2011
Baraka za Fungu la Kumi
Juni 2011


Ujumbe wa Urais wa Kwanza, Juni 2011

Baraka za Fungu la Kumi

Madhumuni ya Mungu katika kutupatia sisi amri ni kutubariki. Anataka kutupa uzima wa milele, karama iliyo kuu kati ya karama Zake zote (Tazama M&M 14:7). Ili kupokea karama ya kuishi pamoja na yeye milele katika familia katika ufalme wa selestia, sharti tuweze kuishi sheria za huo ufalme (ona M&M 88:22).

Ametupa amri katika maisha haya ili kutusaidia kukuza huu uwezo. Sheria ya fungu la kumi ni mojawapo ya hizo amri za matayarisho. Sheria hiyo ni kwamba tutoe kwa Bwana kumi kwa mia ya mazao yetu. Ni rahisi kutosha kwamba hata mtoto anaweza kuelewa. Nimeshapata kuwaona watoto wakimpatia askofu bahasha ya fungu la kumi ambayo ilikuwa kumi kwa mia ya sarafu ambazo wamefanyia kazi.

Mojawapo wa baraka ambazo zinatokana na kutoa fungu la kumi kamili ni kukuza imani na kuishi hata sheria za juu. Ili kuishi katika ufalme wa selestia, ni sharti tuishi sheria ya kujitolea. Hapo ni lazima tuwe tanaweza kuhisi kwamba vyovyote tulivyo na chochote tulichonacho ni cha Mungu.

Kuna angalao njia tatu ambazo kutoa fungu la kumi katika maisha haya hututayarisha sisi ili kuhisi kile tunachohitaji ili kuhisi kupokea kipawa cha uzima wa milele.

Kwanza, wakati tunapotoa fungu la kumi letu kwa Kanisa, Baba yetu wa Mbinguni humimina baraka juu yetu. Mtu yeyote ambaye anayetoa fungu la kumi kila mara anajua kwamba hii ni kweli. Baraka zinakuwa wakati mwengine ni za kiroho na wakati mwengine kimwili. Zinapeanmwa katika wakati wa Bwana na kulingana na kile anachojua ni bora kwetu.

Jinsi hizi baraka zinapokuja, imani yetu huongezeka kwamba Mungu ndiye chanzo cha kila kitu ambacho ni chema katika maisha yetu. Inakuwa rahisi kuona kwamba kujitolea kwa urahisi kutambua ukweli kwamba viumbe vyote vya Mungu ni Vyake. Kunatufanya sisi kuhisi shukrani kwamba Yeye anauliza asili mia 10 ya kile ambacho ametupatia sisi. Kwa hivyo tunajitayarisha vyema kuishi sheria ya kujitolea wakati tutaulizwa kuiishi.

Pili, sisi sote ambao tumetoa fungu la kumi kila mara tunahisi imani kuu katika kumuomba Mungu kile sisi na familia zetu tunahitaji. Ameahadi baraka hata kuu kuliko zile tumepokea wakati tumekuwa waaminfu kwa agano letu la kutoa fungu la kumi letu (ona Malaki 3:10). Kwa hivyo mojwapo wa baraka kuu za fungu la kumi ni imani ya kile ambacho siku za usoni zitakavyo kuwa. Bila kujali hali zetu zinaweza kuwa vipi, mambo yatakuwa mema kwetu. Tunapoweka ahadi zetu, Yeye ataweka Zake. Hisia ya imani ni mojawapo ya baraka kuu za kutoa fungu la kumi kamili. Wale ambao wameweka amri ya fungu la kumi wanaweza kushuhudia kwamba baraka ya imani ni hakika na ya thamani.

Tatu, wale wanaotoa fungu la kumi huhisi ongezeko la upendo wao kwa Mungu na watoto wote wa Mungu. Ongezeko hilo la upendo hutokana na ufahamu wa jinsi Baba hutumia fungu la kumi tunalotoa kubariki watu katika ulimwengu huu na kwa umilele.

Kupitia watumishi wake walio na mamlaka, Yeye hutumia fungu la kumi kwa ungalifu mkubwa. Mtoa fungu la kumi humusaidia Bwana kujenga mahekalu, pale ambapo familia hufunganishwa kwa milele. Mtoa fungu la kumi humsaidia Yeye kueneza injili kwa watu kila mahali. Mtoa fungu la kumi humsaidia Yeye kupunguza njaa na kuteseka katika njia Yake mwenyewe kupitia watumishi Wake. Yeyote wa hawa watumishi wanaweza kuelezea jinsi upendo hongezeka kwa sababu ya fungu la kumi limetumika kuwabariki watu. Na vivyo hivyo mtoa fungu la kumi mwaminifu.

Udhibitishaji wa fungu la kumi katika miezi ya siku za usoni. Naomba sasa wewe na familia yako mtaanza sasa kupanga na kujitayarisha ili kuhitimu kwa baraka ambazo Mungu humimina kwa wale wote ambao wanaotangaza Kwake kwamba wamekuwa watoa fungu la kumi kamili.

Kufundisha kutoka kwa Ujumbe huu

  • Wakati mwengine njia bora ya kufunza kanuni fulani ili kuionyesha (ona Teaching, No Greater Call [1999], 164). Fikiria kumuuliza mwanafamilia kuonyesha kile kumi kwa mia inamaanisha. Anaweza kwa kuonyesha kwa kutenganisha kitu kimoja kutoka kwa kundi la vitu kumi. Kutamatisha, fikiria kumwalika mwanafamilia aonyeshe jinsi ya kujanza cheti cha fungu la kumi.

  • “Wale wanaofunza watafaidika kutoka kwa ushirika wa kila mmoja” Teaching, No Greater Call, 63). Waalike wanafamilia kushiriki kile wanachoamini Rais Eyring alichomaanisha kwa usemi “kuhisi kile tunachohitaji kuhisi ili kupokea kipawa cha uzima wa milele.” Fikiria juu ya kuzungumza njia tatu ambazo kwazo kutoa fungu la kumi kunatutayarisha kuhisi kile tunachohitaji kuhisi ili kupokea baraka za Mungu.