2010
Kutafuta na Kupokea Ufunuo wa Kibinafsi
Aprili 2010


Ujumbe wa Mwalimu Mtembelezi, Aprili 2010

Kutafuta na Kupokea Ufunuo wa Kibinafsi

Funza maandiko na dondoo hizi, au, ikihitajika, kanuni ingine ambayo itabariki akina dada unaowatembelea. Toa ushuhuda wa fundisho hili. Alika wale unaowafundisha kushirikisha walichohisi na kujifundisha.

Ninaweza Vipi Kutafuta Ufunuo wa Kibinafsi?

“Tunajitayarisha kupokea ufunuo wa kibinafsi jinsi manabii wanavyofanya, kwa kusoma maandiko, kufunga, kuomba, na kujenga imani. Imani ndio ufunguo. Kumbuka matayarisho ya Joseph kwa Ono la Kwanza:

“‘Lakini mtu wa kwenu akipungukiwa na hekima, na aombe dua kwa Mungu. …

“Ila na aombe kwa imani, pasipo shaka yo yote.’”1

Mzee Robert D. Hales wa Jamii ya wale Mitume Kumi na Wawili.

“Maombi ni ufunguo wako wa kibinafsi wa mbinguni. Kifuli kimo upande wako wa pazia.

“Lakini hiyo sio yote. Kwa yule aliyefikiria kwamba ufunuo ungemiminika bila juhudi, Bwana alisema:

“Wewe hujaelewa; ulidhani ya kuwa Mimi nitakupatia tu wewe, wakati wewe hukutafakari isipokuwa kuniomba Mimi tu.

“‘Lakini tazama, ninakuambia, kwamba unalazimika kulichunguza katika akili yako; ndipo uniulize kama ni sahihi, na kama ni sahihi nitaufanya moyo wako uwake ndani yako; kwa njia hiyo, utahisi kuwa hiyo ni sahihi.’”2

Rais Boyd K. Packer, Rais wa Jamii ya Wale Mitume Kumi na wawili.

Ninaweza Vipi Kupokea Ufunuo wa Kibinafsi?

“Katika njia zake zinazojulikana, ufunuo au maongozi huja kwa uweza wa maneno au mawazo yaliyowasilishwa akilini (ona Enoshi 1:10; M&M 8:2–3), kwa kutaalamishwa ghafla (ona M&M 6:14–15), kwa hisia za kujenga au za kubomoa juu ya njia ya matendo iliopendekenzwa, au hata kwa utendaji wa msukumo, kama vile kwenye utendaji wa sanaa. Kama vile Rais Boyd K. Packer, … Rais wa Jamii ya Wale Mitume Kumi na Wawili, alivyoelezea, ‘Maongozi huja zaidi kama hisia kuliko sauti.’”3

Mzee Dallin H. Oaks wa Jamii ya Wale Mitume Kumi na Wawili.

“Hekalu ni nyumba ya kujifunza. Mengi ya maagizo yanayoelezwa hekaluni ni ya kiishara na hujifunzwa kwa Roho. Hii inamaanisha kwamba tunafundishwa kutoka juu. … Ufahamu wetu wa maana ya maagizo na maagano utaongezeka tunavyorudi kila mara hekaluni kwa nia ya kujifunza na kutafakari ukweli wa milele unaofunzwa. … Tuweze kufurahia nguvu za kiroho na ufunuo tunaopokea tunavyo hudhuria hekalu kila mara.”4

Silvia H. Allred, mshauri wa kwanza katika urais mkuu wa Muungano wa Usaidizi wa akina mama.

Muhtasari

  1. “Personal Revelation: The Teachings and Examples of the Prophets,” Liahona, Nov. 2007, 88.

  2. “Personal Revelation: The Gift, the Test, and the Promise,” Ensign, Nov. 1994, 59–60.

  3. “Eight Reasons for Revelation,” Liahona, Sept. 2004, 8.

  4. “Holy Temples, Sacred Covenants,” Liahona, Nov. 2008, 113, 114.

Misaada kwa Mafundisho ya Matembelezi

Kama mwalimu mtembelezi, unaweza kupokea maongozi ya Roho kulingana na mahitaji ya akina dada zako na jinsi ya kutimiza mahitaji hayo. Unavyofunza ujumbe huu, shirikisha, vilivyo, maongozi yoyote au usaidizi ambao umepokea kuhusu mafunzo ya matembelezi.

Kujitayarisha Kibinafsi

1 Samueli 3:10

1 Wafalme 19:11–12

Alma 5:46; 26:22

3 Nefi 19:19–23

M&M 8:2–3; 9:8–9; 88:63–64