2010
Urembo wa Kweli ni Nini?
Juni 2010


ujana

Urembo wa Kweli ni Nini?

Rais Monson anasema katika ujumbe huu, “Katika ulimwengu wetu, hulka ya maadili sana sana huonekana kuwa kitu cha pili baada ya urembo au haiba.” Wasichana wanaweza kuhangaika juu ya umbo lao, la wao ni kina nani na kile wanachoweza kuwa Fikiria mawazo haya juu ya urembo wa kweli kutoka kwa Mzee nb}G. Robbins wa wale Sabini:

  • Msichana ambaye sura inang’aa kwa furaha na wema inaonyesha urembo wa ndani.

  • Tabasamu ya wema kwa kweli ni urembo, kwa vile inaonyesha kwa njia ya halisi kabisa. Urembo huu wa kweli hauwezi kupakwa juu yake bali ni kipawa cha Roho.

  • Maadili ni ishara ya nje na mahitaji kwa urembo wa ndani.

  • Kama umevunjika moyo kwa sababu ya umbo lako, unaweza kusaidika kwa kujitazama kupitia macho ya wale wanaokupenda. Urembo uliojificha unaonekana na wale wakupendao unaweza kuwa kioo cha kujiendeleza kibinafsi.

  • Sampuli ya mwanamume ambaye mwanamke mwema anataka kuoa pia “hatazami” kama vile binadamu anavyotazama (ona 1 Samueli 16:7). Atavutiwa na urembo wa kweli ambao anaonyesha kutoka kwa moyo halisi na wenye furaha. Na hivyo ni sawa kwa msichana anayetafuta mvulana mwema.

  • Baba wetu wa Mbinguni anatarajia watoto wake wote wachague kile kilicho haki, ambacho ndicho njia ya pekee ya furaha ya milele na urembo wa ndani.

  • Kwa Bwana, hakuna ushindani. Wote wana nafasi sawa ya kuwa na umbo Lake kuchongwa katika sura zao (ona Alma 5:19). Hakuna urembo halisi.

Ili kusoma ujumbe wote, ona Lynn G. Robbins, “True Beauty,” New Era, Nov. 2008, 30. Wavulana wanaweza kupata ushauri sawa katika Erroll S. Phippen, “Ugly Duckling or Majestic Swan? Ni Juu Yenu,” Liahona, Oct. 2009, 36