2012
Kwa Nini Tunahitaji Manabii?
Machi 2012


Ujumbe wa Urais wa Kwanza, Mechi 2012

Kwa Nini Tunahitaji Manabii?

Kwa sababu Baba wa Mbinguni anawapenda Watoto Wake, Yeye hajawaacha wao kupitia katika haya maisha ya muda bila maelekezo na mwongozo. Mafundisho ya Baba yetu wa Mbinguni si ya kawaida, yanayoweza kutabirika, aina ya chapisho muundo ambao unaweza kupata kwenye vitabu katika duka la vitabu. Ni ya hekima ya kiumbe cha selestia kilicho na uwezo wote, anayejua yote ambaye anawapenda watoto Wake. Kilicho ndani ya maneno Yake ni ficho la mida—muhimu kwa furaha ya maisha haya na katika ulimwengu ujao.

Baba wa Mbinguni ufunua hekima hii kwa Watoto wake ulimwenguni kupitia watumishi Wake manabii (ona Amosi 3:7). Kutoka siku za Adamu, Mungu amezungumza na watoto Wake kupitia wafunuaji wateule ambao wana jukumu la kufunua mapenzi na ushauri Wake kwa wengine. Manabii ni waalimu wenye maongozi na daima ni mashahidi maalumu wa Yesu Kristo (ona M&M 107:23). Manabii hawaongei tu kwa watu wa wakati wao, bali pia huongea na watu katika nyakati zote. Sauti zao hutoa mwangwi katika karne kama ushuhuda wa mapenzi ya Mungu kwa watoto Wake.

Siku hizi sio tofauti na miaka iliyopita. Bwana hawapendi watu wa siku zetu kidogo kushinda siku zilizopita. Mmojawapo wa jumbe tukufu za Urejesho wa Kanisa la Yesu Kristo ni kwamba Mungu anaendela kuongea na watoto Wake! Yeye hajafichwa katika mbingu bali anaongea leo kama Alivyofanya katika siku za kale.

Mengi ya yale Bwana amefunua kwa manabii Wake yamedhamiriwa kuzuia huzuni kwetu kama watu na kama jamii. Mungu anapoongea, Yeye hufanya hivyo kuwafunza, kuwatakasa, na kuwaonya watoto Wake, Watu na Jamii zinapopuuza maelekezo ya Baba yao wa Mbinguni, wanafanya hivyo na kujihatarisha na majaribu, mateso, na shida.

Mungu anawapenda watoto Wake wote. Hio ndio sababu Yeye anatusihi sana sisi kupitia manabii Wake. Kama vile tunavyowatakia mema wapendwa wetu, Baba wa Mbinguni anatutakia mema sisi. Hio ndio sababu maelekezo yake ni muhimu sana na wakati mwingine ni ya dharura. Hio ndio sababu Yeye hajatuacha sisi siku hizi bali anaendelea kufunua mapenzi Yake kwetu kupitia manabii Wake. Hatima yetu na ya ulimwengu wetu inatengemea kusikia kwetu na kulishika neno lililofunuliwa la Mungu kwa watoto Wake.

Maelekezo ya thamani kuu ya Mungu kwa binadamu yanapatikana katika Biblia, Kitabu cha Mormoni, Mafundisho na Maagano, na Lulu ya Thamani Kuu. Zaidi ya hayo, Bwana huongea nasi kupitia watumishi Wake, kama vile atakavyofanya tena katika mkutano mkuu ujao.

Kwa wale wote wanaoshangaa kama kitu kama hicho kinawezekana—wanaoweza kuuliza, “Inawezekana kwamba Mungu anaongea nasi leo?—kwa moyo wangu wote mimi nawaalika “njooni na muone” (Yohana 1:46). Soma neno la Mungu kama linavyopatikana katika maandiko. Sikiliza mkutano mkuu kwa sikio lenye kupendelea kusikia sauti ya Mungu inayotolewa kupitia manabii Wake wa siku za mwisho. Njooni, msikie, na mwone kwa mioyo yenu! Kwani kama unatafuta “kwa moyo mwaminifu, dhamira halisi, mkiwa na imani karika Kristo, [Mungu] ataonyesha ukweli wake kwenu, kwa nguvu za Roho Mtakatifu” (Moroni 10:4). Kwa, na kupitia nguvu hizi, mimi najua kwamba Yesu Kristo yu hai na anaongoza Kanisa Lake kupitia nabii aishie, hata Rais Thomas S. Monson.

Kina ndugu na dada, Mungu anaongea nasi leo. Na Yeye anataka kwamba watoto Wake wote wasikie na kutii sauti Yake. Tunapofanya hivyo, Bwana atatubariki na kutulinda sana, katika maisha haya na kote katika ulimwengu ujao.