2007), 284.

  18. Mosia 4:29. Kwa njia fulani, hiki ndicho Mafarisayo wa wakati wa Yesu walijaribu kukifanya. Katika hamu yao ya kuwazuia watu kutovunja sheria, walitengeneza mamia ya sheria kulingana na uelewa wao wa maandiko matakatifu. Kile ambacho Mafarisayo walikosea ilikuwa kwamba walifikiri sheria zao zingewaokoa. Kisha, Mwokozi alipokuja, hawakumtambua.

  19. Mosia 4:30; msisitizo umeongezwa.

  20. Kitu kingine kwa nini njia mpya ijikitayo kwenye kanuni inahitajika hivi leo ni kwa kuongezeka utofauti wa tamaduni katika Kanisa la Bwana. Kanuni ni za milele na za ulimwenguni kote. Sheria maalum au utumiaji wa sheria hizo hufanya kazi vizuri katika baadhi ya sehemu na kutofanya kazi sehemu zingine. Ambacho hutuunganisha ni Yesu Kristo na kweli za milele Alizofundisha, hata kama matumizi maalum hutofautiana kwa muda mrefu na kwenye tamaduni. Hivyo tatizo la kuorodhesha nini cha kufanya na kutofanya si kwamba tu haitawekana lakini pia haiwezi kuwa endelevu. Tatizo ni kwamba huiondoa fokasi yetu kutoka kwenye Chanzo cha nguvu yetu, Mwokozi wetu, Yesu Kristo.

  21. Miaka mingi iliyopita, Rais Boyd K. Packer alizungumza maneno haya yenye nguvu: “mafundisho ya kweli, yakieleweka, hubadili mtazamo na tabia. Kujifunza mafundisho ya injili kutaboresha tabia haraka kuliko kujifunza kuhusu tabia kutakavyofanya (“Usiogope,” Liahona, May 2004, 79).

    Rais Ezra Taft Benson alifundisha ukweli sawa na huo: “Bwana hufanya kazi kuanzia ndani kwenda nje. Ulimwengu hufanya kazi kuanzia nje kwenda ndani. … Ulimwengu ungetengeneza tabia ya binadamu, lakini Kristo anaweza kubadili asili ya ubinadamu” (“Born of God,” Ensign, Nov. 1985, 6).

    Wakati Alma nabii kwenye Kitabu cha Mormoni alipoona uovu kwenye nchi inayomzunguka, aligeukia neno la Mungu kwa sababu alijua lilikuwa na “nguvu kwenye akili za watu kuliko upanga, au chochote kile, ambacho kimewahi kutokea kwao—kwa hivyo Alma alifikiri ilikuwa bora kwamba wangejaribu matokeo ya uwezo wa neno la Mungu” (Alma 31:5).

  22. Russell M. Nelson, “Acha Mungu Ashinde,” Liahona, Nov. 2020, 94. Rais Russell M. Nelson anatoa mfano wa njia hii wakati alipotufundisha kuhusu kuitunza siku ya Sabato: “Katika miaka ya ujana wangu, nilijifunza kazi za wengine ambazo ziliorodhesha vitu vya kufanya na vya kutofanya katika Sabato. Ilikuwa mpaka hapo baadaye ambapo nilijifunza kutoka kwenye maandiko kwamba mwenendo wangu na mtazamo wangu juu ya Sabato vilijumuisha ishara kati yangu na Baba yangu wa Mbinguni. Kwa uelewa huo, sikuhitaji tena orodha ya vya kufanya na kutofanya. Nilipohitaji kufanya uamuzi kama shughuli ilikuwa ya kufaa au kutofaa kwa ajili ya Sabato, nilijiuliza mwenyewe, ‘Ni ishara gani ninataka kumwonyesha Mungu?’ Swali hilo lilifanya chaguzi zangu kuhusu siku ya Sabato kuwa dhahiri zaidi” (“Sabato ni Siku ya Furaha,” Liahona, Mei 2015, 130).

  23. Mzee David A. Bednar alifundisha kwamba “kanuni ya utakatifu … hutusaidia kuangalia mbele zaidi ya mapendeleo na matamanio binafsi kwa kutoa mtazamo wa thamani wa ukweli wa milele wakati tunapopitia hali mbalimbali, changamoto, chaguzi na uzoefu wa maisha ya duniani” (“Kanuni za Injili Yangu,” Liahona, May 2021, 123–24).

  24. Luka 18:22.