2010
Kuhusu Mambo yaliyo Muhimu Zaidi
Novemba 2010


Ujumbe wa Mafundisho, NOVEMBA 2010

Kuhusu Mambo Yaliyo Muhimu Zaidi

Ikiwa Maisha na kasi yake na dhiki nyingi yamefanya kuwa vigumu kwako kufurahi, basi huenda wakati huu ni wakati bora wa kuangazia mambo yaliyo muhimu zaidi.

Ni jambo la ajabu jinsi tunavyoweza kujifunza kuhusu maisha kwa kujifunza maumbile. Kwa mfano, wanasayansi wanaweza kuona mizunguko ya miti na kukisia kuhusu hali ya hewa na ukuaji mamia na hata maelfu ya miaka iliyopita. Mojawapo ya mambo tunayoweza kujifunza kwa kuchunguza ukuaji wa miti ni kuwa katika misimu ambapo hali ni bora, miti humea katika kiwango cha kawaida. Hata hivyo, katika misimu ambapo hali ya ukuaji si bora, basi miti hupunguza kasi yao ya kumea na kutenga nguvu zao kwa haja za kimsingi za kuishi.

Hadi hapa, baadhi yenu mnaweza kuwa mnafikiri, “haya yote ni sawa, lakini yanahusiana vipi na kuendesha ndege?” Haya, hebu niwaeleze.

Umewahi kuwa katika ndege inapopitia msukosuko? Sababu ya kawaida ya msukosuko ni mabadiliko ya ghafla katika miendo wa hewa inayosababisha ndege kuyumba, kwenda mrama na kubungurika. Ingawa ndege zimejengwa kustahimili msukosuko kuliko chochote unachoweza kukumbana nayo katika usafiri wa kawaida wa ndege, bado inaweza kuleta dhiki kwa abiria.

Unadhani marubani hufanya nini wanapokumbana na msukosuko? Mwanafunzi rubani anaweza kufikiri kuwa kuongeza kasi ni mbinu bora kwa sababu kutampisha kwenye msukosuko haraka. Lakini hiyo yaweza kuwa kitendo kisichofaa kufanya. Marubani watalaamu wanafahamu kuwa kuna kasi inayofaa kupitia kwenye msukosuko ili kudidimiza athari za msukosuko. Na mara nyingi, hiyo humaanisha kupunguza kasi yako. Kanuni hii pia hutumika katika vizuizi vya mwendo katika barabara.

Hivyo basi, ni nasaha bora kupunguza kasi kidogo, kuimarisha mwendo na kulenga mambo muhimu wakati wa kukumbana na hali hatari.

Kasi ya Maisha ya Kisasa

Hili ni fundisho rahisi lakini muhimu. Inaweza kuonekana kuwa jambo la kimantiki mifano ya miti au misukosuko ikitumiwa, lakini ni jambo la kushangaza kuwa ni rahisi kupuuza somo hili inapofikia kutumia kanuni hizi katika maisha yetu ya kila siku. Wakati viwango vya dhiki vinavyoongezeka, wakati mateso yanapoonekana, wakati maafa yanapotukia, kila mara tunajaribu kuendeleza kasi hii ama hata kuizidisha, tukifikiri huenda kasi yetu inapozidi ndipo tutakapokuwa salama zaidi.

Mojawapo ya tabia ya maisha ya kisasa inaonekana kuwa tunasonga katika kasi inayoendelea kuongezeka bila kujali misukosuko au vikwazo.

Hebu tuseme ukweli ni rahisi kuwa na shughuli nyingi Sote tunaweza kufikiria orodha ya majukumu ambayo yatashinda ratiba zetu. Wengine hata wanaaweza kufikiria kuwa thamani yao ya kibinafsi hutegemea orodha ya ratiba zao. Wanafurika nafasi za wazi za wakati wao na orodha za mikutano, na shughuli ndogo hata nyakati za dhiki na uchovu. Kwa sababu wanaleta utata usiofaa katika maisha yao, mara nyingi wanahisi kuongezeka kwa kuvunjika moyo, furaha iliyodidimia, na ukosefu wa maana katika maisha yao.

Inasemekana kuwa kila adili ikizidishwa kupita kiasi huwa uovu. Kuratibu siku zetu kupita kiasi bila shaka hutuhitimisha kwa haya. Wakati hutimia wakati matukio muhimu huwa mizigo mizito.

Je! Suluhisho ni nini?

Wenye hekima huelewa na kutumia mafundisho ya miviringo ya miti na misukosuko ya hewani. Wanakinza majaribu ya kutegwa katika kasi ya kutia wazimu ya maisha ya kila siku. Wanafuata wasia “kuna ubora maishani zaidi ya kuongeza kasi.”1 Kwa ufupi, wanalenga mambo yaliyo muhimu zaidi.

Mzee Dallin H. Oaks katika mkutano mkuu hivi karibuni alifundisha, “Ni sharti tuache mambo mengine mema ili kuchagua mengine yaliyo bora au mema zaidi kwa sababu yanakuza imani katika Bwana Yesu Kristo, na kuimarisha familia zetu.”2

Kutafuta mambo mema zaidi bila shaka huongoza kwa kanuni za kimsingi za injili ya Yesu Kristo, kweli zenye wema na wepesi zilizofunuliwa kwetu na Baba wa Mbinguni wa milele, anayefahamu yote na anayetujali. Mafundisho na kanuni hizi za kimsingi, ingawa nyepesi kiasi cha kueleweka na mtoto, huoa majibu kwa maswali magumu zaidi maishani.

Kuna wema na udhahiri unaotokana na wepesi ambao wakati mwingine hatufurahii katika kiu yetu ya suluhisho zenye utata.

Kwa mfano, haikuwa muda mrefu baada ya wataalamu wanaanga kuzunguka dunia ndipo walipogundua kuwa kalamu za wino hazikufanya kazi angani. Na watu werevu mara moja wakaanza kazi ya kutafuta suluhisho. Ilichukua maelfu ya masaa na mamillioni ya pesa, lakini hatimaye, walitengeneza kalamu ambayo ingeandika kila mahali, katika hali yoyote ya joto na karibu katika kila uso. Lakini wanaanga wao walifanya nini hadi shida hiyo ilipotatuliwa? Ila, walitumia penseli.

Leonardo Da Vinci amenulukiwa kusema kwamba “wepesi ni utata uliozidi.”2 Tunapoangalia kanuni za kimsingi za mpango wa furaha, mpango wa wokovu, tunaweza kutambua na kutambua wepesi wake na ukwasi na wema wa hekima ya BabaWetu wa Mbinguni. Kisha, kubadili njia zetu kwa ajili ya njia zake ni mwanzo wa hekima yetu.

Uwezo wa Mambo ya Kimsingi

Hadithi husimuliwa kwamba mkufunzi maarufu wa kandanda Vince Lombardi alikuwa na kawaida aliyofanya katika siku ya kwanza ya mazoezi. Angeshikilia mpira, kuwaonyesha wachezaji ambao wamekuwa wakicheza mpira mingi na kusema, “Mabwana, …huu ni mpira ya kandanda!” Alizungumza kuhusu ukubwa wake, umbo lake, jinsi ilivyopigwa teke, au kubebwa au kupashwa. Aliichukua timu nje kwenye uwanja mtupu na kusema, “Huu ni uwanja wa kandanda.” Aliwatembeza akiwaeleza ukubwa, umbo, sheria na jinsi mchezo ulivyochezwa.4

Mkufunzi huyu alijua kuwa hata kwa hawa wachezaji wenye tajiiriba na hata timu, ingeweza tu kuwa maarifa kwa kuelewa mambo ya kimsingi. Wangetumia muda wao kujizoesha hali ngumu za mchezo, lakini hadi pale walipoelewa mambo ya kimsingi ya mchezo, hawangeweza kuwa timu ya mabingwa.

Nafikiri wengi wetu huelewa kisilika umuhimu wa mambo ya kimsingi. Ni vile tu wakati mwingine tunapotoshwa mawazo na vitu vingi yanayoonekana kutamanisha zaidi.

Vifaa vilivyochapishwa na vianzo vya aina mbali mbali ya vyombo vya habari, vifaa vya kielektroniki vina manufaa vikitumiwa vyema vinaweza kuwa ya vipotoshi vya kuumiza na vyumba visivyo na huruma vyenye upweke.

Ila, kati ya sauti na chaguo zisizo na kifani, Mtu mnyenyekevu wa Galili anasema na mikono iliyonyoshwa, akingoja. Wake ni ujumbe mwepesi “Njooni mnifuate.”5 Na hasemi kwa kipaza sauti chenye nguvu, lakini kwa sauti ndogo tulivu.6 Ni rahisi kwa ujumbe wa kimsingi wa injili kupotea kati ya wingi wa habari inayotupiga kutoka kila mahali.

Maandiko matakatifu na maneno ya manabii wanaoishi yanatilia mkazo kanuni na mafundhisho ya kimsingi ya injili. Sababu yetu kurudia kanuni hizi za kimsingi, kwa mafundisho masafi ni kwa sababu ni njia za kweli zenye maana kamilifu. Ni milango ya uzoefu wa umuhimu wa ndani ambayo kwa njia nyingine ingekuwa zaidi ya uwezo wetu kuelewa. Kanuni hizi nyepesi ndiyo ufunguo wa kuishi kwa upatanifu kati ya Mungu na mtu. Ni funguo za kufungua madirisha ya mbinguni. Zinatuongoza kwenye amani, furaha na kuelewa kuwa Baba wa Mbinguni amewaahidi wana wake wanaomsikia na kumtii.

Ndugu na dada zangu wapendwa, tungefanya vyema kupunguza kasi kidogo na kuenda kwa kasi ya wastani kulingana na hali zetu, kulenga yaliyo muhimu kuinua macho yetu na kwa kweli kuona vitu vilivyo muhimu zaidi. Tukumbuke kanuni za kimsingi ambazo Baba yetu wa Mbinguni amewapa watoto wake zitakazoimarisha msingi wa maisha ya muda yenye utajiri na mazao yaliyojaa ahadi ya furaha ya milele. Zitatufundisha “kufanya mambo yote kwa kiasi … kwa hekima na mpango; kwani si vyema kwamba mtu akimbie kuliko alivyo na nguvu. Lakini ni lazima kwamba tuwe waangalifu na kwayo … kushinda zawadi.”7

Akina ndugu na dada, kufanya kwa uangalifu mambo yaliyo muhimu zaidi kutatuongoza kwa Mwokozi wa ulimwengu. Hii ndiyo maana tunazungumza kuhusu Kristo, tunafurahia katika Kristo, tunahubiri kuhusu Kristo, tunatoa unabii kumhusu Kristo, … ili watoto wetu wajue asili ya kutegemea kwa msamaha wa dhambi zao.8 Katika utata, kuchanganyikiwa na kasi ya maisha ya kisasa, hii ndiyo “njia bora zaidi.”9

Hivyo basi, mambo ya kimsingi ni yapi?

Tunapomgeukia Baba yetu wa Mbinguni na kutafuta hekima yake kuhusu mambo yaliyo muhimu zaidi, tunajifunza tena na tena umuhimu wa mahusiano manne muhimu: na Mungu wetu, na familia zetu, na Watu wenzetu, na sisi wenyewe. Tunapohakiki maisha yetu na mioyo yenye hiari, tutaona mahali ambapo tumepotoka kutoka kwa njia bora zaidi. Macho ya akili zetu yatafunuliwa, na tutatambua yanayohitajika kufanywa ili kutakasa mioyo yetu na kulenga upya maisha yetu.

Kwanza uhusiano wetu na Mungu ni mtakatifu na muhimu. Sisi ni watoto wake wa kiroho. Yeye ni Baba wetu. Ana haja na furaha yetu. Tunapomtafuta, tunapojifunza kutoka kwa mwanawe Yesu Kristo, tunapofungua mioyo yetu kwa ushawishi wa Roho Mtakatifu, maisha yetu yatakuwa imara na salama. Tunapata amani zaidi, furaha, na ukamilifu tunapotoa mema yetu ili kuishi kulingana na mpango wa Mungu wa maisha ya milele na kutii amri zake.

Tunaboresha maisha yetu na Baba wetu wa Mbinguni kwa kujifunza kutokana naye, kwa kuwasiliana naye, kwa kutubu dhambi zetu, na kumfuata Yesu Kristo, kwani “hakuna ajaye kwa Baba ila kwa [Kristo].”10 Ili kuimarisha uhusiano wetu na Mungu, tunahitaji wakati wenye maana naye pekee. Kwa kulenga kwa upole katika maombi ya kila siku ya kibinafsi na kusoma maandiko, na kuazimia kila mara kustahili kuwa na sifu ya hekalu ya sasa. Haya yatakuwa uwekezaji wenye hekima wa wakati na juhudi zetu za kumkaribia Baba wetu wa Mbinguni. Hebu na tutii mwaliko katika Zaburi “Acheni, mjue kuwa Mimi ni Mungu.”11

Uhusiano wa pili wa muhimu ni wa familia zetu. Kwa kuwa “hapana fanaka itakayofidia kushindwa”12 hapa, ni lazima tuzipe familia zetu kipaumbele. Tunajenga mahusiano yenye kina na upendo na familia kwa kufanya mambo mepesi pamoja, kama vile chakula cha familia, mikutano ya jioni familia nyumbani. Katika uhusiano wa familia upendo kwa hakika ni wakati bora. Kutenga wakati kwa ajili ya kila mmoja ni muhimu kwa upatanifu nyumbani. Tunazungumza na kila mmoja badala ya kuzungumza kuhusu kila mmoja. Tunajifunza kutoka kwa kila mmoja, na tunatambua tofauti zetu na pia usawa wetu. Tunaimarisha mfungo wa kiungu na kila mmoja tunapomjongea Mungu pamoja kwa kupitia maombi ya familia.

Uhusiano wa tatu muhimu ni ule ya watu wenzetu. Tunajenga uhusiano huu mtu mmoja kwa wakati, kwa kuwa wenye kuhisi mahitaji ya wengine, kuwahudumia, na kupeana wakati na vipaji vyetu. Nilivutiwa sana na dada mmoja ambaye alikuwa amekumbwa na changammoto za umri na ugonjwa, lakini akaamua kuwa ingawa hangefanya mengi, angesikiliza, Kwa hivyo kila juma aliwatafuta watu waliooneka kuwa na dhiki na kuvunjika mioyo, na akatumia wakati wake nao, akiwasikiliza. Je! Ni baraka ya jinsi gani aliyokuwa katika maisha ya watu wengi.

Uhusiano wa nne muhimu ni wetu sisi wenyewe. Unaweza kuonekana jambo la ajabu kuwa na uhusiano na sisi wenyewe, lakini tunakuwa nao. Watu wengine hawajipendi. Wanajikosoa na kujidunisha mchana kutwa hadi wanapoanza kujichukia. Hebu nipendekeze kuwa upunguze kasi na kuchukua muda wa ziada ili kujifahamu vyema. Tembea katika asili, tazama jua likichomoza, furahia maumbaji ya Mungu, tafakari kweli za Injili ya urejesho, na kutafuta maana yao kwako binafsi. Jifunze kujiona jinsi Baba wa Mbinguni anavyokuona. Kama Binti au Mwana wake mwenye thamani.

Furahia Injili takatifu

Ndugu na dada, hebu na tuwe wenye hekima Hebu na tugeukie miito ya mafundisho ya injili ya urejesho ya Yesu Kristo Hebu na tushiriki kwa wepesi na udhahiri wake. Mbingu zi wazi tena. Injili ya Yesu Kristo imo tena duniani, na kweli zake nyepesi ni asili ya furaha tele!

Ndugu na dada, kwa kweli tuna sababu kubwa ya kufurahi. Ikiwa Maisha na kasi yake na dhiki nyingi imefanya kuwa vigumu kwako kufurahi, basi huenda wakati huu ni wakati bora wa kuangazia mambo yaliyo muhimu zaidi.

Nguvu haziji kwa matendo ya kuyumbayumba, bali kwa kutulia katika msingi imara wa kweli na mwanga. Inatokana na kuweka nathari yetu na juhudi kwa mambo ya kimsingi ya injili ya urejesho ya Yesu Kristo. Inatokana na kuwa makini kwa mambo ya kiungu yaliyo muhimu kwa yote.

Hebu tufanye maisha yetu kuwa mepesi. Tufanye mabadiliko yanayohitajika na kulenga maisha yetu upya kwa uzuri wa ndani wa mambo mepesi, njia nyenyekevu ya ufuasi wa Kristo njia inayoongoza nyakati zote kwenye maisha yenye maana. Kwa haya naomba nikiwaachia baraka zangu, katika jina takatifu la Yesu Kristo, amina.

Muhtasari

  1. Mahatma Gandhi, in Larry Chang, Wisdom for the Soul (2006), 356.

  2. Dallin H. Oaks, “Good, Better, Best,” Liahona, Nov. 2007, 107.

  3. Leonardo da Vinci, in John Cook, comp., The Book of Positive Quotations, 2nd ed. (1993), 262.

  4. Vince Lombardi, in Donald T. Phillips, Run to Win: Vince Lombardi on Coaching and Leadership (2001), 92.

  5. Luke 18:22.

  6. See 1 Kings 19:12.

  7. Mosia 4:27.

  8. 2 Nephi 25:26.

  9. 1 Corinthians 12:31; Ether 12:11.

  10. Yohana 14:6.

  11. Psalm 46:10.

  12. J. E. McCulloch, Home, The Savior of Civilization (1924), 42: see also Conference Report, Apr. 1935, 116.