2010
Kurumbiza wenye rangi Kijivu kwenye Mabawa Zao.
Juni 2010


Ujumbe wa Urais wa Kwanza, Juni 2010

Kurumbiza wenye rangi Kijivu kwenye Mabawa Yao

Karibu miaka sitini iliopita, wakati nilipokuwa nikihudumu kama askofu kijana, Kathleen McKee, mjane katika kata yangu, aliaga dunia. Miongoni mwa vitu vyake kulikuwa na kurumbiza wa kulea Wawili, walikuwa rangi jano halisi, walipeanwa kwa marafiki zake. Wa tatu, Billie, alikuwa na rangi kijivu ilioparara kwenye mabawa yake. Dada McKee alikuwa ameandika barua kwangu mimi: “Wewe na familia yako mtamtafutia nyumba huyu? Yeye sio mrembo, lakini nyimbo zake ni bora.”

Dada McKee alikuwa sana kama kurumbiza wake wa rangi njano mwenye rangi kijivu kwenye mabawa yake. Hakuwa amebarikwa na urembo, kipawa cha umbo, au kuheshimika kwa uzao. Hata hivyo nyimbo zake ziliwasaidia wengine kuwa upendeleo wa kubeba mzigo yao na kupata uwezo wa kubeba shida zao.

Ulimwengu umejaa kurumbiza wa rangi njano na rangi kijivu kwenye mabawa yao. Yakusikitisha ni kwamba ni wenye thamani wachache waliojifunza kuimba. Kati yao ni vijana ambao hawajui wao ni kina nani, kile wanachoweza kuwa, au hata wanachotaka kuwa; kile wanachotaka ni kuwa mtu tu. Wengine wamepinda migongo kwa uzee, mzigo ya taabu au wamejawa na shaka—wakiishi maisha ya kiwango cha chini ya uwezo wao.

Ili kuishi vyema, sharti tufanyinze uwezo wa kukabiliana na taabu kwa ujasiri, masikitiko kwa furaha, na ushindi kwa unyenyekevu. Unaweza kuuliza, “Je tunawezaje kuyafikia malengo haya?” Nami najibu, “Kwa kupata mwelekeo wa kweli wa kuwa sisi ni kina nani!” Sisi ni wana na mabinti wa Mungu aliye hai, katika umbo lake sisi tumeumbwa. Tafakari juu ya hayo: kuumbwa katika umbo la Mungu. Hatuwezi kwa kweli kushikilia uthibitisho huu bila ya kupata mhemko mpya wa nguvu na uwezo.

Katika ulimwengu wetu, hulka ya maadili sana sana hutelekezwa kuwa kitu cha pili baada ya urembo au haiba. Lakini kutoka zamani sana ushauri wa Bwana kwa nabii Samweli unarudia: “Bwana haangalii kama binadamu aangaliavyo; maana wanadamu huitazama sura ya nje, bali Bwana huutazama moyo” (1 Samweli 16:7).

Wakati Mwokozi alipokuwa akitafuta mtu wa imani, Hakumchagua kutoka kwa umati wa watu wenye kujidai wema, waliopatikana kila mara kwenye sinagogi. Hakika, alimwita kutoka miongoni mwa wavuvi wa Kapernaumu. Simioni aliye na shaka, asiye na elimu, mwenye haraka akawa Petro, Mtume wa imani. Kurumbiza wa njano mwenye rangi kijivu kwenye mabawa yake alihitimu katika imani kuu na upendo wa kudumu wa Bwana

Wakati Mwokozi alichagua mmisionari wa ari na nguvu, hakumpata miongoni mwa watetezi wake bali kati ya washindani Wake. Saulo mtesaji akawa Paulo mhamasishaji.

Mkombozi aliwachagua watu wasio kamili kufundisha njia ya ukamilifu Alifanya hivyo wakati huo. Anafanya hivyo sasa—hata kurumbiza wa njano wenye rangi kijivu kwenye mabawa yao. Anakuita wewe na mimi kumhudumia Yeye hapa chini. Msimamo wetu sharti uwe kamili. Na katika mapambano yetu, tutakapojikwaa, acha tusihi: “Tuongoze sisi, ewe tuongoze sisi, Mfinyazi mkuu wa watu.”1

Ombi langu ni kwamba tutafuata mfano wa Mtu wa Galilaya, ambaye angepatikana akichanganyikana na maskini, waliodhalilishwa, waliodhulumiwa, na walioteseka. Na wimbo wa kweli uje kutoka mioyoni mwetu tunapofanya hivyo.

Muhtasari

  1. “Fight Song,” Yonkers High School.

Kufundisha kutoka kwa Ujumbe Huu

Unapofunza … , mara nyingi kuna usaidizi kwa kuwezesha wanafunzi kutafuta au kusikiliza kitu mahususi”(Teaching, No Greater Call [1999], 55). Ili kusaidia wanafamilia kufahamu ujumbe wa Rais Monson, fikiria juu ya kuwauliza wajitayarishe kushirikisha kile walichojifunza baada ya kuusoma ujumbe huu pamoja. Alika kila mmoja kushirikisha kile anachohisi ni jambo muhimu katika makala haya. Malizia kwa kutoa ushuhuda juu ya ujumbe wa Rais Monson.

Kufunza neno la Mungu, kama linavyotolewa kupitia manabii Wake, unaweza kuwa na mvuto wa nguvu katika maisha ya wale unaowafunza (ona Teaching, No Greater Call 50). Rais Monson ananena kwamba kuna nguvu na uwezo katika kujua sisi tu watoto wa Mungu. Baada ya kusoma nakala, uliza familia kushirikisha kinacho wakumbusha wao ni kina nani.